Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 77
na Marietha Mkoka, DSJ
RAIS Jakaya Kikwete amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es Salaam, Patrick Tsere kuwa balozi mpya nchini Malawi.
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa vyombo habari, ilisema Tsere anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Makame Rashid ambaye amestaafu kwa mujibu wa utumishu wa umma. Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema Tsere ameshika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala tangu mwaka 2006 hadi 2009.
NB: Atakwenda tena Karatu kugombea Ubunge kama ilivyokuwa mwaka 2005??