TTCL na huduma ya internet | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TTCL na huduma ya internet

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tiba, Feb 4, 2010.

 1. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Naleta mbele yenu kisa hiki ambacho kimenipata mimi mwenyewe. Ukipita mitaa mingi ya Dar Es Salaam kuna mabango kila mahali yanayoonyesha kwamba TTCL wanatoa huduma ya internet. Pamoja na kwamba kuna makampuni mengi sasa hivi yanatoa huduma hii, mimi nilishawishika kuwajaribu TTCL kwa maana nzima ya kulipiga tafu shirika letu la umma pamoja na kuonywa na rafiki yangu mmoja kwamba TTCL ni wasumbufu na kwamba itanichukua muda mrefu kupata huduma hiyo. Lakini kinachoendelea kwa sasa huwezi kuamini kwamba ndio watu wale wale walitumia mamilioni ya shillingi kuweka matangazo kwamba wanatoa huduma hii. Tarehe 21 December 2009 nilikwenda pale TTCL Ubungo plaza na kuulizia uwezekano wa kuunganishiwa internet nyumbani kwangu. Nilipewa fomu nikajaza na kuonyesha nitachukua package ipi kati ya zilizokuwepo baada ya kupewa maelezo na kushauriwa nitumie landline ili niweze kupata huduma nzuri zaidi. Niliwafahamisha kuwa ninayo landline nyumbani kwangu na hivyo nikaambiwa atatumwa fundi kuja kuangalia eneo. Ni kweli fundi alikuja na baadae walinitaka nikalipie. Nililipia connection fee ya Tshs. 25,000 na baada ya hapo ikawa kimya. Baada ya kuwafuatilia nikataarifiwa kuwa siwezi kupewa huduma hiyo kwa sasa kwa kuwa wameishiwa modem. Nikaulizia uwezekano wa kununua modem yangu mwenyewe wakasema sawa ninunue halafu niwataarifu waje kufunga. Pamoja na kulipia hiyo gharama ya internet ya mwezi mmoja tarehe 21 January 2010, mpaka leo fundi hajaja kuniunganishia hiyo huduma. Ukienda pale ofisini kwao wanakwambia fundi alikuja hakukuta mtu nyumbani, ukimpigia fundi simu kuuliza anadai alikuwa busy sana bado hajaja!!! (Contradiction)

  Swali langu ni je hali hii imeishamkuta mtu mwingine au imetokea kwa bahati mbaya kwangu tu? Je hawa jama zetu kwa mtindo huu ni kweli wamejiandaa kufanya biashara kwa ushindani? Je wakubwa huko makao makuu wanajua madudu yanayofanywa na watendaji wao hawa?

  Natabiri kufa na kuzikwa kwa TTCL muda si mrefu endapo hali hii haikutokea kwa bahati mbaya tu.

  Tiba
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,618
  Likes Received: 23,708
  Trophy Points: 280
  Pole, That is one isolated case, TTCL broadband is the fastest, cheapest na most reliable!. 40,000/= per month, you enjoy unlimited wireless 24/7.
   
 3. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,768
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Mkuu pole, hujafa hujaumbika. kwani wewe ni mgeni na utaratibu wetu ukitaka huduma ? hasa kwenye mashirika yetu haya? hebu tafakari kuna mahali UNAKOSEA.
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,174
  Likes Received: 3,218
  Trophy Points: 280
  nilienda kuulizia kuhusu huduma zao kwanza customer care ilikuwa mbovu, hovyo kabisa.....na pia nilijibiwa kwa wakati huo modem hazipo nijaribu kupitia baada ya mwezi...hawa ndugu zetu naona wako mahututi na huu ushindani wa biashara nawatakia kila la kheri
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,768
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  mkuu nadhani hiyo unazungumzia ya 45.000 per month ambayo ni shared 1/50. sidhani kama inaweza kuwa as fast kama ya kwako mwenyewe ambayo kuna package za kuanzia 1G kwa 30,000 kwa mwezi
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Feb 4, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Pole ndugu Tiba. Naona ya kwako ni isolated case zaidi, sehemu nyinginezo huduma zao ni relatively good, isipokuwa kwa upande wa customer care, they have some problems. Nakushauri uende kwenye matawi mengine hapo Dar ili upresent issue yake. Otherwise wapigie customer care ili wakusaidie.
   
 7. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,951
  Likes Received: 1,399
  Trophy Points: 280
  Nipo nawe kabisa Kaizer hapa. Mimi nimechukua package ya 2G kwa elfu 60 kwa mwezi. Ni huduma bomba si kawaida.

  Ni kweli kuna usumbufu kidogo katika kuunganishwa. Tena hapo Ubungo Plaza wanamtegemea fundi mmoja kijana anaitwa Ngasapa. Hana makuu, ila tu mizunguko ya mijini ni mingi.
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  Buchanan sijui kama umemsaidia umesema upande wa customer care ndiyo mbovu mwishoni ukamwambia awapigie tena hao hao customer care ili wamsaidie which is which!
   
 9. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,141
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Fair explanations, we are together.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Feb 4, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,210
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Ni kweli inaonekana kama sijamsaidia lakini sivyo. Mimi kuna siku nilijibiwa vibaya sana na mtu wa customer care lakini nilipopiga tena alipokea mwingine aliyenihudumia vizuri sana! Ndio maana nilisema kuwa kuna "some problems" kwenye customer care!
   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,235
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 0
  Siku nyingine wakikusumbua au kampuni yoyote ya mawasiliano niandikie pm
   
 12. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,681
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Tiba pole,
  Nakushauri uende TTCL pale nyerere road katibu na kamapuni ya sigara, wale jamaa wanasikiliza shida za wateja na kufanyia mteja kitu anachohitaji. Mimi nimenunua modem EC226 sikupata usumbufu sasa nakula internet kama kawa. Yawezekana hilo ni tatizo la mtu mmoja lakini sio sera ya TTCL
   
 13. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hiyo modem EC226 inagharimu kiasi gani kwa sasa mkuu?
   
 14. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kaizer,

  Wapi nakosea Mzee nisaidie!!!!

  Tiba
   
 15. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Mkuu Pasco,

  Ndio maana nimeuliza kama kuna mwingine aliishakutana na hadha hii au is just an isolated case kama ulivyosema!!!.

  Tiba
   
 16. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Kama mambo yenyewe ndio hayo kwa nini walijitangaza kwa nguvu kutoa huduma hii? Wana sababu gani za msingi za kuishiwa na modem? Wanaye qualified supplies director?

  Tiba
   
 17. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Mkuu Buchanan,

  Nakushukuru kwa ushauri wako. Itabidi sasa nikamwone meneja wa kanda ambaye nimeambiwa anakaa ofisi ya Osterbay. Hao customer care nikiwapigia wananipa taarifa za uongo mara fundi amekuja hajakuta mtu, mara walimkuta mtu lakini amekataa kuwafubgulia mlango mambo ambayo ni uongo mtupu!!!

  Tiba
   
 18. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160

  Mkuu The Invicible,

  Na mimi nimeomba na kulipia hiyo package ya 2GB kwa Tshs. 60,000 kwa mwezi lakini ndiyo hivyo bado sijabahatika kufungiwa hiyo huduma pamoja na kununua modema yangu mwenyewe.

  Tiba
   
 19. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160

  Mkuu Fungwe,

  Asante kwa ushauri ingawaje umesema hiyo sera ya TTCL (OF COURSE SIO) lakini pamoja na hiyo isolated case yangu kama mnavyosema, inakuwaje hawana moden mpaka wateja tununue wenyewe? Suala hapa kwa mtindo huu hawa jamaa wamejiandaa kushindana kweli kwenye ili soko huria? Nakumbuka wakati naomba nifungiwe line ya simu some 10 years ago, it did not take that much long pamoja na kwamba they were only service provider available. Iweje leo wakati watoa huduma za internet wako kibao?

  Tiba
   
 20. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #20
  Feb 4, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 826
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Nilikua mteja wa Sasatel nikaachananao bada ya kuhesabu MB nikaona zinakwend aupesi hata kama nimefungua webpage isiyo na picha wala video. nimeamua kuachana nao.

  Swali langu, mimi natumia sana Net kucheki shows kweney Youtube, sija jua ni mtandao gani utakau kidogo afadhali maana hizo 1GB ni najidanganya , je Africa online wao wako vipi?,Thanx
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...