Trump: Kibonyezo changu cha nyuklia kina nguvu kuliko cha Kim

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
8,235
8,712
Trump: Kibonyezo changu cha nyuklia kina nguvu kuliko cha Kim
_99444451_53fcfaf5-7dec-4ec6-aa1e-a06fbdad2df5.jpg
Haki miliki ya pichaEPA
Image captionTrump: Kibonyezo changu cha nyuklia ni kikubwa kuliko cha Kim
Rais wa Marekani Donald Trump amejigamba kuwa kibonyezo chake cha silaha za nyuklia ni kikubwa na kilicho na nguvu zaidi kuliko kile cha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un.

Ujumbe wa Twitter wa Trump ndio wa hivi punde wakati ya majibizano kati ya viongozi wa mataiafa hayo mawili yaliyo na silaha za nyukiia.

Mapema wiki hii Kim alionya kuwa kibonyezo chake cha nyuklia kawaida kiko kwenye meza yake.

Korea Kaskazini inadai kuwa ina silaha za nyulia na inaweza kuishambulia Marekani huku wadadisi wakisema kuwa ikiwa Korea Kaskazini ina silaha za nyulia haibainiki ikiwa ina teknolojia ya kuzitumia.

Kando na kuitishia Marekani, ujumbe wa mwaka mpya wa Kim pia uliwashangaza wengi wakati alisema kuwa alikuwa aayari kwa mazungumzo na Korea Kusini na ange[penda kuituma timu kwa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi nchini Korea Kusini mwezi ujao.
 
Hawa wanalao jambo.

Dawa yao waingie ulingoni wapigani mpka watoane damu.

Biashara yakutumia jeshi kumwaga damu zisizo na hatia haina maana.

Watengewe ulingo bila refa watwangane mpka mmoja atoke nyongo.
 
Vita ni nzuri endapo wewe sio mlengwa wakuuliwa ila kama wewe ndio target ya kuuwawa ni lazima uombe suluhu

Watanzania wengi tunashabikia hawa vidume wapigane kwasababu sisi sio walengwa ila tungekua ni walengwa nahisi tungekua tunakesha kumuomba mungu haya yasitupate
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom