Tsh Milioni 500 zinazotangazwa na Wabunge kwamba zimetolewa na Rais mnazielewa?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Hizi fedha zinajenga barababara ukubwa gani? Kwanini fedha hizi kwa idadi ya majimbo tuliyonayo zingekabidhiwa TARURA ZIKAJENGA barabara kwa kuzingatia kipaumbele Cha Tarura kuliko kutawanya fedha kwenye kukwangua barabara ambayo mvua ikinyesha mara moja zinarudia Hali ileile.

Hizi fedha naamini ni walipa kodi na zinapotumika bila kuangalia value for money na quality ya kile tunachokifanya tukaalia siasa tutajikuta tunatumia trillions ambazo hazitakuwa na impact. Bora kujenga barabara za majimbo mawili zakudumu kuliko kuchonga barabara ambazo zinaharibika kila mvua ikinyesha.
 
Milioni 500 zinatangazwa kwamba zimetolewa na Rais Samia, zimepokelewa Kwa hisia tofauti baada ya baadhi ya wabunge wa mkoa Fulani kuelekeza fedha hizo kujenga 1/2 kilometa za lami kwenye majimbo Yao maeneo yaliyopo mjini na ambako ndipo wanaoana walipo wapiga kura wengi na kuachana na wazo la rais la kutengeneza barabara za vijijini kusaidia wakulima na mazao Yao. Serikali ifuatilie fedha hizo Kwa umakini wake na zijengwe kweli barabara za vijijini na sio za mjini.
 
U27mq.jpg
 
Huu utaratibu wa kusema rais katoa hela ukoje? Rais anatumia kodi zetu, inatakiwa waseme Serikali imetoa hela. Ndio maana baadae hawa viongozi wanasifiwa mpaka wanakuja kujiona miungu watu.
 
Kumbe ulifanikiwa kuupigania uhai wako, Mungu ni mwema…. karibu tena mkuu.

Rambirambi tulizochanga sijui itakuwaje..!!
 
Huu utaratibu wa kusema rais katoa hela ukoje? Rais anatumia kodi zetu, inatakiwa waseme Serikali imetoa hela. Ndio maana baadae hawa viongozi wanasifiwa mpaka wanakuja kujiona miungu watu.

Utaratibu huo ulianzishwa na jiwe.
 
Back
Top Bottom