Tsvangirai Amburuza Mugabe Mahakamani


TUKUTUKU

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2010
Messages
11,841
Likes
49
Points
145
TUKUTUKU

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2010
11,841 49 145
Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai ameanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Rais Robert Mugabe kufuatia msimamo wake wa kuwateua magavana wa majimbo. Tsvangirai amelalamikaia msimamo wake wa huo akisema kuwa mugabe alipaswa kumshirikisha juu ya uteuzi huo kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano wa serikali ya mseto ambayo kimsingi ndiyo iliyomuweka madarakani Tsvangirai akiwa kama waziri mkuu.
Wakati Tsvangirai akichukua hatua hizo,Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini yuko nchini Zimbabwe katika ziara yenye shabaha ya kutatua mgogoro wa kisiasa unaoikabili serikali ya mseto nchini humo.
Rais Robert mugabe na waziri mkuu morgan Tsvangirai ambao ni mahasimu wakubwa wa kisiasa kwa miongo kadhaa walikubaliana kugawana madaraka kufuatia matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005.
Hata hivyo serikali yao hiyo ya mseto imekuwa ikikabiliwa na vikwazo kadhaa vikiwamo ugawanaji wa nafasi. Tsvangirai amekuwa akidai kuwa mugabe amekuwa akifanya maamuzi peke yake bila kumshilikisha na kumtuhumu kwa kutaka kumhujumu.Tokea aingie madarakani mawaka uliyopita rais Jacob Zuma amekuwa akijitahidi kuondoa tofauti za viongozi hao wawili lakini mafanikio yamekuwa kidogo.
Waziri Mkuu Tsvangirai pia anamtuhumu rais mugabe kwa kukiuka makubaliano kwa kukataa kumapisha Roy Bennett kuwa naibu waziri wa kilimo pamoja na maafisa wengine kadhaa kutoka chama chake cha MDA kushika nyadhifa muhimu serikalini.Rais mugabe kwa upande wake amesisititiza kuwa hatotekeleza matakwa ya Tsvangirai mpaka chama chake cha MDA kitakapowashawishi washirika wake wa nchi za magharibi kuiondolea vikwazo Zimbabwe.(Chanzo cha habari hii:Tanzania Daima 27/11/2010,pp.17.)

My take
Hivi viongozi wa afrika hawana uwezo wa kutatua matatizo ya nchi zao na kuzipa uwezo wa kuendelea kiuchumi kidemokrasia na ustawi wa jamii,badala ya kujikita zaidi kwenye migogoro isiyokuwa na tija kwa wananchi wa kawaida?
 
Kipala

Kipala

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Messages
3,562
Likes
98
Points
145
Kipala

Kipala

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2009
3,562 98 145
Unafanyeje ukiwa na mkorofi kama Mugabe? Asiyejali wananchi wake wanaokufa tu shauri la njaa au kukosa dawa? Maskini nchi iliyowahi kuwa mbele kiuchumi na kiutamaduni Afrika.
 

Forum statistics

Threads 1,235,534
Members 474,641
Posts 29,225,821