Trump kakurupuka. Na wamerekani wako njia panda

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,833
2,000
Bado vumbi halijatulia tangu kuuwawa kwa commando Jenerali wa Iran.. Alikuwa ni mtu muhimu namba moja wa mikakati yote ya kivita mashariki ya kati na nchi jirani pia

Kuna taharuki kubwa duniani kutokana na kifo hicho cha kichokozi kwakuwa tayari Iran imesema italipa kisasi na marekani nayo kupitia Trumph imesema inalitambua hilo na iko tayari kwa vita... Cha kusikitisha ni kwamba hakuna aliye tayari vita ipiganwe kwake wote chokochoko zao wamezipeleka Iraq.

Kuna mengi sana yameshasemwa kwenye hii vita inayonukia lakini kuna machache yanatoa ujumbe wa kutisha.. Hebu tujaribu kuyapitia moja baada ya jingine

1. Hili japo halisemwi sana kwasasa lakini limemuokoa Trump kutoka kutolewa madarakani.. Wamerekani ghafla wamekuwa wakimya na pengine wamoja kwa sasa lakini pia wamebaki na kiwewe na bado wako njiapanda kwakuwa bado hawajasahau madhara yaliyofuatia baada ya vita ya Iraq na kumuua Saddam Hussein.. Kuna siku watakuja kumuwajibisha Trump...

2. Katikati ya hili sekeseke Henry Kissinger katibu mkuu mstaafu wa marekani aliyekuwa kuwa kimya miaka mingi aliibuka na kuongea mengi mazito.. Kwamba vita hii wamerekani walikuwa wameshajiandaa nayo siku nyingi sana na baada ya kufanya mengine yote.. Vita hii ni msumari wa mwisho kwenye nchi ya Irani na baada ya hapo NWO itasimikwa rasmi huku akiwananga wachina na warusi kuwa itakapofika muda wa wao kuacha ujuha na upumbavu marekani atakuwa ameshamaliza kazi

Anaendelea kujigamba kuwa walishafanya maandalizi yote muhimu na KUWEKEZA kwenye silaha za kisasa na technology ya vita ambayo haipatikani popote ulimwengu na pia wana jumuiya kubwa ya kiislam iko nyuma yake kwakuwa walishawekeza kwao kitambo kwenye mengi

Anasisitiza kwamba vita itapiganwa na watashinda na baada ya hapo watakaobaki (wenye nguvu) ni wao na Israel tuu... Wengine wote watafuata wanachokisema wao...

3. Kissinger, Trump, Balozi wa Iran US na wengine wanataja uwekezaji mkubwa wa silaha na medani za vita kwamba vimekwisha igharimu marekani Dollar trillion 7.. Lakini Balozi wa Iran kwa utulivu kabisa anahoji kwa kuwekeza ama kupoteza kiwango kikubwa namma hiyo cha pesa kwenye silaha nzuri na za kisasa kumeifanya marekani kuwa salama
Balozi anasema watu ndio wanatawala dunia na si silaha.. Na ndio maana pamoja na mmarekani kuwekeza matrilion ya dola kwenye silaha lakini bado haiko salama asilimia mia moja iwe ndani ya US ama nje.. Lakini wao Iran wana watu...

4.Watu wanaitabiri kuwa inaweza kuwa vita ya tatu ya dunia na itapiganwa kwa silaha za nyuklia.. Hili haliwezi kutokea kwakuwa wote wenye hizo silaha wameelekezeana mitutu. Mtusi na Mchina wanatamba kuisambaratisha New York kwa dakika chache tuu huku mmarekani naye akitamba kufanya hivyo kwao

5. Kuna jambo la hatari sana linaweza kutokea... Kama kweli wakiamua kupigana basi hii inaweza kuwa vita ya kikanda na kidini.....
Kuna nchi zitaamua tu kumuunga mmarekani mkono kwakuwa anawapa misaada na pengine anaonekana kama anaupigania ukristo.. Na kuna nchi zitaamua tu kumuunga Iran mkono kwakuwa zitaona kama Iran ni taifa la kiislam hivyo kulishambulia ni kuushambulia uislam... Hapa Saudi Arabia atakuwa na hali ngumu sana

6. Ni wazi kabisa kuwa mmarekani ameiweka dunia kiganjani na anajua nini kinaendelea wapi na ni nani anafanya nini.. Na ya kwamba uamuzi wa kushambulia ama kuua hubaki kwa rais... Ndio maana report zinasema alitoa kibali Jenerali Soleiman auwawe ni rais wa marekani..

Mwisho wa yote tumejumuishwa kwenye mambo tusiyoyajua kwa hakika undani wake huku propaganda zikiendelea kila upande ili kutafuta kuungwa mkono na kujimwambafy... Lakini je mbona sioni aliyehoji ukimya wa baraza la usalama la umoja wa mataifa?

Wamarekani kwa sasa wako njiapanda na hawana amani popote pale ulimwenguni.. Wanaishi kama panyabuku na nguchiro mapangoni.. Wanajua wanatafutwa... Mpango wao wa siri wa kuyauza makanisa kwa ulimwengu wa kiislam ili yawe misikiti na baadae waje kuuchakachua uislam ulikuwa unaenda vema lakini wa republican wapenda vita wameutibua..... Japo vita hii pia inaonesha ni mpango wamuda mrefu wa kuudhoofisha Uislam duniani na wanamuona Muiran kama kikwazo kilichobaki kwakuwa msaudi keshamalizwa..

Yote juu ya yote tusiombe vita hii itokee... Na wamarekani wakumbuke kiporo chao cha kumtimua trump

Iran-orders-its-proxies-to-prepare-for-war-.jpeg
maxresdefault-1.jpeg
downloadfile-12.jpeg


Jr
 

Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
9,165
2,000
Mshana Jr,
Akina Kisinger ndo Matajiri wanaomiliki hisa katika viwanda vya silaha huko USA na kwingine duniani, nachokiona Trump hawezi kupeleka wanajeshi wakaumie tena katika ardhi ya Iran, mikwara yake itasababisha Saudia na nchi zote za waislam wa Sunny kununua silaha za USA kwa ajili ya kujilinda, hivyo na kumsababishia USA na matajiri wake kuingiza pesa, Mafuta yatapanda bei duniani na baada ya miaka michache Uchumi wa dunia utadorora (Recession)
Mikakati ya USA ni kama walivyomfanya Iraq ya Saddam wanaweka vikwazo baada ya miaka hata 10 ukidhoofika wanakuja kukupiga.

Suala la Impeachment linarudi tena kwa kasi, nimeona Watu kadhaa wameibua video za Trump za mwaka 2011/12 akimlaumu Obama kuwa anataka kuipiga Iran ili ashinde uchaguzi sasa umekuwa vice versa mwaka huu mtamu huko USA.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,833
2,000
i missed these points... Kissinger ndio mjenzi wa Mason huko.. Ni mkandarasi wa kutumainiwa na anajua anachoongea lakini shida IMO kwa Trump.. Hashindwi kufyatuka muda wowote
Akina Kisinger ndo Matajiri wanaomiliki hisa katika viwanda vya silaha huko USA na kwingine duniani, nachokiona Trump hawezi kupeleka wanajeshi wakaumie tena katika ardhi ya Iran, mikwara yake itasababisha Saudia na nchi zote za waislam wa Sunny kununua silaha za USA kwa ajili ya kujilinda, hivyo na kumsababishia USA na matajiri wake kuingiza pesa, Mafuta yatapanda bei duniani na baada ya miaka michache Uchumi wa dunia utadorora (Recession)
Mikakati ya USA ni kama walivyomfanya Iraq ya Saddam wanaweka vikwazo baada ya miaka hata 10 ukidhoofika wanakuja kukupiga.
Suala la Impeachment linarudi tena kwa kasi, nimeona Watu kadhaa wameibua video za Trump za mwaka 2011/12 akimlaumu Obama kuwa anataka kuipiga Iran ili ashinde uchaguzi sasa umekuwa vice versa mwaka huu mtamu huko USA.

Jr
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,833
2,000
Hali si nzuri. Kauli za huyo Kiongozi wa Iran kwenye hiyo clip hapo juu ni nzito ingawa ameongea kwa utulivu kabisa na walishaangamiza {askari 80.(!? )}

"We have people on our side, that is much important. The USA believe on beautiful military equipment. Beatiful military equipment cannot rule the world, people rule".....


Jr
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,596
2,000
Lkn D.Trump siyo NWO, kwanza ndo mpingaji mkubwa wa nwo, hata hii Vita ya kutengeneza ya ,,impeachment” ni sababu hiyo, kwamba D.Trump ni kizingiti kwa ma global elites, D.Trump alichaguliwa shauri alikampeni dhidi ya nwo global elites rejea hata hotuba zake UN alipinga globalism live, hata juzi kati kasema ,,USA will never be a socislist country” !
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,596
2,000
New World Order ni kitu kikubwa kuliko huyo chizi mcheza mieleka ndio maana nikasema soon wamarekani watakumbuka impeachment

Jr


Unamuita D.Trump chizi lkn ana Wamarekani nyuma yake ambao hawataki nwo na ndo maana wakamchagua D.Trump badala ya globalist Clintons, isitoshe Wamarekani wako tayari kuingiia civil war kuliko kukabidhi nchi yao kwa maglobalist ambao ni communist, na ndo maana wanatetea ,,second amendment” ambayo inaruhusu kumiliki silaha na kutetea nchi yao hata kwa Vita kama Serikali ikileta communism ya global elites.

Jiulize kwa nini USA imekataa kuitambua Mahakama ya nwo ICC huko Hague, kwa nini imejitoa Paris Climate agreeement, kwa nini imejitoa unesco na mambo mengine mengi, kwanza hata wanataka kujitoa WTO world trade org. kama wto waipofanya reforms, ...
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,833
2,000
Trump na hao walioko nyuma yake hawataweza kamwe kuizuia NWO kwakuwa ni mpango mkakati uliosukwa kwa akili kubwa na ni kandarasi ya mabilioni ya dollar..na ya muda mrefu mbo
Unamuita D.Trump chizi lkn ana Wamarekani nyuma yake ambao hawataki nwo na ndo maana wakamchagua D.Trump badala ya globalist Clintons, isitoshe Wamarekani wako tayari kuingiia civil war kuliko kukabidhi nchi yao kwa maglobalist ambao ni communist, na ndo maana wanatetea ,,second amendment” ambayo inaruhusu kumiliki silaha na kutetea nchi yao hata kwa Vita kama Serikali ikileta communism ya global elites.

Jiulize kwa nini USA imekataa kuitambua Mahakama ya nwo ICC huko Hague, kwa nini imejitoa Paris Climate agreeement, kwa nini imejitoa unesco na mambo mengine mengi, kwanza hata wanataka kujitoa WTO world trade org. kama wto waipofanya reforms, ...
New World Order or NWO is claimed to be an emerging clandestine totalitarian world government by various conspiracy theories.[3][4][5][6][7]

The common theme in conspiracy theories about a New World Order is that a secretive power elite with a globalist agenda is conspiring to eventually rule the world through an authoritarian world government—which will replace sovereign nation-states—and an all-encompassing propaganda whose ideology hails the establishment of the New World Order as the culmination of history's progress. Many influential historical and contemporary figures have therefore been alleged to be part of a cabal that operates through many front organizations to orchestrate significant political and financial events, ranging from causing systemic crises to pushing through controversial policies, at both national and international levels, as steps in an ongoing plot to achieve world domination.[3][4][5][6][7]

Before the early 1990s, New World Order conspiracism was limited to two American countercultures, primarily the militantly anti-government right and secondarily that part of fundamentalist Christianity concerned with the end-time emergence of the Antichrist.[8] Skeptics, such as Michael Barkun and Chip Berlet, observed that right-wing populist conspiracy theories about a New World Order had not only been embraced by many seekers of stigmatized knowledge but had seeped into popular culture, thereby inaugurating a period during the late 20th and early 21st centuries in the United States where people are actively preparing for apocalyptic millenarian scenarios.[4][6] Those political scientists are concerned that mass hysteria over New World Order conspiracy theories could eventually have devastating effects on American political life, ranging from escalating lone-wolf terrorism to the rise to power of authoritarian ultranationalist demagogues.[4][6


Jr
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,596
2,000
Mshana Jr,
Usijiamini hivyo Dunia imeanza kuamka, Brexit ni moja ya sababu ya kupinga nwo, na mengi yanafwatia, sasa hivi nchi nyingi za West Wananchi wanachagua watu type ya D.Trump, kuanzia Australia, Urusi, Uingereza na hata Brazili kuna Bolsonaro, Chile kote huko ni Trump type, ni global movement dhidi ya nwo, na ndo mwanzo tu.

Shida ni hao global elites hawawezi kuweka nwo bila ya kutumia communism, na USA haitaki communism, hivyo patachimbika hapo.
Usisahau communism iliuwa
watu
> milioni 100 Uchina na Soviet Union ili kulazimisha communism, ...
 

sido9797

Senior Member
Aug 15, 2018
161
225
Iran hana uwezo wa kumpiga marekani kivyovyote,zaidi ya kushambulia base za marekani zilizo mzunguka.
Lakini hio sio sababu ya yeye kusita kulipiza kisasi kwa sababu nyuma yake kuna nchi tatu muhimu zinazo mpa kiburi iran 1.urusi2. China. 3. North korea akiliamsha kaamsha hao watu.

Marekani anajua missiles za iran zinaenda kilometa 3000km ambazo hazifiki washington.Ndio anamtesa huyu iran
Hivyo licha ya mazaifu yote hayo iran imepania kulipiza kisasi na ipo tayari kwa vita lakini marekani ameogopa kwa kutazama mbali kwa kuziona nchi kama north korea zenge missiles ambazo zinafika kilometa 13000km au mile 8000 hv.urusi na china ambao wanatamani marekani anguke binafsi naona ni propaganda tu hizo za marekani kuogopa vita mana ndio collapse yake na iran haijatangaza kua imeridhika na ilichokifanya kama kisasi.Sent using Jamii Forums mobile app
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,586
2,000
Shift of technology from fossil energy has and will shake it vehemently.
Aftermath will meet and witness consumer confidence shifting.

Elite are always elite. They have so many options.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,833
2,000
Majaribio kadha yalikwishafanyika hasa ya kuangamiza dunia ya tatu
Kwa magonjwa hata ya kupandikiza
Kwa vita
Kwa vyakula kama GMO
Kwa vinywaji vunavyoua taratibu
Kwa sumu mbalimbali kupitia madawa nknk
Actually project za kuangamiza ni nyingi na karibia zote zilishafanyiwa majaribio dunia ya tatu na matokeo yakawa mazuri sana...

Kitu kimoja kibaya sana ni kwamba wameshatu brain wash na kwasasa wanafikiri na kupanga kwa niaba yetu
Shida ni kwamba wanataka kuleta communism Dunia nzima na kama ilivyokuwa Uchina au Ulaya Mashariki ni ngumu sana kusambaza commumism bila ya kuuwa mabilioni ya watu wa leo hii, unajua kwamba moja ya ajenda ya nwo ni kubakiza watu nusu bilioni tu Dunia nzima? Sasa hivi Dunia nzima iba watu > bilioni 7, sasa hao mabilioni ya watu watawauwaje?

Kuhusu Bolivia inachanganya kwa maana Morales ni communist, hivyo ni sehemu ya nwo, ...

Jr
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom