TTCL CEO awe Kevin Twisa

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,842
8,231
Kwa mara ya kwanza leo nimefurahia uteuzi uliofanywa na Waziri Chiligati kumteua ndugu Nehemia kuongoza NHC, na kwa kuangalia kwa sasa TTCL inakoenda inahitaji kijana msomi ambaye amekubuhu katika mambo ya mawasiliano

Kwa kuangalia haraka Kevin Twisa anasimama kifua mbele ukiangalia alikoitoa Tigo na sasa Zain nimeona kuna umuhimu kwa shirika kama TTCL likaongozwa na mtu kama Kevin.

Pia kwa maoni yangu TTCL ingejigawa kuwe na kampuni mbili tofauti mpja iwe ni kwa ajili ya simu za mezani tu na ingine iwe ni ya simu za viganjani pamoja na mambo ya data na hiyo kampuni ya simu za mkononi ndio Kevin ashike usukani.

Pia kuna kijana mwingine mahiri anaitwa Ali naye alikuwa Tigo na sasa yuko Zain hao ni vijana wa kitanzania ambao naamini wanaweza kuibadili TTCL ambayo pamoja na kuwa na kila kitu na ipo mahala pote Tanzania imelala usingizi wa doro, hayo ni maoni yangu,wengine wanakaribishhwa kuchangia hasa kuhusiana na mashirika yetu ya umma
 
Ushabiki wakijinga. A marketer who is good at FMCG cant make a good CEO. Wake up. What a cheap campaign. Prick!
 
Sarcastic!
 
Ushabiki wakijinga. A marketer who is good at FMCG cant make a good CEO. Wake up. What a cheap campaign. Prick!

Hivi Bill Gates na Steven Job wamesomea nini na katika level gani?

Nilishaona Wayahudi wakiwa maboss wa makampuni yenye capital kubwa kuzidi hilo shirika letu. Au una kichwa cha kuongoza na kuwa na washauri wazuri au huna kichwa hata kama una elimu uliyoipata kwa sababu UNA KARIRI sana.

Anyway, simfahamu huyo bwana. Ila kama kweli kazisaidia TIGO na Zein kuwa hapo zilipo, basi kajitahidi. Ila ZEIN walikuwa wanalalamikiwa hapa kuwa wanahuduma nzuri za internet ila watu hawafahamu. Ovyo kabisaa........
 
Kwa jinsi ninavyomsikia na kumuona huyo bwana mdogo yeye nadhani ni mtaalamu wa matangazo ya biashara, TTCL kama state owned Telecommunication company inahitaji zaidi ya hicho alicho nacho Kelvin mtamchanganya bure kijana wa watu. Pale kuna mambo ikiwemo siasa za nchi na utashi wa viongozi wa kitaifa waliopo kuweza kuperform unavyofikiria. Hali ya uongozi iliyopitiwa na inayoendelea ya kampuni hiyo ya umma ilifika wakati haikuwa tofauti sana na Railways unayoifahamu.

Naamini wadau wengine watachangia zaidi.
 
Kwakuwa TTCL ni kampuni ambayo mauzo yake yanategemea namna utakavyoweza kuwashawishi watu kuitumia technologia yao, si vema kumchukua mtu ambaye persee hana knowledge ya technologia hiyo.

Kuna tetesi kuwa makampuni makubwa ya technologia kama General Motors yame suffer sana na kufanya vibaya kibiashara kwasababu ya kuwaweka watu kwenye vyeo vya juu ambao hawakuwa na background ya technologia zao.

Wataalamu hao walikuwa makini zaidi kuhakikisha balance sheet zao zinaonekana vizuri bila kuangalia pia kama technogia iliyopo inakidhi matakwa ya market kwa kipindi hicho.
 
Nadhani kwa sasa TTCL haihitaji Marketer bali inamuhitaji Strategist. Kwa huyo bwana nadhani ni mtu wa masoko zaidi na siyo kwa General Strategic management!
 
Huko alikopita amejitahidi kuintroduce products & services mpya as a Marketer. Lakini being a CEO, haswa wa shirika nyeti la umma kama TTCL tena kwa hali yake ya sasa kujumlisha competition iliyopo kwenye industry, ain't think that Twisa really fits for the post.
 
Ni corruption, greedy na kila kitu na pia kama anaweza basi itakuwa safi sana kwake yeye binafsi
 
Muulize au jiulize kwa nini ameshuswa cheo zain juzix2? anajua kucheza na media ila sio productive
 
Hii ni takataka, haya mambo ndiyo yaliyotumfanya tuchague raisi asiekuwa na sifa yoyote kiutendaji sasa tunalia!
Tusipokuwa makini kuna siku tutaongozwa na Kingwendu!
 
TTCL needs strategical management and inhouse campaign to change the atititudes of employees and their bosses. Kampuni utadhani ni ya kiserikali, they have no customer service, no dedication na mambo mengine mengi ya kuudhi.

Sasa hivi they only control 1.2 of the mobile phone industry. Its needs a full company overhaul na sio Kevin Twisa, Banana Zorro or Bill Gates kubadilika
 
kwenye mashirika ya umma kama hao kina kevin twisser wako kibao ila mzee ni kubaniwa na waliowakuta, mashirika kama hayo watu kibao watu wana interest, attempt zozote za kustreamline operations zitakuingizza ktk matatizo, hao akina kevin twisser wangekuepo ktk mashirika ya umma tusingewasikia mjomba! engineer wa bot aliyelipua bomu (whitsle blower) hivi karibuni yeye alikataa kuunga mkono juhudi za kina liyumba za kuongeza garama za jengo, uliskia kilichompata, alihamishiwa mwanza na akaambiwa kwanza ni incompitent kwani pale engineering mlimani ktk degree yake alipata lower second kwa iyo hana akili za kupima kama garama ni sahihi au la na akatupwa mwanza akale samaki sijui ndio akili zirudi!

kifupi mashirika yote ya umma yanaitaji major overhaul, kuanzia system ya kuajiri hasahasa then twende kwenye operations.
 
Me naunga mkono Twisa kupewa TTCL. Huu ni mtazamo hasi ambao tunakuwa nao zidi ya Vijana wetu, ambao binafsi naupinga sana.
Naamini kama jina la Nehemia lingeletwa hapa kabla hajateuliwa, tungesikia kejelia hizi hizi anazopata Twisa.
Kwa haraka haraka kampuni yoyote ambayo iko katika ushindani, ili ifanikiwe ni lazima CEO awe na uelewa wa hali ya juu wa mambo ya masoko, na hapo ndo jina la Twisa linapokuja.
Lazma tukubali kuwa Twisa ni mahiri kwenye mambo ya masoko dispite the fact kuwa ni DJ.

Yeye kuwa DJ kwangu sio tatizo, kwani he does that for the love of the Music, ni sawa wewe unaependa mpira na mara moja moja ukawa unaenda uwanjani kucheza wakati una kazi ya maana kabisa.

TTCL ili iweze kutoka hapo ilipo ni lazima iajiri mtaalamu wa mambo ya masoko kama Twisa, na sio kuajiri CEO engineer au Accountant. That won't take them anywhere!
Na katika hii industry ya communication hamna marketer alieprove anaweza kumzidi Twisa, he is the shinning star on that Industry. I do believe he will take TTCL to where it's suppossed to be.

Naunga mkono hoja!
 
Back
Top Bottom