TTB: Jinsi biashara ya ku burn CD ilivyowajaza pesa vijana hapo zamani

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Kuna biashara za misimu, na katika hizi biashara kuna biashara niliyoshuhudia kwa macho yangu iliyotajirisha mno vijana, biashara hii ilikuwa ni ku burn cd miaka ya 2000 hadi 2006

Mimi nitazungumzia scenario ya mkoa niliopo wa nyanda za juu kusini.

Enzi hizo miaka ya 2000s bongo flava ilikuwa imeanza kuchanua vlivyo na kulikuwa na deki zinazotumia cd na ningine zilionyesha video kwa vodeo cd.

Watu waliiona hii fursa, wakawa wanasafiri na hard disks zao kwenda Dar, wanajaza miziki na videos kibao, yani wakifika huku mikoani wanajaza mifuko acha kabisa.

Cd ya muziki wa kusikiliza ulikuwa unalipia elf 2 unawekewa nyimbo 18, ukitaka video kwa mfumo wa vcd hapo elf 5, ukitaka pilau andaa elf 10, pia kulikiwa na games zilizotamba enzi hizo kama mortal kombat, nedd for speed, vice city, game 1 elf 5 ,,,,,,,,,,,na enzi hizo miaka ya 2000 kiukweli hizo hela zilikuwa na thamani sana,

kuingiza hata laki kwa siku ilikuwa kawaida, Jamani tunazungumzia laki ya 2000s msifanye masihara aisee.

Changamoto ilikuwa kwamba vijana wengi waliofanya hii biashara walikuwa wanapenda sana starehe, fursa ilipoanza kuchuja walipata wakati mgumu sana
 
Back
Top Bottom