Eng. Y. Bihagaze
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 1,488
- 908
- Thread starter
- #41
Hii hoja ya Eng Y. Bihagaze sidhani kama ina kosa lolote lile.
Ametoa hoja nzuri tu ya msingi kwamba serikali haijali raia wake ambao kwa bahati mbaya kwa miaka nenda rudi hawaoni kwamba kuna tofauti kubwa ya maisha kugawiwa kati ya walicho nacho na wasio nacho.
Serikali ya CCM ingejaribu kusema kwamba sasa (kwa mfano) kwamba kuna mpango wa miaka mitano ya kuboresha hali ya miji yetu na kwa kuanzia tunataka kuliimarisha jiji la Dar-es-Salaam kwa kila kitu- miundo mbinu kama barabara, huduma ya usafiri, na kusema kwamba wilaya zake zitakuwa zikifanya kazi kwa kujitegemea zaidi kwenye maeneo kama kwenye ukusanyaji kodi za maendeleo.
Kwa mfano barabara nyingi za jiji la Dar-es-Salaam kwa sasa zina foleni ndefu sana na huweza kuchukua masaa zaidi ya sita hii ni moja ya makosa kwani upangaji mzuri wa njia za usafiri haujafanywa na ni pesa ndio inahitajika.
Pili, pamoja na kuandaa usafiri wa mabasi ambayo inasemwa yatakuwa yakienda kwa kasi bado kuna maeneo mengi tu ambayo yanahitaji marekebisho na si kwa kuzibaziba tu bali hata kujenga upya. Barabara kama ya tabata relini haipaswi kufanywa ndo njia ya mkato kwenye mjini kutokana na foleni ndefu hapo katikati.
Mheshimiwa raisi kama mimi analifahamu vizuri jiji la Dar-es-Salaam kama alivyo mzee Balozi Skyes na viongozi wengine. Lakini hata siku moja sidhani kama mheshimiwa raisi katika miaka kumi ambayo amekaa madarakani amewaza kuboresha miundo mbinu ya jiji hili ambapo mvua ikinyesha tu jiji zima hufurika maji.
Sasa kwenye suala la wana taaluma wetu hasa madaktari, mheshimiwa raisi akaleta uamuzi wake kwamba kama hawataki hizo milioni 3.5 watafute mwajiri ambae ataweza kuwalipa pesa hizo. Halafu watu wengi nao wanaunga mkono wazo hili la raisi.
Hii ni kasoro kwenye jamii kwani jamii imekuwa imefungwa na haiwezi kufikiri.
Pale Muhimbili bado mpaka leo akina mama wajawazito wanalala chini, chumba cha maiti bado ni kidogo sana na hata kuna wakati niliwahi kushuhudia mama mmoja akiondoka kwa miguu huku akiwa ameshikilia mfuko wa Rambo ambao niligundua kuwa ni maiti ya kitoto kichanga ambacho kilipoteza maisha baada tu ya kuzaliwa kutokana na matatizo kadhaa.
Na kwakuwa nafasi zilijaa kwenye kachumba hako basi aliambaiwa maiti ya mtoto huyo isingeweza kukaa humo zaidi ya siku moja.
Jamii yetu ya Watanzania ambao wamebahatika kuwa kwenye nafasi mbalimbali imefungwa na hatuna nafasi ya kufikiri na kubuni mambo yetu wenyewe.
Hospitali ya Muhimbili ilitakiwa iwe ni mfano wa kuigwa wa hospitali nyingi nchini mwetu na hata nje ya mipaka yetu.
Hospitali hii ipo tokea tupate uhuru na ni miaka mingi imepita. Hopitali hii ingeendelezwa kwa kuwa na ukubwa unaostahili kutoa huduma zote muhimu zikiwemo hata za kuhudumia viongozi wetu na familia zao badala ya kwenda nje ya nchi.
Kwahio mheshimiwa raisi na serikali yake angeangalia upya sekta ya Afya na kutafuta mawazo labda kwamba aunde bodi au utawala au kwa kiingereza trust ambayo itakuwa na kazi ya kusimamia hospitali zote kubwa nchini. Bodi hii itajitegemea kwa kila kitu na itasimamia ajira za madaktari, manesi, idara ya huduma za dharura, na ajira za mpaka wapiga deki.
Bodi hii inakuwa inaundwa na watu ambao hawahusiani na serikali ingawa wanaweza kuulizwa maswali kuhusu bajeti zao na mambo mengine lakini kazi yao kuwa ni kuhakikisha inasimamia hospitali zote na kuhakikisha hospitali zinajiendesha katika viwango vinavyokubalika kimataifa.
Pamoja na mambo mengine bodi hii itasimamia pia malipo ya mishahara kwa wafanyakazi wa hospitali wakiwemo madaktari na pia itaangalia ubora wa huduma watoazo na pia kuwadaidia madaktari katika masuala mbalimbali kwa kushirikiana na chama chao na jumuiya zao.
Ndio tutaona hapo kwamba kila hospitali inakuwa na nafasi kwa kila mgonjwa ambae anahijtaji kulazwa, magari ya kutosha ya kubeba wagonjwa, huduma za hali ya juu kutoka kwa madaktari wenye uhakika wa kazi na maisha yao, na mambo mengine mengi tu ambayo yatakuwa yakiongezeka siku hadi siku hata kufikia kila hospitali siku moja kuwa na helikopta yake yenyewe na hata madaktari wa njiani au "paramedics"
Serikali kila mwaka katika bajeti yake isiyo na longolongo inakuwa inatenga fungu la kutosha kupitia wizara yake ya Afya ambayo inahakikisha fedha inakuwepo kwa hii bodi kwa ajili ya mishahara.
Kama kila mheshimiwa raisi aliepita na serikali yake na washauri wao mimi sijaona mambo haya isipokuwa kuwepo migomo au mawazo ya kutaka kugoma katika kila serikali hizi ambazo tokea uhuru hazijawa na ubunifu au hazijapanga vizuri mipango yenye kuleta maendeleo ambayo sisi wananchi tungeyaona.
Badala yake waheshimiwa maraisi wetu wote na viongozi wengine na washirika wao wamekuwa wakijisahau mara tu baada ya kutua Ikulu magogoni na wakipata tatizo la kiafya madaktari wao wanawashauri kuhusu hospitali za nje na wanakwenda kuangaliwa afya zao au kutibiwa huko.
Hizi hospitali za nje ya nchi haitoi huduma za bure, kuna pesa nyingi ya kutoka kwenye kodi za wananchi ndio zinalipwa kwa mfano katika hospitali za London Bridge na ile ya wanawake na watoto ya Portland zote za mjini London Uingereza, kuangaliwa tu afya, kufanyiwa uchunguzi, malazi, chakula na huduma nyingine tu za manesi kunaweza kugharimu si chini ya tshs 12,300,000 au £50,000 au zaidi kutegemea na urefu na namba ya siku kwa huduma hiyo.
Lakini mawazo yakitolewa kwamba nchi yetu ni tajiri wa kutupwa mpaka watu wanakufa njiani wakipita njia za mkato wakitafuta kuja kuishi na kujaribu kupora utajiri tulio nao lakini ambao hatuutumii, mawazo hayo yanaonekana ni ya kuleta vurugu na wanatafutwa watoaji wa mawazo hayo ili wang'olewe ukucha kavukavu.
Umefika wakati wa kukaa chini na kufikiri sana juu ya matatizo tuliyo nayo kwamba tumeyazoea au tumezoweshwa.
...
Kweli....
Ufikie muda sasa.. Tuitumikie nchi yetu.. Tusiidharau.. Lakini Richard, bodi zipo Na zinatoa mapendekezo mengi, Lakini kuna kiitikio toka serikalini..'SINA HELA'
Hii sina hela mpaka lini.. Serikali haikusanyi mapato Na inalalamika sina hela sasa nani akukusanyie mapato yako ee serikali..
Tukiachana na sekta ya madini, viwanda, mawasiliano, na nyinginezo
Tumulike kurunzi kwenye kijisekta kidogo cha usafiri
ukisoma jalada la Tanzania profile Dec 2005, nchi ilikadiriwa kuwa Na magari 382,000 Na Kwa kadirio la ongezeko la asilimia 17 hadi 18 Kwa mwaka..Na sasa inch inakadiriwa kuwa Na magari 1,204,000.
Tukiacha aina nyingine za kodi Na tuongelee road license tu ambayo ni lazima.. Magari madogo Hulipoa 130,000 Na penati ya 50,000 wakizidi grace time.. Mabasi Na magari mengine makubwa huenda zaidi ya milioni.. Na hapa hatujajumlisha magari ya serikali, jeshi au mashirika ya uma..
Tukichukulia wastani Wa 260,000 Tsh Kwa GARI tunapata zaidi ya billioni 313.. Hela hii inakusanywa?.. Au jibu ni mwekezaji?
Kila kitu siwezi, kila kitu sina pesa.. Halafu Mtu akisema hazina haina pesa, anapigiwa kelele za Kufa Mtu.. Kha sasa Kama hazina hela Ipo walipeni Basi waganga chao....'SINA PESA' .. Kujichanganya tu..
Serikali haikusanyi kodi , haiwazi njia za kutunisha kipato cha Taifa .. Inachojua ni kunyofoa kucha zetu Na meno yetu tisile nyama tena... AIBU
Last edited by a moderator: