TSN yawasimamisha kazi waliofanya uzembe wa kuandika Rais Samia amefariki

Unatangaza Rais kafa kimakosa kwenye gazeti la serikali, adhabu kusimamishwa kazi? Na sio kufukuzwa kazi? Je lingekuwa ni gazeti la mwananchi au nipashe la kampuni binafsi?
 
Mmh huu ni uzembe wa hali ya juu kwa kiongozi mkuu kama huyu, sasa kwani huwa hawalikagui kabla halijatoka
 
  • Thanks
Reactions: cmp
Dr Abbas, msemaji mkuu wa serikali na Katibu mkuu wizara ya habari afukuzwe kazi na kushitakiwa
2. TISS wawajibike
3. Gazeti hii lifungiwe mwaka mmoja
Tangazo hili limeleta taharuki nchi nzima na ni uchochezi.
 
Huo uzembe wao hauvumiliki!

Yaani hata proof reading iliwashinda?
Mambo ya kuajiri wajomba serikalini ndo matokeo yake. Kuna watu wanafanya kazi serikalini ila uelewa wao unatia kinyaa utadhani waliishia la nne halafu unaambiwa Ana diploma.
 
Mambo ya kuajiri wajomba serikalini ndo matokeo yake. Kuna watu wanafanya kazi serikalini ila uelewa wao unatia kinyaa utadhani waliishia la nne halafu unaambiwa Ana diploma.
Usinikumbushe aliyekuwa kuwa Naibu Waziri wa madini akashindwa kuapa
 
Exq9pMCWQAUcR-Z.jpeg
ExqaiStXMAcAdjB.jpeg
Ndiyo zao hao, wasituzuge sisi.
 
Miaka ya nyuma ktk mji wa tarime trafik mmoja wa kike alielekeza vibaya msafara wa kikwete,alikamatwa kesho yake ikatangazwa amejuia kwa risasi akiwa mahabusu
 
Yaani, wameshindwa hata kuomba radhi; kuwasimamisha inawezekana ni makosa ya kibinadamu lakini uongozi wenyewe ulitakiwa kumuomba radhi Rais na wasomaji wao kwa usumbufu wowote unaoweza kuwa umejitokeza.
 
Waliwe vichwa tu hakuna namna, huu ni uzembe wa kiwango cha PHD.
 
Shida hapo ni Lugha tu. Tangazo lingekuwa la Kiswahili kusingetokea shida kubwa kama hiyo. Lkn kwakua tangazo lilikuwa kwa Lugha ya kimalkia, basi wasamehewe tu maisha yaendelee.
Uzuri mama mwenyewe ni muungwana sana.
 
Hapo hata mhariri mkuu anahusika.... Waache kuonea visamaki vidogo wakati mapapa yanapiga punyeto.
 
Back
Top Bottom