Trump: Nachunguzwa mimi binafsi

mteulethebest

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
261
250
Rais wa Marekani Trump amethibitisha kwamba anachunguzwa yeye binafsi kutokana na hatua yake ya kumfuta kazi mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai la Marekani FBI James Comey.
Kupitia Twitter, Bw Trump amekariri kwamba uchunguzi unaoongozwa na mwendesha mashtaka maalum kuhusu tuhuma kwamba maafisa wa Urusi waliingilia uchaguzi wa mwaka 2016 ili kumfaa Trump hauna msingi.
Ni mara ya kwanza kwa Bw Trump kuzungumzia taarifa kwenye magazeti kwamba anachunguzwa kwa tuhuma za kuhujumu mifumo ya haki kwa kumfuta kazi Bw Comey.
Awali, taarifa kwenye vyombo vya habari Marekani vilikuwa vimeripoti kwamba wasaidizi wake pamoja na watu waliojitolea kusaidia katika kundi lake la mpito wameamrishwa kuhifadhi nyaraka zote kuhusiana na uchunguzi huo wa madai kuhusu Urusi.
Taarifa zinasema mawakili wa maafisa hao wa Trump wametakiwa kuhifadhi nyaraka zote zinazohusiana na Urusi, Ukraine na washauri wengine kadha wa kampeni.
Kuna makundi kadha yanayofanya uchunguzi, kundi moja likiongozwa na mkurugenzi wa zamani wa FBI Robert Mueller, ambayo yanachunguza iwapo maafisa wa Trump walishirikiana na maafisa wa Urusi wakati wa kampeni.
Bw Trump amekana tuhuma hizo.
 

Attachments

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,447
2,000
Mailluminat yalimtaka clinton ili aanzishe vita wale damu leo wanatumia hila zote jamaa huyu akipona bahati yake...watafanya njia zote wamtoe...hebu.fikiria Rais hana absolute Power ya kumfukuza mtu kazi hii kwa upande mwingine ni mzuri kibongo bongo mana ingepunguza tumbua
 

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,318
2,000
Wazungu wanapenda sana kesi na kila kitu wanataka kukigeuza kuwa kesi.
 

Yamakagashi

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
8,682
2,000
Kwa wenzetu ni raha sana,,njoo bongo uone kama kuna mwenye uwezo wa kumchunguza mkuu wetu,,weeeeeeee atakiona cha mtema kuni,sisi ni dunia ya mwisho kwa kweli
Sio kumchunguza, kumuongelea tu kiongozi kwenye vita ya makinikia ni marufuku

Bongo bahati mbaya tu...
 

hukumundo

JF-Expert Member
Oct 8, 2011
830
500
Mailluminat yalimtaka clinton ili aanzishe vita wale damu leo wanatumia hila zote jamaa huyu akipona bahati yake...watafanya njia zote wamtoe...hebu.fikiria Rais hana absolute Power ya kumfukuza mtu kazi hii kwa upande mwingine ni mzuri kibongo bongo mana ingepunguza tumbua
Achana na box la "illuminati" kwanza halafu chunguza kama Trump anafanya mambo kama ana akili sawasawa? Illuminati or not, the guy is a time bomb.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom