Trump: Kuweza kushinda vita dhidi ya wauza madawa inabidi kuwa mkali ikiwa ni pamoja na adhabu ya kifo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa mpango wake uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu wa kupambana na matumizi ya madawa ya kutuliza maumivu kupita kiasi Jumatatu .

Katika hotuba kwenye mkutano huko Manchester New Hampshire Trump aliahidi kuwepo na kizazi kisichotumia madawa akisema kwa pamoja tutamaliza janga hili la ulevi wa madawa hapa Marekani moja kwa moja.

Trump amesema ili kushinda inabidi kuwa mkali kwa wauza madawa .

"Kama tusipokuwa wakali kwa wauza madawa tunapoteza muda wetu”.Na ukali huo ni pamoja na adhabu ya kifo aliongeza huku waliokuwa wakimsikiliza wakimpigia makofi.

Kiongozi wa walio wachache bungeni Nancy Pelosi ameonya kwamba mapendekezo ya rais yanahitaji fedha au yataishia kuwa ahadi hewa kutoka utawala wake.

Bajeti ya Trump ilipendekeza makato makubwa fedha za huduma kwa wazee,idara ya magonjwa ya kuambukliza , magonjwa ya akili na utumizi mbaya wa madawa ambao ulikuwa ni muhimu kusaidia familia zinazopambana na matumizi mabaya ya madawa hayo ya kutuliza maumivu.

Amefanya kazi kuharibu mpango wa afya wa gharama nafuu na kuruhusu uuzaji wa bima isiyo na faida kwa wengi ambayo haihudumii walioathirika na madawa. Na sasa Rais Trump anazungumzia kuweka adhabu ya kifo kwa makosa ya madawa" Pelosi alisema.

Bado haijafahamika ni jinsi gani waendesha mashitaka wanaweza kuomba adhabu ya kifo bila kubadili sheria za Marekani baadhi ya wasomi wa sheria wanasema jambo hilo huenda ikabidi kuamuliwa na mahakama ya juu ya Marekani.


Chanzo: VOA
 

Attachments

  • E6519179-E991-4F92-B09F-D511E9D0E25D_w1023_r1_s.jpg
    E6519179-E991-4F92-B09F-D511E9D0E25D_w1023_r1_s.jpg
    25 KB · Views: 28
Rais Donald Trump amesema kuwa anataka kuweka adhabu kali ikiwemo ya kifo kwa wale watakaobanika kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Amesema hatua hiyo inalenga kukabiliana na ongezeko kubwa uraibu ndani ya Marekani.

Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa New Hampshire amesema wauzaji wa dawa za kulevya wamesababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa kufungwa wanakaa muda mfupi tu gerezani jambo ambalo anasema haridhishwi nalo.

Ameongeza kuwa tatizo hili linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara pamoja na kutenga fedha.

"Mwezi Oktoba tulitangaza tatizo hili kama janga la dharula kiafya ambalo limedumu kwa muda mrefu.Tumelifanyia kazi na Bunge kuhakikisha tunatenga kiasi cha dola billion sita katika bajeti mpya ya mwaka 2018/2019 ili kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya,ambapo tutakuwa tumetenga kiasi kikubwa cha fedha kuwahi kutokea dhidi ya tatizo hili."

(Chanzo:BBC)
 
Back
Top Bottom