TRUMP NA UKUTA KUKABILI WIMBI LA ILLEGAL IMMIGRANTS TOKA MEXICO

godson Lomayani

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
538
711
Tangu alipokuwa akifanya Kampeni za kuwania kiti cha Urais nchini Marekani,Donald Trump aliahidi atakapopata nafasi hiyo atajenga ukuta kudhibiti wimbi la wakimbizi kutoka Mexico,amefanikiwa kuingia kwenye Jumba Jeupe na sasa anashinikiza kuidhinishiwa Fungu la kutosha na Bunge la Nchi hiyo ili aweze kutimiza ahadi yake lakini amekutana na kikwazo Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi na wabunge wa Democratic wameonyesha kuwa tofauti na BOSS wao kwa kugoma kupitisha fedha anazohitaji ili huo ukuta wa kudhibiti wahamihaji haramu uweze kujengwa. Marekani ina mchanganyiko wa raia wa nchi mbalimbali duniani ambao ndio wanalifanya Taifa hilo lenye nguvu ya kiuchumi na kiulinzi kusonga mbele katika nyanja zote hizo,Kama sio hao Wahamihaji bila shaka Marekani isingefika hapo ilipo. Mpango wa Trump kuzuia Wahamihaji utafanikiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sioni kosa la Trump.Kuna wanafiki wa kitanzania eti wanamlaumu Trump eti mbaguzi wakati sisi Tanzania kila siku tunawakamata waethiopia na kuatupa jela.Bora yeye anayewazuia wasiingie kuliko sisi tunaowafunga jela.Kila nchi ina haki ya kulinda mipaka yake na wala si ubaguzi.
 
Back
Top Bottom