Tshs bilioni 2 kutumika kwa kesi 43 tu za uchaguzi

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,315
306
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jaji kiongozi Ndg. Fakhih Jundu jumla ya Tshs 2bn zitatumika kwa ajili ya kusikiliza kesi 43 za kupinga matokeo ya ubunge katika uchaguzi mkuu.

Hizi ni pesa nyingi sana kwa sasa na ukizingatia hali yetu ya umaskini tulio nao. Mie nadhani itafutwe njia mbadala ya kushughulikia kesi za namna hii kwani zitalifilisi Taifa. Madarasa mangapi yangejengwa kwa hela hii ? mahospitali mangapi mangapi? madawa kiasi gani yangenunuliwa ? nk
 
Naomba nielimishwe, wakati jaji anasikiliza hizo kesi za malalamiko ya uchaguzi si anakuwa anafanya kazi yake ya siku zote aliyo ajiriwa kufanya, sasa hizo gharama kubwa kiasi hicho zinatokana na nini?
 
Inafaa watupe mchanganuo, kwa sababu Lawyers wanalipwa na wahusika, wanasheria wa serikali wanapata mshahara, wanakadilia kuwa na Mashahidi 15 ambao mara nyingi hukaa nyumba za wageni kweli mimi nashindwa kuelewa hivi hawa majaji wanalipwa per diem kiasi gani. Watupe mchanganuo, wanahabari mupo hebu muulizeni huyu Jaji.
 
Hizi ni hela nyingi sana ndugu zanguni, kwa mtindo huu ina maana bila hela haki haitendeki. Ina maana kuwa wasipo pewa hizo hela hakuna kesi itakayo sikilizwa, sasa hapo haki ipo wapi ?
 
Naomba nielimishwe, wakati jaji anasikiliza hizo kesi za malalamiko ya uchaguzi si anakuwa anafanya kazi yake ya siku zote aliyo ajiriwa kufanya, sasa hizo gharama kubwa kiasi hicho zinatokana na nini?

Kila sehemu pamejaa ufisadi, kila mbuzi anakula usawa wa kamba yake aisee
 
Naomba nielimishwe, wakati jaji anasikiliza hizo kesi za malalamiko ya uchaguzi si anakuwa anafanya kazi yake ya siku zote aliyo ajiriwa kufanya, sasa hizo gharama kubwa kiasi hicho zinatokana na nini?

Lazima utambue kuwa kesi hizo zitasikilizwa Mikoani, kwa hiyo Majaji watatakiwa kulipwa Perdiem na Posho mbalimbali.
 
Pesa nyingi kwasababu mnafikiria in 'personal terms' ni nyingi kama tukikupa wewe ukamalizie nyumba yako boko huko..kesi zina gharama kubwa hizi. Mnataka haki mkipewa mnasema gharama kubwa...sasa kama sio nyege nini hizo tuite? Tulieni tuone kama kweli haki itatendeka. Too much criticism breads irrationality.
 
Lazima utambue kuwa kesi hizo zitasikilizwa Mikoani, kwa hiyo Majaji watatakiwa kulipwa Perdiem na Posho mbalimbali.

Actually kama kimbo liko wilayani basi kesi itakuwa huko, hii hurahishisha kuwasafirisha mashahidi gharama inakuwa ndogo
 
Lazima utambue kuwa kesi hizo zitasikilizwa Mikoani, kwa hiyo Majaji watatakiwa kulipwa Perdiem na Posho mbalimbali.

Lakini kila kanda ina majaji wake na bajeti yake ya mwaka, sioni sababu ya gharama hizi. Kama ni mashahidi hawa watakuwa wanatoka huko huko, na sidhani itahitajika fedha nyingi kiasi hiocho. Kwa mchanganuo wa magazeti ya leo, kila kesi itagharimu Tshs 52m! Kwa ajili gani? Kushuhudia uongo ni kazi kubwa, inahitaji gharama kubwa!
 
"Izingatiwe kuwa ili haki itendeke na ionekane kutendeka, Jaji hatasikiliza kesi katika kituo chake cha kawaida cha kazi. Tunalazimika kuwasafirisha majaji kutoka kituo kimoja kwenda kingine," alieleza Jundu.

Alisema kwa kuzingatia yote hayo, kila kesi itagharimu Sh 52,644,000, hivyo zinahitajika Sh 2,263,692,000 kuendesha mashauri hayo, ambayo kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi Namba 1 ya mwaka 1985, yanatakiwa kukamilika ndani ya miaka miwili tangu
yalipofunguliwa.

"Fedha hizo zinahitajika na ni lazima serikali ibebe mzigo huu, tumekwisha waandikia Hazina tukielezea mahitaji yetu ya fedha na kama zitapatikana, kuanzia Februari mosi mwakani kesi zianze kusikilizwa," alieleza Jaji Kiongozi na kufafanua kuwa kama ikitokea ndani ya miaka hiyo miwili kesi haijamalizika, Waziri wa Katiba na Sheria ana mamlaka ya kutoa nyongeza ya muda usiopungua miezi sita na ikionekana ucheleweshwaji wowote wa makusudi, basi kesi hiyo itafutwa.
 
Pesa nyingi kwasababu mnafikiria in 'personal terms' ni nyingi kama tukikupa wewe ukamalizie nyumba yako boko huko..kesi zina gharama kubwa hizi. Mnataka haki mkipewa mnasema gharama kubwa...sasa kama sio nyege nini hizo tuite? Tulieni tuone kama kweli haki itatendeka. Too much criticism breads irrationality.

None sense, nawe kweli ni great thinker ? Jiondoe tu humu jamvini
 
Hizi ni gharama za matokeo ya kuchakachua kura na ung'ang'anizi wa uongozi au kutokubali kushidwa.
Anayelipa ni mlipa kodi na kuzidi kuchunwa kwa mwananchi wa kawaida.
 
“Izingatiwe kuwa ili haki itendeke na ionekane kutendeka, Jaji hatasikiliza kesi katika kituo chake cha kawaida cha kazi. Tunalazimika kuwasafirisha majaji kutoka kituo kimoja kwenda kingine,” alieleza Jundu.

Alisema kwa kuzingatia yote hayo, kila kesi itagharimu Sh 52,644,000, hivyo zinahitajika Sh 2,263,692,000 kuendesha mashauri hayo, ambayo kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi Namba 1 ya mwaka 1985, yanatakiwa kukamilika ndani ya miaka miwili tangu
yalipofunguliwa.

“Fedha hizo zinahitajika na ni lazima serikali ibebe mzigo huu, tumekwisha waandikia Hazina tukielezea mahitaji yetu ya fedha na kama zitapatikana, kuanzia Februari mosi mwakani kesi zianze kusikilizwa,” alieleza Jaji Kiongozi na kufafanua kuwa kama ikitokea ndani ya miaka hiyo miwili kesi haijamalizika, Waziri wa Katiba na Sheria ana mamlaka ya kutoa nyongeza ya muda usiopungua miezi sita na ikionekana ucheleweshwaji wowote wa makusudi, basi kesi hiyo itafutwa.

KINACHO SIKITISHA NI GHARAMA KUBWA NA CHANZO NI DHANA NZIMA YA UCHAKACHUJI NAWAHUSIKA WAKUU NI TUME YA UCHAGUZI NEC KAMA HAWANA KINGA KISHERIA WAKIWEMO WAKURUGENZI WATENDAJI MBALIMBALI, KWA VILE WALIFANYA MAKUSUDI (KUKIBEBA CHAMA TAWALA KWA % KUBWA KWA MAELEKEZO YA kundi la mafisadi), NI BUSARA BASI WAKAWAJIBISHWA ILI WAJIFUNZE IWE MFANO KWA WENGINE ILI UZEMBE WA KUSABABISHA FEDHA ZA WALIPA KODI WA TZ KUTUMIKA KUTAFUTA HAKI YAO KINYUME NA MALENGO TARAJIWA YA KULETA MAENDELEO YA AFYA, ELIMU, MAJI, MIUNDOMBINU NK nawasilisha
 
Back
Top Bottom