TTCL Fanyeni haya ili muwe Kampuni yenye ushindani wa kibiashara

Jan 9, 2020
54
95
1. Kuboresha na kusambaza minara kwa wingi.
Jitoeni kwenye ROAMING ya Tigo, jengeni minara yenu.

2. Kufungua matawi au ofisi zao.
Vuta picha pale Kibaha, ofisi ipo sehemu moja tu. Je huko vijijini itakuwaje?

3.Ondoa wazee, wekeni vijana.
Wazee wameshachoka wapo zama za Ujima(Communalism) wakati vijana tupo dunia ya 3.

4.Fumua menejementi yote.
Wekeni watu wenye uchungu na hiyo kampuni.

Nyingine mtaongezea
 
Hawa jamaa walikuwa sharp sana mwaka 2016 kuja 2018 ila sasa wamebadili vifurushi mwaka huu 2020.
Nani kawashauri wabadili?
 
Wataalamu wa biashara, miundombinu na wengineo naomba kufahamu. Je Nini kifanyike ili TTCL iwe kampuni ya kiushindani kama ilivyo Tigo, Voda na Halotel?

Maana sahivi wanajikongoja na muda si mrefu wataporomoka kama zamani.
 
Hawa jamaa walikuwa sharp sana mwaka 2016 kuja 2018 ila sasa wamebadili vifurushi mwaka huu 2020.
Watapata akili tu. Watapoteza wateja mpka waisome number. Watu walifata ttcla kwa ajili ya internet wao wanapunguza vifurushi vya internet wanajaza madakika. Ya nini sasa. Nimetoa line nimeweka kwenye kabati mimi
 
Wataalamu wa biashara, miundombinu na wengineo naomba kufahamu
Je Nini kifanyike ili TTCL iwe kampuni ya kiushindani kama ilivyo Tigo, Voda na Halotel?
Maana sahivi wanajikongoja na muda si mrefu wataporomoka kama zamani.
TTCL haijawahi kufanya kazi kibiashara.
Hili ni shirika la serikali.
Wapate faida au wapate hasara, mshahara upo pale pale na pengine na bonasi juu, tofauti na wafanya kazi sekta binafsi. Kushindwa kwa mashirika ya umma ni mentality mbovu tu.

Pale hakuna motivation yoyote kufanya kazi kibiashara. Kampuni ya kibiashara inatazama shimo kule mbele, ukizembea unaangukia shimoni, na motivation ni kujihakikishia kuwa kesho watakuwa hai kibiashara.

Katika sekta binafsi si tu unajihakikishia kuwa kesho uko hai bali ufanye vizuri zaidi ili ujijengee amana ya akiba utakazoweza kuzitumia siku za biashara mbaya.

Na hii model ya vision always works.
 
Kama kwa watoto walioko chuo mnawapa ofa ya bei ya juu kiasi hiki katika vifurushi vyenu, kwakweli hamtoboi. yaani huyu ni anayepata ofa ya chuo sasa vipi ambaye hana ofa hiyo?
Screenshot_20200804-113220.jpg
 
1. Kuboresha na kusambaza minara kwa wingi.
Jitoeni kwenye ROAMING ya Tigo, jengeni minara yenu.

2. Kufungua matawi au ofisi zao.
Vuta picha pale Kibaha, ofisi ipo sehemu moja tu. Je huko vijijini itakuwaje?

3.Ondoa wazee, wekeni vijana.
Wazee wameshachoka wapo zama za Ujima(Communalism) wakati vijana tupo dunia ya 3.......

Unamaanisha nini dunia ya tatu?
 
Wataalamu wa biashara, miundombinu na wengineo naomba kufahamu. Je Nini kifanyike ili TTCL iwe kampuni ya kiushindani kama ilivyo Tigo, Voda na Halotel?

Maana sahivi wanajikongoja na muda si mrefu wataporomoka kama zamani.
Magari yawe kifaa cha kazi siyo starehe... Engineers wapewe magari kwa ajili ya ku-atend downtimes za minara....

Kuwe na distribution ya towers kwa site Engineers
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom