Tsh 20,000,000! kuzawadiwa kukomesha mauaji ya Albino!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Polisi kutumia mamilioni ya fedha kukabili mauaji ya albino
Na Paulina David, Mwanza

JESHI la Polisi nchini, limetenga Sh20milioni kwa ajili ya kuwazawadia watu watakaotoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa wauaji wa vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

Mkuu wa jeshi la Polisi nchini,, Said Mwema aliyasema hayo jana wakati akizungumza na askari polisi wa jeshi hilo, maafisa wa polisi na waandishi wa habari jijini hapa.

Alisema fedha hizo, zimetengwa kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watu watakaotoa taarifa za uhalifu hususan za mauaji ya albino na vikongwe yanayoendelea kutokea nchini.

Alisema lengo la kutoa fedha hizo, ni kuhakikisha vitendo vya mauaji ya vikongwe na albino, vinatokomezwa nchini.

Alisema mpango huo, utafanikiwa endapo polisi watapata taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa watu wanaopewa kazi ya kuwakata mapanga albino, ili kuchukua viungo vyao kutokana na imani za kishirikina.

Alisema endapo watuhumiwa watakamatwa, ni wazi kuwa watawataja watu ambao wamewakodisha kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

“Tunatambua kuwa wahalifu wana mbinu nyingi na siye tunapopanga mikakati ya kukabiliana nao, wao pia wanabuni mbinu nyingine, ili wananchi watusaidie kuwadhibiti wauaji hao,” alisema Mwema.

Alisema katika Mkoa wa Mwanza vitendo vya kuwakata mapanga vikongwe, albino na ajali za barabarani zimekuwa tishio, hivyo jeshi hilo, linafanya kila jitihada za kuhakikisha vitendo hivyo vinadhibitiwa.

“Timu ya watu kutoka makao makuu wakiwemo ofisi ya mkemia, usalama wa taifa, polisi waliobobea kwenye upelelezi, wanasheria wanatarajia kufika jijini hapa kwa ajili ya kuona jinsi ya kukabiliana na vitendo hivi,” alisema.

Akizungumzia suala la askari polisi kujihusisha na vitendo vya rushwa kutokana na kutoboreshewa mazingira ya kazi, alisema kosa moja haliwezi kuhalalisha kosa jingine, hivyo askari anayetaka kula rushwa kwa kisingizio cha maslahi kidogo, anapaswa kuondoka kwenye jeshi hilo kwa kuwa hastahili.

Alifafanua kama askari mla rushwa atabainika, atafukuzwa kazi na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria, hivyo asisubiri hadi afukuzwe kazi na badala yake ajiondoe mwenyewe.

My Take:

Hatua hii japo ni ya kupongezwa na iliyopaswa kutekelezwa muda uliopiga bado naamini haijaweza kubadilisha odds za usaliti. Kiasi kilichotengwa bado ni kidogo kuvutia tamaa ya watu. Lakini zaidi mgawanyo wa zawazi ni vizuri uwekwe hadharani.

Kwa mfano:

a. Ataketoa taarifa ya mfanyabiashara anayetumia viungo vya Albino na Mfanyabiashara huyo akatiwa mbaroni na hatimaye kukutwa na hatia basi mtoa taarifa atapata Tsh. milioni tano no questions asked

b. Atakayetoa taarifa ya mganga mwenye kuagiza matumizi ya viungo vya albino au kutangaza fulani ni mchawi au mwenye kushirikiana na wafanyabiashara wa aina hiyo na mganga huyo akanyakwa, naye anapata milioni 4

c. Mwenye kutoa taarifa itakayozuia jaribio la kudhuru, kushambulia au kumuua Albino au kikongwe yeyote huyo anazawadiwa milioni mbili!

n.k

Kwa kufanya hivyo tunabadilisha odds za maisha kwa ndugu zetu Albino. Nashukuru kwamba pendekezo hili ambalo lilitolewa na wenu mtiifu karibu mwaka mmoja baadaye limeanza kufanyiwa kazi. Hata hivyo zaidi inahitajika.

Mtu atajiuliza kati ya kutoa taarifa ya kuzuia mauaji ya albino na kucheza bahati nasibu ya simu n.k ni kipi kinalipa. Kama mshindi wa kupiga simu analipwa milioni 50 au kama huyo mwingine aliyepewa gari ya mamilioni hivi majuzi. Pamoja na zawadi hizo kubwa, ni vizuri pia kutoa zawadi nyingine ndogondogo kama motisha.

Vinginevyo, nawaunga mkono kwa hatua hii na ninapendekeza dau liongezwe hadi kufikia kama milioni 200 hivi.

Na zaidi nawasihi wabunge ambao walichangia karibu milioni 400 kuchangia tibu ya Taifa baada ya kuifunga Togo, wawe wa kwanza kuchangia mfuko huu wa Polisi na iundwe timu maalum (inayowakilisha maalbino, wanasheria na asasi za kidini) ambayo itasimamia utoaji wa zawadi hizi ili watu wengine wasije kuwa mafisadi wengine!
 
Last edited by a moderator:
Ni hapo....

Ikitokea kwamba viungo vya albino ni moja kati ya mahitaji ili mbunge awe na mvuto jimboni kwake, serikali iko tayari kula sahani moja na wahusika?
(si lazima uwe ubunge tu, ni pamoja na mvuto wa kupata vyeo vya kiserikali, hasa vya kuteuliwa na Rais, kila kona ikiwa ni pamoja na ukuu wa polisi)

Ushirikina kwa nje unaonekana ni shughuli ya watu mbumbumbu, lakini uzoefu unaonyesha wasomi na watu wenye heshima kubwa serikalini na taifa kwa ujumla ni washirikina wakubwa ambao wako tayari kufanya lolote, ikiwa ni pamoja na kuua, ili kufanikisha malengo yao.

Mchungaji akiambiwa kiungo cha albino kitamsaidia kuukwa Ubaba Askofu, anaweka uchungaji,amri kumi za Mungu na ile amri kuu kutoka kwa Yesu Mesia ya Pendaneni pembeni na kukisaka kiungo hicho kwa udi na uvumba ili aukwae mkwaju,ile kofia kaa fukizio la muhunzi achilia mbali gauni la kichungaji na pete.

Ipo kazi, tutasikia mengi.
 
You said it all men!

Mimi nashangaa sana lack of seriousness kwa upande wa serikali kwenye kutatua au kulipatia ufumbuzi suala hili. Nina kila sababu ya kuamini kwamba watendaji wengi wa serikali na baadhi ya wabunge wanahusika moja kwa moja na biashara hii chafu ya mauaji ya albino. Inashangaza kuona viongozi wanakemea tu bila kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hii. Kuandaa maandamano, au waziri mkuu kwenda kutembelea kanda ya ziwa haitoshi. Tunataka hatua madhubuti. Tunaamini serikali ina intelligence ya kutosha kulikabili hili.

Iweje kwenye uchaguzi mdogo kama Tarime, Mbeya etc wanamwagwa polisi wengi tena tunaambiwa ni kikosi maalumu, lakini huko kanda za ziwa hatusikii lolote? Kamanda Tossi yuko wapi? Vikosi maalamu ni kupambana na wezi wa mifugo tu? (walitudanganya kwamba Tarime walikwenda kupambana na wezi wa mifugo na sio kuwatisha wafuasi wa CHADEMA). Mbona vikosi havikabiliani na wauaji wa albino? Kipi muhimu kati ya albino na mifugo?

Hali hii ndio inasababisha tuone serikali inahusika moja kwa moja na haya mauaji. Chukueni hatua!
 
Na wale watakaofichua ufisadi ndani ya chama, serikali na mashirika yetu ambao unasababisha nchi yetu kutoendelea watazawadiwa nini!?
 
Ila milioni 20 kwa vijijini watauzana kama wapakistani ,Maana pakistani ukimchomea jamaa tu anahusika na BinLadin basi kitita cha dola,unapewa ,na jamaa haulizwi ila ataenda kusemea Gwantanamo.
 
Na wale watakaofichua ufisadi ndani ya chama, serikali na mashirika yetu ambao unasababisha nchi yetu kutoendelea watazawadiwa nini!?

Bubu hapa umenichekesha kweli.

Yaani unatarajia serikali ya mafisadi imzawadie mtu anayewaumbua hadharani? Yaani kwa mfano leo tusikie Dr. Slaa kazawadiwa tuzo ya utumishi uliotukuka!

Kwi kwi kwi kwi kwi!

Itabidi na hapa jambo forums watupe wote Phd!
 
Hivi hili wazo kweli ni zuri au ni matumizi mabaya ya fedha?

Mimi nadhani haya ni matumizi mabaya ya fedha. Hii ni proof kwamba jeshi la polisi limeshindwa kazi yake. Hii ni proof kwamba wanasiasa wanatufanyia usanii tu. Wao ndio wateja wakubwa wa hawa waganga. Hapa tunapigwa changa la macho. Wanataka ikifika uchaguzi watuambie "Katika juhudi zetu za kupambana na mauaji ya albino, serikali ilitangaza dau la Tsh 20,000,000 kwa yeyote yule atakayesaidia kukamatwa kwa wanaohusika" and blah blah blah.
 
Mimi nadhani haya ni matumizi mabaya ya fedha. Hii ni proof kwamba jeshi la polisi limeshindwa kazi yake. Hii ni proof kwamba wanasiasa wanatufanyia usanii tu. Wao ndio wateja wakubwa wa hawa waganga. Hapa tunapigwa changa la macho. Wanataka ikifika uchaguzi watuambie "Katika juhudi zetu za kupambana na mauaji ya albino, serikali ilitangaza dau la Tsh 20,000,000 kwa yeyote yule atakayesaidia kukamatwa kwa wanaohusika" and blah blah blah.

huoni kwamba kama fedha hizi zikipangwa na kutumiwa vyema zinaweza kuchochea watu kufikiria mara mbili kula njama ya kufanya mauaji ya kupata laki tano, wakati wakimsaliti mwenye mpango huo anaweza kupata kupata milioni moja?
 
Back
Top Bottom