Haipo chini ya Wizara ya Elimu bali ni Idara ndani ya Ofisi ya Rais-Tume ya Utumishi wa Umma.ni taasisi ndani ya wizara ya elimu.
1.kumfukuza na kumwajiri mwalimu kazi
2.kumsimamisha mwalimu kazi au kumpa nusu mshahara.
3.inaongeza vyeo vya walimu na kupandisha mishahara
4.kuingia mkataba na walimu wapya kwa niaba ya serikali.
kwa ufupi ndivyo niujuavyo.mia
Mkoa gani huo Mkuu? Hata hivyo jambo la msingi sio mavazi ya kiofisi ila mavazi rasmi na T-shirt sio vazi rasmi labda kwa watu kama bank na NSSF kuna siku kama Ijumaa au J'mosi wanavaa T-shirt (sare). Kuna waraka wa mavazi kwa mtumishi wa umma, tafuta na usome utajua kwanini huyo Katibu alikusumbua. Kuna Mwalimu alikwenda kwenye semina ya kusimamia mitihani ya darasa la saba akiwa na rasta jamaa wakambana sana. Alijitetea akidai ni dini yake, Afisa Elimu kimya kimya akfuatilia mkataba aliojaza akiwa wilaya nyingine ikathibitika jamaa alijaza dini yake kama Mkristo basi ikala kwakeGreater thinkers nawashukuru na nitaendelea kuwashukuru kwa michango yenu.Niende mbele kidogo kwa kuelezea kisa cha mimi kuambiwa mpaka nijue majukumu ya tsd ndio fomu zangu zipokelewa.
Nilienda ofsi za tsd nikiwa nimevaa t-shirt (nzuri tu) na suruali ya kadet (nzuri pia) na ndipo msala ulianzia hapo. Nikaambiwa hayo mavazi hayatakiwi kwa mtumishi wa serikali.Mi nikajitetea nikasema ninapokuwepo kazn kwangu sivai hvyo.Akaniambia hata hapo (ofsi za tsd) niko ofsin kwangu na mm nikamkatalia na ndo chanzo cha kutoelewana.Wadau tuhabarishane hilo ni kosa?