Tshs 98,000/- Zilichakachuliwa

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 alikuwa anahitaji sana shilingi 100,000
(Lakimoja). Akamuuliza mama yake ni jinsi gani anaweza kupata pesa hizo. Mama yake
akamwambia "muombe Mungu atakupatia. Mtoto alianza kuomba kila siku na kila
mara lakini hakupata hiyo pesa toka kwa Mungu. Hatimaye akafikia uamuzi wa
kumuandikia barua Mungu ili asome maombi yake.

Kisha akai-post barua ile. Wakati wafanyakazi wa posta wakichambua barua
kwa ajili ya kuzipeleka sehemu husika, walishangazwa kuona bahasha iliyoandikwa
"Kwa Mwenyezi Mungu" na wakashindwa kuelewa mahali pa kuipeleka, Wakaamua
kuifungua.

Barua ilisomeka hivi:

"Mpendwa Mungu,

Jina langu ni JANET, nina umri wa miaka 9 na ninasoma darasa la tatu
katika jiji la Dar es salaam ambalo liko katika nchi ya Tanzania , bara la Africa .

Nimeamua kukuandikia barua hii kukuomba kiasi cha shilingi laki moja baada ya
kuomba bila kupata majibu toka kwako.

Naomba sana unisaidie kwani mimi ni mtoto mdogo na sina uwezo wa kufanya
kazi nakupata pesa. Pia wazazi wangu hawana uwezo kwani hata nchi yetu ni maskini
sana .

Natanguliza shukrani.

Wako mtiifu,


JANET."

Wafanyakazi wa posta walifurahishwa sana na barua hiyo na kisha wakaamua
waipeleke kwa Rais . Rais naye alipoipokea ilimfurahisha
sana na kisha akamwambia Secretary wake achukue sh. 2000 amtumie mtoto huyo akidhani kuwa pesa hizo ataziona kuwa nyingi sana .


Mtoto huyo alipopokea hizo shilingi 2000 alijibu hivi:

"Mpendwa Mungu wangu,
Nashukuru sana kwa kusikiliza maombi yangu na kunitumia pesa nilizokuomba.
Lakini nimebaini kuwa uliamua kuzituma kupitia serikali yetu ya Tanzania .
Kama ilivyo kawaida yao hao wezi, wamekata kiasi cha sh. 98,000 kwa ajili ya
kodi , kwa hiyo wameniletea Sh. 2000 tu.

Kazii Kwelikweli!!!!!!!!!!! Tshs 98,000 ZILICHAKACHULIWA?
 
Hii niliwahi kumsikia fisadi Mkapa akisema somewhere...teh! teh! teh!
 
That is what hapens to our lives. Those who are poor, will continue being more poor and those rich will continue being more and more richer.
 
Ni hatari kuwa na serikali isiyojali wananchi, tunachopata sisi ni kidogo sana, kikubwa chote kinachakachuliwa juu kwa juu. Mfano bajeti ya serikali 80% inaishia huko huko kwenye vikao vyao, posho na marupurupu, magari yao ya kifahari mwananchi wa hali ya nchi anabakia kuishi bila matumaini katika nchi yake yenye utajiri lukuki - Pole sana Janeth hizo 98,000 wamezichakachua.

Kidogo kilichopo tugawane wote, Rais angeamua kumpa ELIMU na AFYA bure mtoto Janeth basi angekuwa amemjengea maisha bora ya baadaye lakini badala yake anampa buku mbili - duh
 
Back
Top Bottom