kinjumbi one
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 1,694
- 2,132
TTCL bado hawajaweza kujipanga na kupambana na movement za soko huria. Nasema hivyo kwasababu mwaka 2010 walikuja kujaribu kuleta line za simu ya mkononi, na vocha zake kama ilivyo mitandao mengine na code yao wao walitumia 073. Ilikua poa na vocha zao zikaanza kuuzika kwa kiasi flani.
Lakini pamoja na uzuri huo, ila kuna kasoro kubwa waliifanya hima kwa makusudi au ndo ujuaji sana, hata sijui. Ni kwamba line yao ilikua huwezi kuweka katika simu yeyote ispokua katika simu yao tu yani ilikulazimu kama unataka line ya TTCL, ni lazima ununue na simu yao. Hii ilipunguza morali au kushusha kabisa muamko wa mtandao wao, kama ilivyoshuka Sasatel.
Leo wamekuja tena na matangazo kemkem na hashtag ya "rudi nyumbani kumenoga". Kwa kiasi flani wapo poa na watu wameanza kuwaelewa. Ila sasa kasoro yao kubwa ile ya miaka nane iliyopita wameileta tena, eti line yao haisomi katika simu za kawaida hadi iwe ya 4g au kwa uchache zipo za 3g, lile tabaka la 2010 wamelileta tena, lakini kwa namna nyingine.
Kwa maoni yangu hata iweje kwa style hii ya kutoa bidhaa za ajabuajabu huku wenyewe wakijiona ndo wanafanya jambo la maana hawataweza kutoboa, yani kuwashinda akina Voda, Tigo na Airtel bado ni ndoto za mchana.
Nawasilisha.