mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,855
- 8,253
Kwa mara ya kwanza leo nimefurahia uteuzi uliofanywa na Waziri Chiligati kumteua ndugu Nehemia kuongoza NHC, na kwa kuangalia kwa sasa TTCL inakoenda inahitaji kijana msomi ambaye amekubuhu katika mambo ya mawasiliano
Kwa kuangalia haraka Kevin Twisa anasimama kifua mbele ukiangalia alikoitoa Tigo na sasa Zain nimeona kuna umuhimu kwa shirika kama TTCL likaongozwa na mtu kama Kevin.
Pia kwa maoni yangu TTCL ingejigawa kuwe na kampuni mbili tofauti mpja iwe ni kwa ajili ya simu za mezani tu na ingine iwe ni ya simu za viganjani pamoja na mambo ya data na hiyo kampuni ya simu za mkononi ndio Kevin ashike usukani.
Pia kuna kijana mwingine mahiri anaitwa Ali naye alikuwa Tigo na sasa yuko Zain hao ni vijana wa kitanzania ambao naamini wanaweza kuibadili TTCL ambayo pamoja na kuwa na kila kitu na ipo mahala pote Tanzania imelala usingizi wa doro, hayo ni maoni yangu,wengine wanakaribishhwa kuchangia hasa kuhusiana na mashirika yetu ya umma