Tsh 3,500,000 Kwa Daktari wa Watanzania ni aibu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tsh 3,500,000 Kwa Daktari wa Watanzania ni aibu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eng. Y. Bihagaze, Jul 4, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Watanzania Kwanini Tusiongee Ukweli wetu tuujuao..Nchi ni yetu tusipoongea sisi nani atatuongelea..

  Daktari wetu wa Watanzania anaomba aongezewe mshahara lau ufike Tshs3,500,000(2,200USD) kwa Mwezi..anaambulia jibu l a "SINA PESA" Kwa Nchi hii yenye Neema kulikoni Zote Duniani, Hii si aibu kubwa kwetu sisi wenye nchi..

  Ukienda Mbele zaidi unaweza kuhoji kwani hapo awali viumbe hawa,walikuwa wanalipwa Kiasi gani , kuna mtu atakwambia ni kiasi Fulani Chini ya Milioni Moja, kama 860,000 na Take Home yake 720,000(461USD) haya Ni maafa kwa Daktari wa Binadamu mwenzie. Kuna Jambo Limetufanya wengine tugande siku mbili hizi pale tuliposikia kwamba mkuu wa Kaya Hili la Watanzania ametamka waziwazi kwamba kiasi hicho ni kikubwa na hakiwezi Kulipika.. Inatisha sana sentensi hii .."SINA HELA"

  Mbali na Hapo nikaona wenzetu wengi wameweka takwimu za mishahara ya madaktari kwenye kanda ya Nchi mbalimbali Afrika humu jamvini.. na kwamba TZ ikaonekana ndio inayowalipa watanzania wake hawa vijisent kiduuchu, mimi si mtaalam wa takwim hizi ila niliwapigia cm marafiki zetu wa Libya hata na wewe unaweza kuwapigia +353 85 134 3515 , Mshahara wa RMO umefikia zaidi ya 8million za kitanzania, mbali na Nyumba na Food allowances, matibabu na security na anafanya kazi wiki tatu za mwezi. T

  anzania si NCHI ya KUFANANISHAna nchi yoyote barani Afrika na Duniani kwa ujumla, ni nchi ya kipekee inayojibeba kwa kusheheni Utajiri uliopitiliza.

  Tanzania ina zaidi ya Mito 46, Mto Ambala , Bangala , Great Ruaha, Kafufu, Kagera, Kalambo, Kilasi, Kipoke, Kiwira , Luhumuka, Lukuledi, Lumi, Magamba , Malagarasi , Manonga , Mara, Marogala,Mbaka ,Mkulumuzi ,Mkuzu ,Mrambo,Msangazi,Mulagala,Mwatisi,Myakaliza ,Ngerengere ,Pangani ,Rufiji ,Rurubu , Ruvuma , Ruvyironza,Selian,Semu ,Sibiti ,Sinini,Suma ,Ulanga,Ulanga ,Umba River, Wami ,Wembere,Zigi Mito hii ina mamilioni ya samaki wanozaliana kila mchao, Ila wewe "SINA HELA" Tanzania yako bado wananchi wanakula takataka, wanavimbiana kiunoni hadi .., mito yenye maporomoko na uoto wa ajabu.

  Tanzania ina Maziwa Mengi Makubwa ya Kimataifa, Ziwa Ambussel, Babati, Burigi, Chala, Eyasi, Ikimba, Jipe, Kitangiri, Manyara, Mdutu, Natron, Nyumba ya Mungu Reservoir, Rukwa, Sagara, Tanganyika, Victoria .. Achilia Mbali Mbuga za Wanyama Kubwa sana lakini zimechukua asilimia 4.4 ya eneo la nchi yetu, Mbuga za Arusha, Gombe Stream, Jozani Chawaka, Katavi, Kilimanjaro, Kitulo, Lake manyara, Mahale,Mikumi, Maunt Meru, Ruaha, Rubondo, Saadani, Serengeti, Tarangire, Udzungwa

  Umewahi kusikia Hifadhi za Kisiwa Cha Mafia, chenye nchi chini ndani ya maji, bahari mavu, ukizama chini ya bahari yake unakuta majani mengi tu (sea grass) tena maji yake masafi utadhani ni mbuga za wanyama chini ya Bahari, Umewahi kusikia Mnazi Bay kijieneo kidogo ha bahari kama Kilometa za mraba 650, lakini kimesheheni samaki aina 440, nadhani mwenzangu umeshasikia juu ya Ngorongoro Kreta, sehemu ya mchoto mkubwa wa meguko la kivolkeno la mlima mkubwa ulioacha uwanda mkubwa usio na maji AMBAO hakuna kama hivi Duniani.. ni maajabu makubwa sana ndani ya Tz inayosema "SINA HELA", wanasema nyayo za mwanadamu wa kale ziligunduliwa hapo, mwanamke Daktari leakey akagundua Fuvu la mwanadamu wa kale zaidi. Mie najaribika kusema Edeni labda ilikuwa Tanzania.. Utajiri wote huu.. "SINA HELA".. mie sijui kama weye umeshasikia habari za Ndege wanaotengeneza michoro angani, ndege wanaoruka kama waoteao shambulizi hapo naongelea hifadhi ya Selous. Niseme nini "SINA HELA UNIELEWE??"

  Tanzania yenye madini ya kila aina, Nikuulize ‘SINA HELA" embu Tafuta ni madini gani hapa Duniani hayapo TANZANIA, Kila Madini kila kito TZ ni asili yake, Zaidi ya Yote Mwenyezi Mungu ameweka upendeleo maalum na kutulazia Madini ambayo ni yetu tu, hayapo pengine kwenye dunia Yote, TANZANITE, nani anabisha.. "SINA HELA".

  Mbali na Uranium, Leo hii Tuna Mafuta, Vitalu nane vyenye ratili za mafuta laini yenye thamani sana Duniani. Nikikupa ujazo wa gesi tuliyonayo Tanzania ikiuzwa kwa usahihi kwa soko la ndani linatosha kuibeba bajeti kwa asilimia 89. Tukisema hivi mtu atasema tunakuza jambo, lipi tumekuza mbumbumbu wa kufikiri wewe. Mvivu wa kutumia kichwa, unatia joto kiti cha ofisi kwa kutengeneza midokezo ya posho kila siku na kuvizia visafari vya kukabana, bingwa wa kukopi vibajeti mwaka hadi mwaka unazidisha kwa 5%icrement.. Mvivu hadi nywele zako zinakusuta.. fia mbali kulee..

  ‘SINA HELA" karne hii nchini kwako bado wananchi wako wanalima kwa jembe la mkono, miaka hamsini ya Uhuru, tukisema mawazo yamerogwa na yakarogeka ni uongo? Leo Daktari maskini ya Mungu anaomba kamshahara kiduchu unamaka "SINA HELA" kama unaona haitoshi "TIMUA" UNAFUNGA MJADALA, UNAONDOKA , full stop, aisee, aisee!! .. Uvivu wa viongozi wetu kufikiri ndio unaoburuza taifa..

  Taifa ni Letu kwanini TUSISEMEE.. tusiposema sisi machozi ya watoto wetu yatatusuta..kila mtu ni mzazi ana familia, kila mtu ana haki ya kusema, kama hutaki mtu aseme UA..

  Kiongozi bora hupima kila changamoto na kuijaribu lakini si kuikataa na kuipinga kwa kunyofoa watu wake kucha na meno bila ganzi.. aisee IMENIUMA SANA..

  Sijamaliza kuchimbua utajiri wa nchi hii isiyo na ukabila, isiyo na Udini, isiyo na Lugha changanyiko, kila mtu anajua Swahili, Nchi Tulivu.. , sijaenda kwenye mazao.. ‘SINA HELA" basi hiyo slogan "SINA HELA" ingekuwa na uwiano, Unaposema SINA hela basi hata nyumbani kwako uwe kweli huna hela watu watasema huyu bwana muungwana. Sasa unaposema sina hela huku watoto wako (mawaziri) wakijenga Dream Houses ufukweni, wanabadili magari ya kifahari kama mashati, wanatenda wanavyotaka halafu unasema"SINA HELA" Huu ni Ungwana?,

  Kuna Shule siku hizi zinaitwa English Medium, ada yake ni nene sana kiasi, kuna nyingine hadi milioni 14 kwa mwaka kama ada ya mototo. Na wanaosoma huko ni watanzania watoto wa watanzania.. sasa hii Fortune ndani ya nchi hii hawa wenzetu wameitoa wapi kama "SINA HELA" ina uwiano sawia? Huku mnatujengea shule sizizo na walimu na ambazo wanafunzi wanasogeza umri tu na kupotezea muda. Watoto wa "HAO" wala hawasomi shule za kata. Ni zetu mliotubagua..

  Tusiseme, tukisema mnaandaa operesheni ya kunyofoa Kucha na meno bila ganzi, na kuponda maeneo Mwenyezi Mungu aliyoamuru yalete Uzao? Tanzania yetu ni nchi ya Kipekee, hakuna nchi ya kuifananisha Duniani, Ina ziwa lenye kina Kirefu kuliko yote Duniani,-Tanganyika, Ina mlima wa Pili kuliko yote Duniani na wa kwanza mrefu Barani, wanasema Africa Watch. Huwezi kuifananisha Tanzania na japan au Korea ambapo hakuna Madini hata tone wala Mbuga za wanyama..

  Mimi nasema Madaktari wangedai Mshahara kuanzia Milioni 15 kwa mwezi kwa kuanzia, Nchi kama Japan ambayo haina Madini hata tone, Haina ardhi ya kutosha by then ardhi yenyewe miambamiamba tu, haina mbuga za wanyama.. daktari wake anaanza na Mshahara wa Japan Yen 1,000,000 sawa na Milioni 19.7za Kitanzania(1YEN = 19.7 Tshs), sasa Daktari wetu akisema anaanzia mil 15 kosa lake nini, kwenye nchi Tajiri kama hii.

  Fikirini Mtapata vipi fedha ndio maana ya Uongozi sio kunyofua Kucha watu. Shame!!. Utasema inshu za Uchumi, Utakuwa Mshamba wa karne weye, Japan wasiojua Lugha nyingine, japan inayozungukwa na maadui, japan nchi ya watu wanye aibu, WANACHOKIFANYA KIPI SISI HATUKIWEZI?.. kama ni Hummer Technolpgy sisi nani katuzuia.. Kulalama kulalama.. SIWEZI.. SIWEZI.. MI SIWEZI.. Mbona bingwa wa kuzaa na kuzalisha.. shit…

  Mimi siwezi wala sithubutu kuongelea mishahara wa kada Nyingine, Eti wahandisi, Kwani Tanzania Kuna wahandisi, au ni Ubatizo waliotupa ERB na sisi tunajiita Eng, Kufukuzia vitenda vya kuziba barabara viraka ambavyo unahonga mpaka unachakaa kabla ya kukipata, utamwita mhandisi huyo, barabara ya mbagala juzi tu imetengenezwa lakini wahandisi tumeshindwa kusimamia ijengwe kwa viwango leo imekuwa kama chapati.. Rushwa na Ujinga, FTC anaitwa Mhandisi wa Wilaya, huyo huyo anaingia kwenye vikao vinavojadili barabara, maji, umeme, ukichunguza cheti ana FTC ya welding.. Fani ya Uhandisi Tanzania Tumejidhalilisha, Tumedhalilishwa, na nadhani Tumeridhika Kudhalilishwa.. INATOSHA!! Unamlipa Mhandisi Tsh420,000 Gross na Net 360,000, kwa mwezi, Kisha mhandisi huyo utamkuta ana gari, kila siku mafuta ya 20,000 (sawa na 600,000) kwa mwezi kwenda kazini na kurudi, anapata wapi hela hizi na yeye mshahara wake ni nusu ya gharama za mafuta.. Mwizi HUYU.. MWIZIII!! Hata kama Ukichuki Mwizi tu.. System Imekulazimisha uwe Mwizi.. na wewe umeikubali.. Mdhambi tu..

  Wabunge wetu ndio Usiseme, Kijiposho tunachowapigia kelele chenyewe kiduuchu, sasa Wako Hoi bin dhoofu, Walipoona mshahara wakakurupukia mikopo, sasa inawatafuna, wengine sasa hata pa kukaa gharama kubwa Dodoma, wanalala kwenye nyumba za Ibaada na kwenye vihoteli vya uchochoroni Hali ni mbaya kila mtu isipokuwa wajanja wachache ambao ukiwazungumzia wanakungoa meno na kucha bila ganzi.. Mbona mtatung'oa wengi .. kwa maisha mliyotupa bora mtusaidie tu kutuwahisha kwa muumba tuwaachie Dunia yenu wajinga wakubwa..

  Mimi Bihagaze nadhani kuna haja ya fani zote za ualimu, uhandisi, uchumi, kuamka kama wanavyoamka madaktari, kuiwajibisha serikali ifikiri na kufanya kazi ya kutumia rasilimali za nchi hii kwa ajili ya wananchi wenyewe, Huo ndio Uongozi sio kutia Joto Viti vya wachina na "Eliza", Kama Huwezi HUJALAZIMISHWA.. Ulizia Migodi, ulizia viwanda, ulizia hata baaadhi ya Mbuga za wanyama 100% zinamilikiwa na wageni, wewe Tanzania unaaambulia nini? "SINA HELA" Kama mliokasmiwa madaraka hamuwezi muondoke na safu nyingine iingie kufanya kile wanachodhani wanataka kufanya kwa maslahi ya Nchi yao.

  HII NI NCHI YETU SOTE SIO YA KIKUNDI FuLANi PEKEE.. TUSITISHANE..
   
 2. mzalendokweli

  mzalendokweli JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama ni mbu tumeshapiga kelele saaana lakin mlalaji kalewa pombe hata hasikii yuko ndani ya chandarua anakoroma tu.
  Masikin mbu tunalialia tu ng'weee na njaa zetu.

  Kilichobaki tutafute namna ya kuchana chandarua tuingie humo humo. Sitaki kusikia kelele tena mana hazitusaidii.
  Tumekalia "anakula,anakula" so what? Acha ale nasi tuendelee kukodoa macho tu. Ikifika uchaguz anawalambisha wazee wetu wakamchague na si vijana;" Aah, sipigi kura mimi,inanisaidia nn..! WTF...!!!!???
  Shame on us Tanzanians. Talkin too much matendo hakuna
   
 3. k

  kindafu JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona umeamua kuwa "liwalo na liwe"!! Ila hakika bila ya sie wananchi kuamua kuwa sasa basi - "enough is enough", wataendelea kutufanyia usanii mpaka tukome! Tusitarajie waachie ngazi hivi hivi - ni sisi kuwaambia "pisha njia"!!!
   
 4. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  wavivu wa kusoma wamekosa jambo la maana sana hongera sana Comrade hakika wewe ni MZALENDO
   
 5. whizkid

  whizkid JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 301
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Bihagaze, lake Tanganyika lina kina kuliko yote Afrika, Lake Baikal ndio namba moja Duniani. Lakini bado, hazina ya utajiri tulio nao ni kubwa mno! Hatupaswi kuishi maisha duni kiasi hichi. Tusiishie kuilaumu serikali pekee, bali tuwajibike kuiwajibisha! Sio kulia lia tu, inabidi tuwalize na wao washike adabu. Tugome woteeeee!

  Nawashangaa wanaosema madktari wanaomba hela nyingi sana, milioni 3.5 ni nyingi?
   
 6. M

  Makupa JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  maji marefu nalipwa mshahara mzito kuliko Profesa.wa chuo kikuu
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,492
  Likes Received: 5,593
  Trophy Points: 280
  Umenena Eng.Bihagaze.We have to do something NOW!
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,079
  Likes Received: 6,540
  Trophy Points: 280
  Ni hela ya kawaida sana tena siyo mshahara mkubwa kwa mtu aliyesoma vizuri,
  sijui watu wanachosema ni hela nyingi kipo wapi.
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,492
  Likes Received: 5,593
  Trophy Points: 280
  Nchi hii inaweza kulipa mshahara kila mwezi kila mtanzania tena mishahara minono! msinione mwendawazimu! mnajua hata USA haipo level zetu kwa utajiri? tatizo WATAWALA TU!
   
 10. paty

  paty JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,256
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Watanzania tumelala usingizi wa pono, tunawaangalia tu hawa jamaa wanvyogawana kwa pupa mali zetu, wakula mishahara mizito na ponsho zilizo nono, kazi yao kupiga porojo, kutuambia mambo tunayojua, wana tupa maslai madogo ili tuendelee kuwanyenyekea, KWA UMASKINI WETU WA KIPATO,KAKA ZETU WANAKUWA ADUI KWA KUDAI MASLAI, ambayo ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na maslai ambayo MMAFISADI wanajipatia,

  TUAMKE, TUAMKE NDUGU ZETU, madaktari wameonesha nia, hatukuwa wapa support, tuamke, tuamke tugawane utajairi wa nchi yetu, tuamke tudai maslai mazuri , mazuri sawa sawa ya wanayopata wao A LUTAAA CONITUA................ALUTA.... http://www.youtube.com/watch?v=uAlC_VYzHzU..A luta continua....A luta continua
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ninachokiomba kwa madaktari waendeleze ushirikiano wao siku sinyingi wataona nne na pengine wao watawazindua watanzania...
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Katika insha yako ndefu na isiyo na mantiki umetoa mfano wa Libya ambayo kwa vyovyote vile haina ufanano na Tanzania nami ningetarajia kwamba ungetueleza nchi za Afrika ukiondoa Libya, madkatari wao wanalipwa kiasi gani. Unazungumzia rasilimali zilizopo. Swali ni je, rasilimali hizo bila kuziwekea uwekezaji zikaleta tija zaweza kutuondoa hapa tulipo? Hivi wewe ukiwa na shamba la urithi ambalo ni pori na halijafanyiwa uwekezaji linaweza kutatua tatizo la njaa?

  Unashuku uwezo wa wahandisi wetu hapa nchini. Wana tofauti gani na hawa wakamua majipu ambao wanachojua wao ni kutoa mimba, kufanya tohara na kupasua vichwa wagonjwa wa miguu. Mbona wameshindwa kumtibu Ulimboka mpaka wakalazimika ku-outsource huduma hizo kwa wenye weledi wao? Muache kutumiwa mkidhani watanzania ni wapuuzi? Umeona ambavyo watanzania wameghadhabishwa na ujinga huu wa hao wafunga vidonda wako wenye tamaa?
   
 13. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Hizi ni hisia za Mzalendo wa kweli kuhusu Tanzania, we will never fail to deliver the truth top keep us free.......
   
 14. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Mbopo

  Tazama ramani ya AFRICA kuhusu migodi ya madini inayofanya kazi kwa mujibu wa ANGRO ASHANT, Tanzania ndio iko mingi inayofanya kazi ikifuatiwa na SA. Katika kile kinachopatikana Tanzania inapata mrahaba wa 3% na ni mikataba ya 100yrs jamani hapohapo wana Tax exemption (Capital allowance) ya miaka mitano. VENEZUELA mikataba yote kati ya serikali na wawekezaji kuna clauz ya kukatisha mkataba bila malipo ya fidia pindi utakapogundulika hauna maslahi ya chi yao. Tanzania waziri anasaini mkataba hotelini kashalala na malaya na pombe za kirusi usiku kucha kwa nini asisaini madudu??????????......

  Toka kwenye box and think without bias, hii nchi yaweza kua katika level za nchi zinazochimba mafuta kama Libya. Uranium inakaribia kuanza kuchimbwa na Wamarekani sasa hebu katazame Mikataba ambayo CCM imeingia na wachimbaji (eti wawekezaji). Tuna gesi na makaa ya mawe hivi serikali inashindwa kuchukua msaada kwa minajiri ya kuwekeza katika sekta hizi (Government owned mines) na kufaidika kwa 100% ya rasilimali zetu?

  TANZANIA IS A SLEEPING GIANT
   
 15. controler

  controler JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 1,537
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbopo Kwa sasa sisi unaotuita wakamua majipu tupo Huku Private hospitals tunalipwa per person! Ofcoz mimba tunatoa as per request kama ya yule mwanao wa form two nimeinyofoa mm! mchunge vizuri mwanao sawae?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. S

  Shembago JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  3,500,000Tsh Ki ukweli ni Hela ndogo sana ukizingatia rasilimali tulizonazo,shida ni hawa magamba yanayosema yanatutawala! jamani hivi kuna haja ya kuvumilia mpaka 2015? Can we do something now to save our own country? Kuna mkataba wowote tuliofunga nao mpaka 2015?
   
 17. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mbopo Unajiongelea mwenyewe Mtanzania mjinga..........ndio wana tamaa kwasababu wamezungukwa na utajiri wasioweza kuutumia, hata mimi na tamaa....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Craaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapo zaidi ya porojo tulizo kwisha zizoea. Mkuu wa nchi ameisha waambia kama wanaona mshahara wanao upata ni mdogo waache kazi, sasa shida iko wapi mpaka utokwe na povu lote hilo? mie nilitegemea uwahamasishe madaktari waache kazi na sio kuleta ***** humu ndani
   
 19. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mbopo
  kweli jambo usilolijua ni kama usiku wagiza inaonekana mkuu wewe ni mmoja wawale wanaoila nchi yetu mawazo yako ni mgando kiasi hauwezi fikiria au hata kushaurika na inaonekana wewe wewe ni mfu wa mawaz na kama mwili wako unafanyakazi baadhi ya viungo vyako vinamatatizo makubwa sana. Naomba fikiria mara kwa mara ndio uje uchangie hapa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hahaha kwa utajiri ulioutaja hapo juu viongozi kama hayati gadafi basi kila mtanzania angekuwa anakula mshahara, kamishen ya utajiri wa nchi kila mwezi.......lol!!!!!!
   
Loading...