Ttb yaratibu na kuongoza msafara kupanda mlima kilimanjaro kuadhimisha uhuru wa tanzania bara

Aug 15, 2011
30
11
Photo 2.JPG Photo3.JPG
Wafanyakazi wa TTB wakiongozwa na Mwenyekiti wa TTB Balzo Charles Sanga (wanne kushoto) katika picha ya pamoja na wapanda mlima wengine katika msafara huo akiwemo Meja Jenerali Gimongi (wa tano kushoto) wakiwa na bendera ya Taifa muda mfupi kabla ya kuanza kupanda Mlima. Katika picha ya pili msafara ukichanja mbuga kuelekea kituo cha Mandara.



Na: Geofrey Tengeneza
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania – TTB anaongoza timu ya watu saba miongoni mwao wakiwemo wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro ambao pia ni mrefu kuliko yote barani Afrika na ambao pia ni miongoni mwa maajabu saba ya asili barani Afrika.
Msafara huu ujulikanao kama Uhuru Expedition ambao ni mahsusi kwa ajili ya kuadhimisha miaka 52 ya uhuru umeratibiwa na kufadhiliwa na Bodi ya Utalii Tanzania na umeanza kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 6/12/2013 kupitia njia ya Marangu na unatarajia kumaliza zoezi hilo tarehe 10/12/2013.
Msafara huo wenye jumla ya wapandaji mlima saba (7) ambapo kutoka TTB ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Charles Sanga, Bw. Musa Kopwe na Bw. Hillary Mushi. Aidha katika msafara huo yumo pia Meja Jenerali mstaafu Gimonge, Bley Mayo, Bibi Lidya Kayuni na Bw. Joan Mwamlima wote kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Hii ni mara ya pili kwa Bodi ya Utalii Tanzania kuratibu msafara huu kwa lengo la kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania Bara. Mara ya kwanza kwa TTB kufadhili Uhuru Expedtion ilikuwa mwaka jana ambapo pamoja na TTB Kampuni nyingine mfano bia ya Serengeti ilijitoleza pia kudhamini Msafara huo wa Uhuru ulioongozwa na aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali mstaafu George Waitara.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom