Tsh. Milioni 200 kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike wilayani Rungwe

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Halmashauri ya Rungwe mkoani Mbeya imetenga zaidi ya Sh 200 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Kisondelo, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu na kudhibiti utoro.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mpokigwa Mwankuga ameeleza kuwa mradi huo utakuwa mwarobaini na kichocheo cha matokeo mazuri ya elimu, kwa wanafunzi wa kike wilayani humo hasa kutokana na jiografia ya wilaya hiyo ambapo uwepo wa mabweni utasaidia kupunguza adha ya wanafunzi wa kike kutembea umbali mrefu kufuata elimu, jambo litakalokuwa chachu ya ufaulu.
 
Back
Top Bottom