Tshisekedi: DRC itanufaika na SGR, bandari Dar

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1128162



RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi (pichani) ameahidi kuimarisha ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania hususan katika matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam, barabara pamoja na reli ya kisasa mara itakapokamilika kwa ajili ya kusa rishia mizigo ya nchi yake.

Alisema hayo jana wakati alipotembelea ujenzi wa reli hiyo kwenye eneo la Vingunguti, pamoja na Bandari ya Dar es Salaam akiongozana na mawaziri kadhaa akiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe aliyekuwa akimwelezea namna ambavyo reli hiyo itainufaisha DRC.

Rais Tshisekedi alianza kwa kutembelea ujenzi wa reli hiyo na kusema kuwa itafungua milango zaidi ya biashara kwa wananchi wa DRC pamoja na kukuza uchumi wa nchi nne zitakazounganishwa na reli hiyo ikiwamo DRC yenyewe, Tanzania, Rwanda na Burundi.

Alisema reli hiyo ni ishara ya ushirikiano na uraki kati ya Tanzania na DRC uliodumu kwa miaka mingi zaidi na kuwa atahakikisha katika kipindi cha uongozi wake anaimarisha ushirikiano huo maradufu. “Tanzania na DRC ni ndugu wa muda mrefu na kwa sasa tumeamua kudumisha ushirikiano huu katika nyanja za uchumi zaidi, na nitahakikisha ninaunga mkono jitihada zote za kukuza uchumi kati ya nchi zetu hizi mbili na hata majirani pia,” alisema Baada ya kutembelea ujenzi huo, Rais Tshisekedi alitembelea Bandari ya Dar es Salaam alikotumia dakika kadhaa pia kutembelea sehemu ambapo mizigo ya DRC inahudumiwa na kuweka wazi kuwa bandari hiyo ni msaada wa kuimarisha uchumi wa DRC.

Alimshukuru Rais John Magufuli kwa kile alichosema kuwa amekuwa msaada kwa DRC hasa kwa kuiwezesha mizigo ya nchi yake kupitia bandari hiyo kwa wakati na usalama. “Kabla hata ya kuwa Rais niliona harakati za Tanzania katika kusaidia Congo na kwa sasa nimekuwa rais nitahakikisha kuwa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii unaimarika zaidi na ndio maana nimeamua kuja Tanzania kujionea namna miundombinu ya nchi hii inavyoweza kutusaidia,” alisema.

Waziri Kamwelwe alimueleza Rais huyo kuwa reli hiyo ya kisasa ikikamilika itarahisha uingizwaji wa mizigo nchini mwake kiurahisi na kwa haraka huku akimwelezea kuwa kwa sasa kuna bandari kavu mkoani Kigoma inayopokea mizigo ya DRC kabla ya kuisarisha kwa meli kwenda nchini humo kupitia Ziwa Tanganyika.

Alisema kupitia reli hiyo treni ya abiria itakuwa na uwezo wa kwenda kilometa 130 kwa saa na kisha kwenda kilometa 160 kwa saa kwa treni ya mizigo huku akimueleza kuwa kama nchi za DRC, Rwanda, Burundi zikiungana kufanikisha ujenzi huo kwenye nchi zao zitanufaika kiuchumi zaidi.

Akiwa bandarini hapo Waziri Kamwele alimueleza Rais huyo kuwa kwa sasa serikali imeanza kuchimba kina kirefu zaidi cha bahari kitakachowezesha meli kubwa za kubeba magari hadi 4,000 kutia nanga. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameahidi kushirikiana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi kuleta mabadiliko katika nchi ya DRC yenye utajiri mkubwa lakini uchumi wake unakua kwa kiwango kidogo. Alitoa ahadi hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na Rais huyo kabla ya kuelekea Dodoma kuendelea na ziara yake.

Rais Magufuli alimtaka Rais Tshisekedi akaikomboe nchi hiyo na kushughulikia kero za wananchi wake huku akimueleza kwamba Tanzania imeondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi hizo mbili pamoja na kuimarisha miundombinu ya kibiashara. “Nimemuhakikishia kwamba Tanzania na Congo ni ndugu kwa miaka mingi, nimemuomba akashughulikie shida za watu wake na kuikomboa nchi hiyo… nimemuhakikishia kwamba tutashirikiana naye kwa kila hali katika mabadiliko hayo,” alisema Rais Magufuli.

Alisema nchi hiyo pamoja na kwamba ni ya pili kwa ukubwa Afrika na ina rasilimali kama vile ardhi yenye rutuba na madini ya aina mbalimbali lakini ukuaji wake kiuchumi ni asilimia nne tu. “Kuna watu ambao wameikisha nchi ya Congo hapo, sasa wewe ukalete mabadiliko,” alisema. Rais Magufuli alisema kuwa amemuahidi Rais huyo kwamba Tanzania itaipigia debe nchi hiyo iingie katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili waweze kunufaika na umoja huo. Aidha, alisema ushirikiano kati ya Tanzania na DRC ni wa miaka mingi lakini kwa upande wa kibiashara haukua mkubwa na kuwa kwa mwaka jana miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa ilikua minane, ajira 418 na biashara za thamani ya Sh bilioni 305.

“Kiwango hicho ni kidogo ikilinganishwa na ukubwa wa nchi zetu, fursa zilizopo ardhi, madini, gesi na mafuta, tulitakiwa kufanya biashara kubwa zaidi na kwa manufaa ya nchi zetu,” alisema Rais Magufuli. Alisema ziara hiyo ya Rais Tshisekedi itafungua milango zaidi ya ushirikiano wa kibiashara na kwamba katika mazungumzo yao, msisitizo ulikua katika kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na imeondoa vikwazo vya kibiashara.

Rais pia alisema kuwa wamekubaliana kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiashara na amewakaribisha wafanyabiashara wa DRC kuja Tanzania kununua bidhaa mbalimbali na kuwekeza katika viwanda, uvuvi, kilimo, madini na amehamasisha benki za hapa nchini kufungua matawi katika nchi hiyo kurahisisha mazingira ya biashara.

“Wananchi wa DRC waione Tanzania ni nchi yao na watanzania waione DRC ni nchi yao,” alisema na kuongeza kuwa Tanzania imeanzisha soko la madini katika mikoa yote hivyo wanakaribishwa kuja kununua na kuuza. Mengine wamekubaliana kuimarisha ulinzi na usalama, sanaa, utamaduni na pia kuimarisha matumizi ya lugha ya kiswahili.

Aidha, Rais Magufuli alisema wamekubaliana kufufua tume ya pamoja ya ushirikiano katika masuala ya maendeleo ambayo iliundwa lakini haijakutana tangu mwaka 2002 na kuwa nchi ya DRC ni nchi ya kushirikiana nayo katika biashara kwa sababu wana fursa nyingi za kibiashara na pia kuna muingiliano mkubwa wa kijamii kati ya raia wake na kwamba wataendeleza ushirikiano huo kitaifa na kimataifa.

Rais Magufuli alimuekleza Rais huyo kuwa Tanzania imeboresha huduma za bandari kudhibiti vitendo vya rushwa, kuboresha mifumo ya bandari, kufuta tozo ya dola 600 ya kusindikiza mzigo kwenda DRC. Nyingine ni uboreshaji wa usari wa anga, barabara, reli, maji na ujenzi wa mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tanzania hadi Rwanda alisema kuwa lengo ni kuikisha reli hiyo DRC ili kukisha mizigo ya nchi hiyo.

Kwa upande wake, Rais Tshisekedi alimshukuru Rais Magufuli kukubali kuunga mkono nia yao ya kujiunga na EAC na kwamba wanaamini hivi karibuni watakua wanachama, pia alisema amekubali mualiko wa Rais Magufuli wa kushiriki mkutano Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwani utafungua fursa zaidi kwao.
 
Hahaha nyie jengeni tu, mkimaliza ndio mtapata akili, TAZARA inawafia sasa tafuteni sifa na SGR yenu kwa wakongo.
Kama inafaida kwao walete pesa za kujengea.
 
Back
Top Bottom