Tshabalala amemdhalilisha meneja wake, Henry Mzozo

AIsee andiko jepesi saana kaka umeandika...nikuulize maswali madogo tu umejuaje kama Kasaini bila kuwepo Manager wake leo?
Mohammed Husein Hana uwezo wa kusain karatasi lolote la mkataba bila ya uwepo wa meneja wake. Izo stori zako ni za vijiwe vya kahawa.

Mnaokataa kuwa Tshabalala amesaini bila ya kumshirikisha meneja wake, sikieni hii hapa halafu mrudi kufuta post zenu


 
Kitendo cha Tshabalala kuongeza mkataba wa kuitumikia Simba SC bila kumshirikisha meneja wake, Henry Mzozo, hakuna namna nyingine ya kukielezea zaidi ya kusema ni udhalilishaji wa hali ya juu wa mchezaji kwa meneja huyo.

Mzozo katika siku za hivi karibuni amekuwa akizungumza katika vyombo vya habari kwa ujasiri mkubwa kwamba safari hii hakuna chaguo la 'mchezaji wake' kusalia Simba, na kwamba uamuzi walioufikia ni kuondoka kabisa Simba hata kama ikibidi kwenda Gwambina, kwa kile alichoeleza kuwa ilikuwa mchezaji huyo asisaini Simba hata kipindi cha miaka miwili iliyopita ila waliivumilia tu, lakini safari hii hawatasaini kabisa.

Kabla hata masaa 24 hayajapita, taarifa ya maandishi, picha na video ikatolewa katika mitandao rasmi ya kijamii ya klabu ya Simba zikimuonyesha na kumnukuu Tshabalala akikiri kusaini mkataba mpya na klabu hiyo, tena bila ya uwepo wa 'meneja wake' ambaye amekuwa akimpamba mchezaji huyo katika vyombo vya habari

Jambo hilo mimi binafsi nimelitafsiri kama ni dharau na udhalilishaji wa mchezaji kwa meneja wake, na hivyo kuwafanya baadhi ya watu waliokuwa wakifuatilia sakata hili, kufanya dhihaka na kejeli kwa meneja huyo pamoja na waliokuwa wakimuunga mkono, hasa baadhi ya wachambuzi wa soka la Tanzania

Tshabalala asiishie hapo, amuombe radhi meneja wake, na pia asimsahau moja kwa moja hasa kwa mgao walau kidogo wa dau alilotengewa na Simba
Kwa taarifa yako meneja ni mwajiriwa wa mchezaji! Anaweza kufukuzwa na mchezaji wakati wowote! Mzozo has been fired!! Akale jeuri yake!!
 
Dauda ni simba,watu wa mikia awajajua tu km dauda alikua anawashtua na yeye hao wachezaji mwisho wa msimu wangekua wachezaji wa Yanga,mikia mumshukuru sana mkia mwenzenu sio wa kumlaumu kabisa
Dauda ni utopolo damu damu! Japo Jamaa anatanguliza maslahi binafsi kabla ya upenzi wa timu. Ni kanjanja huyo kazi yake ni mdomo umtengenezee pesa! Saa hii anatarajia Mohamed Hussein amkatie pande kwa kisingizio cha kusaidia dili la usajili wake! Asipomkatia pande tayari keshakuwa adui na ajiandae kuandamwa kwa maneno!
 
Mzozo hajielewi!! Hata kama ni kweli alimlea hicho si kigezo cha kumpangia!! Kumbe kwa maneno yake mwenyewe Mzozo anasema yeye si meneja wa Mohamed Hussein bali ni mlezi wake tu! Ukimlea mtu hutamlea milele. Akikua akawa mtu mzima ki-umri na ki-fani anajitegemea, anakuwa na maamuzi yake mwenyewe! Kwa hiyo Mohamed amekua!! Mtu akikua akaweza kufanya maamuzi binafsi anapongezwa si kulaumiwa! Kwa mtu mzima kuomba ushauri ni hiari wala si lazima! Na ushauri unaweza kukataliwa pia. Namshauri Mzozo ampongeze kijana wake na bila shaka mlezi ataendelea kumegewa pande kwa hiari wala si kwa kipangiwa. Hongera Mzozo kwa malezi!!
 
Dauda ni utopolo damu damu! Japo Jamaa anatanguliza maslahi binafsi kabla ya upenzi wa timu. Ni kanjanja huyo kazi yake ni mdomo umtengenezee pesa! Saa hii anatarajia Mohamed Hussein amkatie pande kwa kisingizio cha kusaidia dili la usajili wake! Asipomkatia pande tayari keshakuwa adui na ajiandae kuandamwa kwa maneno!
Dauda kishagombea hadi ujumbe huko mkiani akatoswa
 
Back
Top Bottom