TTCL, Benki ya Posta, ATC, TRL taswira ya ujamaa

Mbaya kiasi gani? Mimi nilibadili dola kwenda Tshs kwa 2370 kwenye bureau moja Kariakoo, baada ya siku kadhaa nikaenda kubadili tena ika ndio zikawa zimefungwa nikabadiki benki ta posta kwa rate ya 2330 nikaona sio mbaya sana maana nilitegemea ingeshushwa hadi 2200 huko..
Duh..mkuu tofauti ya Tsh.40 unaiona ndogo kwa $ 1?? Ungekuwa na $ 10000 ungekuwa umepoteza kiasi gani!?? Halafu hao wenye bureau de change,usd wengine walikuwa hawapati hiyo Tsh.40 km faida. Labda kwa pesa za nchi zingine ambazo hazina mzunguko mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio ndogo, ila 2330 sio ndogo pia kwani miezi miwili iliyopita nilikuwa nabadili kwa 2200,
 
Serikali ya awamu ya Tano inatengeneza mazingira ya ujamaa kwa nchi yetu na kututoa kwenye mixed economy.

Mashirika hayo hapo Juu yanafufuliwa kwa kasi lakini ufufuaji wake si wa ushindani bali ni kupitia kuwadhibiti washindani wao kwa kutumia dola ili wateja wahamie kwenye mashirika hayo.

Ni wazo zuri kuwa na mashirika ya umma ila ni vyema kuwa na mashirika ya umma yaliyoibuka na kukuwa kupitia ushindani wa wazi. Ukibebwa na kulipiwa kila kitu hauwezi kuwa imara bali unaandaliwa kuwa mtegemezi.

Mashirika ya simu yanaandamwa kuilinda TTCL ambayo ubunifu wake ni mdogo Sana lakini pia pesa za uendeshaji hazipangwi na kundi la wataalamu ndani ya shirika bali Hadi wapate ruzuku kutoka serikalini. Watendaji siyo wabunifu kwani ajira zake zinafuata mfumo wa serikali unaozingatia vyeti bila kujali uzalishaji unaotokana na huyo mwenye vyeti husika. Mishahara yake si yakuvutia kulingana na sekta binafsi.

Bank ya posta naona inajitanua na kuanza kuwa mbadilishaji fedha mkuu lakini ukiwaangalia watoa huduma katika benki hii hawawezi kuchukua kasi iliyokuwa inafanywa na bureau de change zinazofungwa kwa kasi. Badala ya kuisadia benki hii tumezalisha biashara haramu ya ubadilishaji fedha. Lakini pia huduma nyingine za kibenki hazileti ushindani kwa sabababu shirika halipo kibiashara

Fast jet imekufa kupisha ATC wakati mashirika haya yote yalipaswa kufanya kazi pamoja kwa sababu yanalipa kodi

Pamoja na Nia nzuri ya serikali ninaona Kama tunatumia fedha nyingi kwenye mashirika haya lakini akija mtawala mwingine atapuuza juhudi za mashirika haya na kuja na mipango mipya na hivyo serikali kuendelea kupata hasara.

Kama serikali ya Sasa imeweza kuua miradi mingi iliyoanzishwa na hawamu zilizopita ikiwemo mradi wa DART na Shirika la utangazaji basi lazima tuchukue taadhari kuweka mafedha kwenye mashirika ya umma na kuyajengea uwezo wa ushindani yajiendeshe yenyewe.

Kutumia dola kuboresha mashirika hakuyajengi yakawa imara bali yanapaswa kuacha yasimamame kushindana na sekta binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
good analysis bro hii kitu imeshiba. watakwambia unatumiwa na mabeberu
 
Nadharia,umezoea "debate" ya "capitalism is better than socialism" discuss.Hakuna uchumi imara bila udhibiti wa sekta za kiuchumi,pamoja na umuhimu wa sekta binafsi serikali kuwa na mkono ni muhimu.Leo hizi benki kubwa duniani kama Citi,Stanchart, Barclays ni mali ya serikali za magharibi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani kwenye list yako naomba uwaongeze na TBC na CCM
(i) TBC - Naona ving'amuzi vingi vinazuiwa kuonesha channel za ndani ya nchi isipokua TBC tu, hii inaaka kuhalalisha kua TBC ibaki channel pekee ya kuangalia taarifa zao za habari
(ii) CCM - Naona vyama vya upinzani vinakandamizwa na kuhujumiwa kwa kila namna adi kupelekea kununuliwa kwa wanachama wake ili tu kuvidhohofisha na kubaki na chama kimoja cha CCM

Naomba waongeze na hao ili roho yangu itulie
 
Ujamaa ni mfumo wa maisha ulioshindwa popote pale duniani ambako wamejaribu kuutumia. Ujamaa upo kinyume na hulka ya mwanadamu. Wale wanaotaka kuturudisha huko wamejiandaa kushindwa kabla ya kufanikiwa kutufikisha kwenye huu ujamaa-mamboleo wao.
Duh umenikumbusha nilipokuwa form 3 wakati huo tuna somo la Siasa shuleni. Nilisimama kuchangia darasani na kumwambia mwalimu kuwa ujamaa ni kinyume na hulka za binaadamu - aisee mwalimu wangu, mzee akaro, alipaniki sana karobu aniadhibu.
 
Back
Top Bottom