Ttb yatunukiwa tuzo kwa kupambana na malaria

Aug 15, 2011
21
45
Na: Geofrey Tengeneza
BODI ya Utalii Tanzania TTB imekabidhiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kupambana na ugonjwa wa Malaria hapa nchini.
Tukio la kukabidhi vyeti hivyo ilifanyika hivi karibuni katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa kutokomeza Malaria nchini unaoitwa “ Malaria safe”. Mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya afya na Ustawi wa jamii alikuwa ni Waziri MKuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda ambaye pia alikabidhi tuzo hizo kwa taasisi kadhaa ikiwemo Bodi ya Utalii kutokana na michango wake katika mapambano dhidi ya Malaria nchini.
Oktoba mwaka jana Bodi ya utalii Tanzania kwa kushirikiana na NGO ya kimarekani iitwayo John Hopkins University na Shirikisho la vyama vya kitalii nchini TCT walizindua kampeni maalumu katika hoteli kwa watalii na wafanyakazi katika sekta ya utalii hapa nchini.
 

Attachments

  • Tuzo 2.jpg
    Tuzo 2.jpg
    88.1 KB · Views: 32

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom