Tsh 3,500,000 Kwa Daktari wa Watanzania ni aibu!

Basi na Polisi nae tumpe 3.5 , Afisa masijala aanze 3.5M , kwa ujumla TGS D wote waanze na 3.5 ikimaanisha huko juu iwe adjusted accordingly wengine walipwe 5M wengine 15 M based on experience . Halafu zile pesa tulizotumia kwenye vita ya Kagera ambazo madeni yake hadi kesho hayalipiki riba zinaongezeka utakuja kulipa wewe?

Tulieni Kikwete atengeneze nchi, Nyerere alikuwa busy na ukombozi wa Africa tukatumia pesa nyingi hata barabara hakutengeneza zilianza kutengenezwa awamu ya pili na mambo mengine ya maendeleo. Sasa angalia hao ambao tumewakomboa hata Mozambique na Namibia wanatushinda. Madaktari mwacheni rais aweke mambo sawa madeni aliyoacha baba wa Taifa ni mengi ndio tunalipa kidogo kidogo na itachukua muda sana hii mgomo ilitakiwa mlete kipindi kile cha kujifunga mikanda.
 
Tanzania ya sasa si yakupiga kelele hizi tena, cha msingi na maana ni kujadili NINI KIFANYIKE kwani kama ni madudu yapo mengi na wengi tunayajua......lets us come with a solution. JE NINI KIFANYIKE SASA???
 
Bihagaze, lake Tanganyika lina kina kuliko yote Afrika, Lake Baikal ndio namba moja Duniani. Lakini bado, hazina ya utajiri tulio nao ni kubwa mno! Hatupaswi kuishi maisha duni kiasi hichi. Tusiishie kuilaumu serikali pekee, bali tuwajibike kuiwajibisha! Sio kulia lia tu, inabidi tuwalize na wao washike adabu. Tugome woteeeee!

Nawashangaa wanaosema madktari wanaomba hela nyingi sana, milioni 3.5 ni nyingi?
'

Lake Tanganyika is an African Great Lake. It is estimated to be the second largest freshwater lake in the world by volume, and the second deepest, after Lake Baikal in Siberia. source: wikipedia
 
Craaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapo zaidi ya porojo tulizo kwisha zizoea. Mkuu wa nchi ameisha waambia kama wanaona mshahara wanao upata ni mdogo waache kazi, sasa shida iko wapi mpaka utokwe na povu lote hilo? mie nilitegemea uwahamasishe madaktari waache kazi na sio kuleta ***** humu ndani

Mbayuwayu utawajua tuu sasa hili kamasi umeweka hapa nani asome kinyaa hichi;;utakufa na ujinga wako mbweha wewe
 
Eng. Y. Bihagaze Umemaliza mkuu Heshima kwako,mwenye sikio la kusikia na asikie neno ambalo unawaambia WADANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Eng. Y. Bihagaze Umemaliza mkuu Heshima kwako,mwenye sikio la kusikia na asikie neno ambalo unawaambia WADANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Nchi hii inaweza kulipa mshahara kila mwezi kila mtanzania tena mishahara minono! msinione mwendawazimu! mnajua hata USA haipo level zetu kwa utajiri? tatizo WATAWALA TU!

Nimeipenda hii, ubarikiwe!
 
Kama ni mbu tumeshapiga kelele saaana lakin mlalaji kalewa pombe hata hasikii yuko ndani ya chandarua anakoroma tu.
Masikin mbu tunalialia tu ng'weee na njaa zetu.

Kilichobaki tutafute namna ya kuchana chandarua tuingie humo humo. Sitaki kusikia kelele tena mana hazitusaidii.
Tumekalia "anakula,anakula" so what? Acha ale nasi tuendelee kukodoa macho tu. Ikifika uchaguz anawalambisha wazee wetu wakamchague na si vijana;" Aah, sipigi kura mimi,inanisaidia nn..! WTF...!!!!???
Shame on us Tanzanians. Talkin too much matendo hakuna
Hapo kwenye red pananikera kiasi kwamba nitajatembea na bakora kwa wajingawajinga kama hawa....nyambaffu!!!
 
Watanzania Kwanini Tusiongee Ukweli wetu tuujuao..Nchi ni yetu tusipoongea sisi nani atatuongelea..

Daktari wetu wa Watanzania anaomba aongezewe mshahara lau ufike Tshs3,500,000(2,200USD) kwa Mwezi..anaambulia jibu l a "SINA PESA" Kwa Nchi hii yenye Neema kulikoni Zote Duniani, Hii si aibu kubwa kwetu sisi wenye nchi...
Uchambuzi mzuri sana ,nakupongeza tunatakiwa kuamka.Kuna watu wanauza nchi kwa fedha za kununilia karanga za kupima wakituacha tunataabika.Kiongozi yupo radhi amsaidie mgeni anayetuibia trilion 10 kwa mwaka kwa yy kupewa milioni 150 akajenge nyumba mbezi,kweli hii ni akili ama matope.!!!
 
Katika insha yako ndefu na isiyo na mantiki umetoa mfano wa Libya ambayo kwa vyovyote vile haina ufanano na Tanzania nami ningetarajia kwamba ungetueleza nchi za Afrika ukiondoa Libya, madkatari wao wanalipwa kiasi gani. Unazungumzia rasilimali zilizopo. Swali ni je, rasilimali hizo bila kuziwekea uwekezaji zikaleta tija zaweza kutuondoa hapa tulipo? Hivi wewe ukiwa na shamba la urithi ambalo ni pori na halijafanyiwa uwekezaji linaweza kutatua tatizo la njaa?

Unashuku uwezo wa wahandisi wetu hapa nchini. Wana tofauti gani na hawa wakamua majipu ambao wanachojua wao ni kutoa mimba, kufanya tohara na kupasua vichwa wagonjwa wa miguu. Mbona wameshindwa kumtibu Ulimboka mpaka wakalazimika ku-outsource huduma hizo kwa wenye weledi wao? Muache kutumiwa mkidhani watanzania ni wapuuzi? Umeona ambavyo watanzania wameghadhabishwa na ujinga huu wa hao wafunga vidonda wako wenye tamaa?

..
Mbopo, ukisikia watu wanatumia neno 'mawazo mgando Basi ndio Kama Haya yako , wawekezaji, who is wawekezaji, Wa ndani au nje, nadhani u meen Wa nje, Yaani wewe mbopo, Kichwa yako haiwezi kifanya chochote mpaka Mtu Wa nje aje kukufanyia? Ni mfano Wa Mtu aliyeoa Na kuita majirani waje kumsaudia kuweka ujauzito ..

Ni ujinga mbopo, huu usemi 'SIWEZI' ... 'SINA HELA' Unatoka wapi, wao waliweza, jiulize nani aliwasaidia waweze?, ni mashetani gani au malaika wapi walishuka kuwasaidia 'WAO?', walitumia vichwa kwani sisi vichwa hatuna, kwanini kujidhakilisha kila siku siwezi siwezi , umeshakua Mtu mzima sasa , miaka HAMSINI sio kinda ee TZ..
 
baada ya kusoma makara yako nimeshindwa kujizuia kwa machozi! juisho ya yote wengi ukweli wanauona achana na hao wengine wanaofikiri kwa kutumia makalio, nalipenda pendekezo la nn kifanyike? ukweli ni kwamba baada ya mateso kuzidi juu ya wana wa izrael huko utumwani misri mungu alikisikia kilio chao akashuka na kumtumia musa kiongozi shupavu kuwakomboa atu wake LEO tz madaktari wamejitoa muanga ktk ukombozi wa taifa hili jamani kada zingine muko wapi tuungane tuwakomboe watz? muko wapi wakulima , walimu, wachumi; wanasheria,wanazuoni n.k kwani tupinge/ tukubari woga wa wassomi wa nchii hii ndio sababu ya matatizo yote. mfumo hautujari wana taaruma ili tuendelee kuwanyenyekea. ama kweli NJAA KITU KIBAYA SANA. NATANGAZA MSIMAMO kuanzia kesho mm naanzisha harakati za mageuzi, how ? wasiliana nami kwenye ulimwengu wa roho. com (MAOMBI)
 
Basi na Polisi nae tumpe 3.5 , Afisa masijala aanze 3.5M , kwa ujumla TGS D wote waanze na 3.5 ikimaanisha huko juu iwe adjusted accordingly wengine walipwe 5M wengine 15 M based on experience . Halafu zile pesa tulizotumia kwenye vita ya Kagera ambazo madeni yake hadi kesho hayalipiki riba zinaongezeka utakuja kulipa wewe?

Tulieni Kikwete atengeneze nchi, Nyerere alikuwa busy na ukombozi wa Africa tukatumia pesa nyingi hata barabara hakutengeneza zilianza kutengenezwa awamu ya pili na mambo mengine ya maendeleo. Sasa angalia hao ambao tumewakomboa hata Mozambique na Namibia wanatushinda. Madaktari mwacheni rais aweke mambo sawa madeni aliyoacha baba wa Taifa ni mengi ndio tunalipa kidogo kidogo na itachukua muda sana hii mgomo ilitakiwa mlete kipindi kile cha kujifunga mikanda.

Unasemaaa! Hebu soma hii news hapa DailyNews Online Edition - Tanzania's external debt doubles

Afu uniambie hapa kama ni vita vya kagera au ni baba wa taifa kasababisha!

Nimeona niitoe kwenye gazeti lenu pendwa!
 
Mbopo

Tazama ramani ya AFRICA kuhusu migodi ya madini inayofanya kazi kwa mujibu wa ANGRO ASHANT, Tanzania ndio iko mingi inayofanya kazi ikifuatiwa na SA. Katika kile kinachopatikana Tanzania inapata mrahaba wa 3% na ni mikataba ya 100yrs jamani hapohapo wana Tax exemption (Capital allowance) ya miaka mitano. VENEZUELA mikataba yote kati ya serikali na wawekezaji kuna clauz ya kukatisha mkataba bila malipo ya fidia pindi utakapogundulika hauna maslahi ya chi yao. Tanzania waziri anasaini mkataba hotelini kashalala na malaya na pombe za kirusi usiku kucha kwa nini asisaini madudu??????????......

Toka kwenye box and think without bias, hii nchi yaweza kua katika level za nchi zinazochimba mafuta kama Libya. Uranium inakaribia kuanza kuchimbwa na Wamarekani sasa hebu katazame Mikataba ambayo CCM imeingia na wachimbaji (eti wawekezaji). Tuna gesi na makaa ya mawe hivi serikali inashindwa kuchukua msaada kwa minajiri ya kuwekeza katika sekta hizi (Government owned mines) na kufaidika kwa 100% ya rasilimali zetu?

TANZANIA IS A SLEEPING GIANT

Unazungumzia hazina bila kuzungumzia kilichopo. Unazungumzia potential wakati wenzie tunazungumzia hali ilivyo kwenye hazina yetu. Kama msingi wa mgomo wa watu hawa mnaowaita madktari ni wingi wa rasilimali bila extraction na bila kuangalia kinachoingia hazina then tunalo tatizo la kichwa hapa kwetu.

Kama ungekuwa unafuatilia mikataba ya sasa ungeelewa kwamba baada ya kugundulika tu, nchi iko entitled to 12.5% ya proceeds zote na hiyo ni kabla ya kuingiza USD 1.8 billion that would entitle us to 37% of the stakes. Kwa vile watu hapa ni activists ambao hawajali stats ndiyo maana wanapiga makelele. Hatujaambiwa kama madktari wa Venezuela au South Africa wanalipwa ngapi, na je ni sawa na aggregate ya TZS 7.5 million wanayodai hawa wauguzi (hawana sifa ya udaktari) wetu? Je adherence to professionl and ethical standards za doctors wa huko nje ni sawa na hawa wajawa tamaa wenu?

Maelezo uchwara ya wanaounga mkono vitendo vya wahuni hawa yanadhihirisha kwamba mgomomule haramu umechochewa na sababu nyingine ambazo si za kisheria wala za kimantiki. Hawa waganga wanajua kwamba serikali hulipa mishahara kutoka na vyanzo vyake ambavyo vinafahamika. Kama leo unazungumzia hazina ya samaki na dagaa wa ziwa tanganyika walioko mita elfu nne chini ya usawa wa bahari, au uranium ambayo haijaanza kuchimbwa na ile gesi iliyoko kilomita mbili chini ya sakafu ya bahari, kama ndiyo basis ya kuongezewa mishahara basi kumbe wao ni wagonjwa kuliko wale wnaowatibu kwenye ile wodi ya vichaa.

Muanzisha thread hii na wengine wote wanaotumia mgomo huu ku-settle political score hawazungumzii jinsi wahuni hawa walivyopuuza sheria na amti ya mahakama kuhusu uharamu wa mgomo huu. Lakini lords of impunity wanauchekea upuuzi huu. I say this is sheer non sense and tightly so!
 
Basi na Polisi nae tumpe 3.5 , Afisa masijala aanze 3.5M , kwa ujumla TGS D wote waanze na 3.5 ikimaanisha huko juu iwe adjusted accordingly wengine walipwe 5M wengine 15 M based on experience . Halafu zile pesa tulizotumia kwenye vita ya Kagera ambazo madeni yake hadi kesho hayalipiki riba zinaongezeka utakuja kulipa wewe?

Tulieni Kikwete atengeneze nchi, Nyerere alikuwa busy na ukombozi wa Africa tukatumia pesa nyingi hata barabara hakutengeneza zilianza kutengenezwa awamu ya pili na mambo mengine ya maendeleo. Sasa angalia hao ambao tumewakomboa hata Mozambique na Namibia wanatushinda. Madaktari mwacheni rais aweke mambo sawa madeni aliyoacha baba wa Taifa ni mengi ndio tunalipa kidogo kidogo na itachukua muda sana hii mgomo ilitakiwa mlete kipindi kile cha kujifunga mikanda.

..
Shemeji mishahara ni sumni sumni kila kona, Mtu anayelipwa kijimshahara hawezi kusimamia mradi endelevu.. Imagine Leo Barabara zinachongwa, baada ya mwaka mahandaki mengi, serikali inapoteza mabilioni tena kwenye ukatabati..

Mradi ukisimamiwa Na Mtu asiye Na dhiki sana kimaslahi lazima itakuwa mkataba.. Miaka kumi bila kuona shimo..

Nchi yetu Imejaa watu wenye Mawazo mzungu njoo, mzungu njoo uwekeze utume hela, mzungu mwenyewe akija anajilipa mshahara Wa package ya 32 mil, Na watu wenye rangi Kama yake anawaza 12 to 17 mil mshahara, ila wataalam Wa nchini anawalipa laki Tisa au Saba .. Na rasilimali zote ni zetu, halafu Mtu unakataa HUJALOGWA...!!!
 
Mbopo
kweli jambo usilolijua ni kama usiku wagiza inaonekana mkuu wewe ni mmoja wawale wanaoila nchi yetu mawazo yako ni mgando kiasi hauwezi fikiria au hata kushaurika na inaonekana wewe wewe ni mfu wa mawaz na kama mwili wako unafanyakazi baadhi ya viungo vyako vinamatatizo makubwa sana. Naomba fikiria mara kwa mara ndio uje uchangie hapa

Kama kukataa upuuzi ni kuwa na mawazo mgando then i happily accept that. Nchii hii haiwezi kuendeshwa kwa mob justice ya wahuni wanaotumiwa kupotosha ukweli. I will not badge on this and i will not be cowed!
 
Katika insha yako ndefu na isiyo na mantiki umetoa mfano wa Libya ambayo kwa vyovyote vile haina ufanano na Tanzania nami ningetarajia kwamba ungetueleza nchi za Afrika ukiondoa Libya, madkatari wao wanalipwa kiasi gani. Unazungumzia rasilimali zilizopo. Swali ni je, rasilimali hizo bila kuziwekea uwekezaji zikaleta tija zaweza kutuondoa hapa tulipo? Hivi wewe ukiwa na shamba la urithi ambalo ni pori na halijafanyiwa uwekezaji linaweza kutatua tatizo la njaa?

Unashuku uwezo wa wahandisi wetu hapa nchini. Wana tofauti gani na hawa wakamua majipu ambao wanachojua wao ni kutoa mimba, kufanya tohara na kupasua vichwa wagonjwa wa miguu. Mbona wameshindwa kumtibu Ulimboka mpaka wakalazimika ku-outsource huduma hizo kwa wenye weledi wao? Muache kutumiwa mkidhani watanzania ni wapuuzi? Umeona ambavyo watanzania wameghadhabishwa na ujinga huu wa hao wafunga vidonda wako wenye tamaa?
kama kuna watu wajinga(sio wapumbavu) humu JF we ndo wakwanza yaani mpaka leo unajua wakisema mtu anapelekwa nje inamaanisha madaktari wa bongo wameshindwa pole sana..mtu anapopelekwa nje ni kwamba madaktari wamegundua tatizo lakini tiba yake haipo Tanzania (kwa sababu sekta ya afya haina vitendea kazi muhimu) mfano kwa tatizo la ulimboka asingetibiwa hapa kwa sababu mashine ya kumsaidia figo zake haipo hapa nadhani umeelewa unapo post hapa km kitu hujui bora uulize kwanza usikurupuke
 
Hii hoja ya Eng Y. Bihagaze sidhani kama ina kosa lolote lile.

Ametoa hoja nzuri tu ya msingi kwamba serikali haijali raia wake ambao kwa bahati mbaya kwa miaka nenda rudi hawaoni kwamba kuna tofauti kubwa ya maisha kugawiwa kati ya walicho nacho na wasio nacho.

Serikali ya CCM ingejaribu kusema kwamba sasa (kwa mfano) kwamba kuna mpango wa miaka mitano ya kuboresha hali ya miji yetu na kwa kuanzia tunataka kuliimarisha jiji la Dar-es-Salaam kwa kila kitu- miundo mbinu kama barabara, huduma ya usafiri, na kusema kwamba wilaya zake zitakuwa zikifanya kazi kwa kujitegemea zaidi kwenye maeneo kama kwenye ukusanyaji kodi za maendeleo.

Kwa mfano barabara nyingi za jiji la Dar-es-Salaam kwa sasa zina foleni ndefu sana na huweza kuchukua masaa zaidi ya sita hii ni moja ya makosa kwani upangaji mzuri wa njia za usafiri haujafanywa na ni pesa ndio inahitajika.

Pili, pamoja na kuandaa usafiri wa mabasi ambayo inasemwa yatakuwa yakienda kwa kasi bado kuna maeneo mengi tu ambayo yanahitaji marekebisho na si kwa kuzibaziba tu bali hata kujenga upya. Barabara kama ya tabata relini haipaswi kufanywa ndo njia ya mkato kwenye mjini kutokana na foleni ndefu hapo katikati.

Mheshimiwa raisi kama mimi analifahamu vizuri jiji la Dar-es-Salaam kama alivyo mzee Balozi Skyes na viongozi wengine. Lakini hata siku moja sidhani kama mheshimiwa raisi katika miaka kumi ambayo amekaa madarakani amewaza kuboresha miundo mbinu ya jiji hili ambapo mvua ikinyesha tu jiji zima hufurika maji.

Sasa kwenye suala la wana taaluma wetu hasa madaktari, mheshimiwa raisi akaleta uamuzi wake kwamba kama hawataki hizo milioni 3.5 watafute mwajiri ambae ataweza kuwalipa pesa hizo. Halafu watu wengi nao wanaunga mkono wazo hili la raisi.

Hii ni kasoro kwenye jamii kwani jamii imekuwa imefungwa na haiwezi kufikiri.

Pale Muhimbili bado mpaka leo akina mama wajawazito wanalala chini, chumba cha maiti bado ni kidogo sana na hata kuna wakati niliwahi kushuhudia mama mmoja akiondoka kwa miguu huku akiwa ameshikilia mfuko wa Rambo ambao niligundua kuwa ni maiti ya kitoto kichanga ambacho kilipoteza maisha baada tu ya kuzaliwa kutokana na matatizo kadhaa.

Na kwakuwa nafasi zilijaa kwenye kachumba hako basi aliambaiwa maiti ya mtoto huyo isingeweza kukaa humo zaidi ya siku moja.

Jamii yetu ya Watanzania ambao wamebahatika kuwa kwenye nafasi mbalimbali imefungwa na hatuna nafasi ya kufikiri na kubuni mambo yetu wenyewe.

Hospitali ya Muhimbili ilitakiwa iwe ni mfano wa kuigwa wa hospitali nyingi nchini mwetu na hata nje ya mipaka yetu.

Hospitali hii ipo tokea tupate uhuru na ni miaka mingi imepita. Hopitali hii ingeendelezwa kwa kuwa na ukubwa unaostahili kutoa huduma zote muhimu zikiwemo hata za kuhudumia viongozi wetu na familia zao badala ya kwenda nje ya nchi.

Kwahio mheshimiwa raisi na serikali yake angeangalia upya sekta ya Afya na kutafuta mawazo labda kwamba aunde bodi au utawala au kwa kiingereza trust ambayo itakuwa na kazi ya kusimamia hospitali zote kubwa nchini. Bodi hii itajitegemea kwa kila kitu na itasimamia ajira za madaktari, manesi, idara ya huduma za dharura, na ajira za mpaka wapiga deki.

Bodi hii inakuwa inaundwa na watu ambao hawahusiani na serikali ingawa wanaweza kuulizwa maswali kuhusu bajeti zao na mambo mengine lakini kazi yao kuwa ni kuhakikisha inasimamia hospitali zote na kuhakikisha hospitali zinajiendesha katika viwango vinavyokubalika kimataifa.

Pamoja na mambo mengine bodi hii itasimamia pia malipo ya mishahara kwa wafanyakazi wa hospitali wakiwemo madaktari na pia itaangalia ubora wa huduma watoazo na pia kuwadaidia madaktari katika masuala mbalimbali kwa kushirikiana na chama chao na jumuiya zao.

Ndio tutaona hapo kwamba kila hospitali inakuwa na nafasi kwa kila mgonjwa ambae anahijtaji kulazwa, magari ya kutosha ya kubeba wagonjwa, huduma za hali ya juu kutoka kwa madaktari wenye uhakika wa kazi na maisha yao, na mambo mengine mengi tu ambayo yatakuwa yakiongezeka siku hadi siku hata kufikia kila hospitali siku moja kuwa na helikopta yake yenyewe na hata madaktari wa njiani au "paramedics"

Serikali kila mwaka katika bajeti yake isiyo na longolongo inakuwa inatenga fungu la kutosha kupitia wizara yake ya Afya ambayo inahakikisha fedha inakuwepo kwa hii bodi kwa ajili ya mishahara.

Kama kila mheshimiwa raisi aliepita na serikali yake na washauri wao mimi sijaona mambo haya isipokuwa kuwepo migomo au mawazo ya kutaka kugoma katika kila serikali hizi ambazo tokea uhuru hazijawa na ubunifu au hazijapanga vizuri mipango yenye kuleta maendeleo ambayo sisi wananchi tungeyaona.

Badala yake waheshimiwa maraisi wetu wote na viongozi wengine na washirika wao wamekuwa wakijisahau mara tu baada ya kutua Ikulu magogoni na wakipata tatizo la kiafya madaktari wao wanawashauri kuhusu hospitali za nje na wanakwenda kuangaliwa afya zao au kutibiwa huko.

Hizi hospitali za nje ya nchi haitoi huduma za bure, kuna pesa nyingi ya kutoka kwenye kodi za wananchi ndio zinalipwa kwa mfano katika hospitali za London Bridge na ile ya wanawake na watoto ya Portland zote za mjini London Uingereza, kuangaliwa tu afya, kufanyiwa uchunguzi, malazi, chakula na huduma nyingine tu za manesi kunaweza kugharimu si chini ya tshs 12,300,000 au £50,000 au zaidi kutegemea na urefu na namba ya siku kwa huduma hiyo.

Lakini mawazo yakitolewa kwamba nchi yetu ni tajiri wa kutupwa mpaka watu wanakufa njiani wakipita njia za mkato wakitafuta kuja kuishi na kujaribu kupora utajiri tulio nao lakini ambao hatuutumii, mawazo hayo yanaonekana ni ya kuleta vurugu na wanatafutwa watoaji wa mawazo hayo ili wang'olewe ukucha kavukavu.

Umefika wakati wa kukaa chini na kufikiri sana juu ya matatizo tuliyo nayo kwamba tumeyazoea au tumezoweshwa.
 
Unazungumzia hazina bila kuzungumzia kilichopo. Unazungumzia potential wakati wenzie tunazungumzia hali ilivyo kwenye hazina yetu. Kama msingi wa mgomo wa watu hawa mnaowaita madktari ni wingi wa rasilimali bila extraction na bila kuangalia kinachoingia hazina then tunalo tatizo la kichwa hapa kwetu.

Kama ungekuwa unafuatilia mikataba ya sasa ungeelewa kwamba baada ya kugundulika tu, nchi iko entitled to 12.5% ya proceeds zote na hiyo ni kabla ya kuingiza USD 1.8 billion that would entitle us to 37% of the stakes. Kwa vile watu hapa ni activists ambao hawajali stats ndiyo maana wanapiga makelele. Hatujaambiwa kama madktari wa Venezuela au South Africa wanalipwa ngapi, na je ni sawa na aggregate ya TZS 7.5 million wanayodai hawa wauguzi (hawana sifa ya udaktari) wetu? Je adherence to professionl and ethical standards za doctors wa huko nje ni sawa na hawa wajawa tamaa wenu?

Maelezo uchwara ya wanaounga mkono vitendo vya wahuni hawa yanadhihirisha kwamba mgomomule haramu umechochewa na sababu nyingine ambazo si za kisheria wala za kimantiki. Hawa waganga wanajua kwamba serikali hulipa mishahara kutoka na vyanzo vyake ambavyo vinafahamika. Kama leo unazungumzia hazina ya samaki na dagaa wa ziwa tanganyika walioko mita elfu nne chini ya usawa wa bahari, au uranium ambayo haijaanza kuchimbwa na ile gesi iliyoko kilomita mbili chini ya sakafu ya bahari, kama ndiyo basis ya kuongezewa mishahara basi kumbe wao ni wagonjwa kuliko wale wnaowatibu kwenye ile wodi ya vichaa.

Muanzisha thread hii na wengine wote wanaotumia mgomo huu ku-settle political score hawazungumzii jinsi wahuni hawa walivyopuuza sheria na amti ya mahakama kuhusu uharamu wa mgomo huu. Lakini lords of impunity wanauchekea upuuzi huu. I say this is sheer non sense and tightly so!

Hizo 200Bil zinazodaiwa kutengwa kwa ajiri ya madaktari wa nje unadhani haiwezi kuboresha huduma za Afya? Usikariri kama panya na njia yake kwa masihara ya JK eti wamegomea mshahara pekee. Kushusu AMRI ya mahakama tazama hapa coz inaelekea kusoma na kuelewa hutaki kama CCM basi TAZAMA PICHA hii.....
 
Attachments

  • 730606353.jpg
    730606353.jpg
    119.8 KB · Views: 49
viumbe dizaini ya mbopo ndo ilitakiwa mnyofolewe kucha bila ganzi pumbafu wewe
 
Similar Discussions

29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom