TTCL Hatarini kupoteza soko

Dive

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
868
1,424
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Tanzania imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) liko katika hatari kubwa zaidi ya kunyang’anywa soko na makampuni mengine ya simu kutokana na upungufu wa mtaji.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Februari 16, 2022 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jerry Silaa wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli zilizofanywa katika kipindi cha Januari 2021 hadi Februari 2022.

Mbali na TTCL kamati hiyo imebaini upungufu wa mitaji katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

Amesema TTCL lipo katika hatari kubwa zaidi ya kunyang’anywa soko kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na kampuni nyingine za simu hapa nchini hasa Vodacom, Airtel, Tigo na Halotel.

Silaa amesema ili TTCl iweze kufanya uwekezaji mkubwa linatakiwa kuwa na mtaji wa Dola za Kimarekani milioni 752 lakini hadi sasa shirika hilo lina mtaji wa Sh370.465 bilioni tu.

“Serikali iangalie namna bora zaidi ya kuongeza mtaji wa Shirika hili kwa kuwapatia kiasi cha Sh360.09 bilioni kilichoombwa na Shirika kwa sasa ili Shirika liweze kufanya uwekezaji wenye tija,”amesema.

Kwa upande wa TPDC umeendelea kuwa hasi ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/20, mtaji huo uliongezeka kutoka mtaji hasi wa Sh 354.8 bilioni mwaka 2018/19 hadi mtaji hasi wa Sh331.2 bilioni mwaka wa fedha 2019/20 ambapo ni ongezeko la asilimia 6.7.

Amesema licha ya ukweli kwamba, mtaji wa TPDC umeendelea kuwa hasi kutokana na hasara iliyopatikana katika mwaka wa fedha 2014/15 ambayo ilisababishwa na mkopo wa Dola za Kimarekani bilioni 1.194 zilizotolewa kwa ajii ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. “Mkopo huo uliingizwa kwenye hesabu za Shirika na hivyo kusababisha Shirika kupata hasara ya Sh257.2 bilioni iliyotokana na matumizi ya gharama za riba na mikopo na hasara ya kubadilisha fedha (exchange loss) kutokana na mkopo husika,”amesema.

Amesema kwa kiasi kikubwa mkopo huu ndiyo umesababisha mtaji wa Shirika kuwa hasi pamoja na faida ambayo Shirika limekuwa likipata katika mwaka wa fedha 2019/20 na 2018/19.

Amesema pia katika TADB imebaini changamoto ya upungufu wa mtaji katika benki ambapo benki ilianza na mtaji wa Sh60 bilioni ingawa mtaji ulioidhinishwa (Authorized Capital) ni Sh800 bilioni.

“Ili kukamilisha mtaji ulioidhinishwa, Serikali iliahidi kutoa katika bajeti yake ya kila mwaka kiasi cha Sh100 bilioni. Kamati inatambua juhudi mbalimbali za Serikali katika kuiwezesha Benki hii kwa kuipatia kiasi cha Sh208 bilioni, mnamo Disemba 2021,”amesema.

Amesema kamati hiyo inashauri kuwa jitihada za Serikali ziendelee ili TADB iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi
 
Back
Top Bottom