Trump Kaanza Kuwatimua Watu Marekani.......Tayari Wasomali 90 na Wakenya 2 wameondolewa Marekan

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
72ef4c669191bddec9d5e4ef659c57b6.jpg
Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.


Wote wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.


Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba raia hao wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu.


Bw Trump alisema Jumatano itakuwa siku muhimu kwa usalama wa Marekani.


Anatarajiwa kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda Marekani.


Nchi hizo ni Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen
 
kama hawana hati halali vyema ila atakumbana na changamoto nyingi hasa za adui wa nchi yake maana unapoamua kupuliza moto kumbuka na cheche
 
Kwa ufupi trump atatekeleza mambo mengi sana aliyoyasema japo watu wengi wanafikikia tofauti kuwa USA hapa Trump atapingwa sana ila siyo.

Pia, mradi wa ukuta unajengwa kati ya USA na Mexico amesaini jana executive order .

Hapo napo, wote tukumbuke kuwa hizo ndiyo sera zilizompitisha Trump kuwa rais kwa hiyo tusubirie mengi na ambayo hakuyataja katika majukwaa.

Mfano, namnuukuu Trump katika moja wapo ya hotuba katika kampeni alisema, *jeshi la USA na special forces wote ifike mahali ambapo wakiisha maliza kuwapiga ISS na magaidi popote pale ndiyo walete mrejesho, na siyo kutangaza kuwa kesho wanaenda kushambulia eneo fulani*

Hiyo maana yake ni kuwa; yeye mwenyewe pana mengi sana atakayofanya bila kusema matokeo yake tu yataongea.

Hivyo, bado kazi ni pevu na sisi huko Africa ifike sasa wakati tuache kutokwa povu ni wakati wa kufanya kazi maana Trump siyo mtu wa kisportsport kabisaaa!
 
Obama aliwabeba wakenya wake kama kwao wamekutana na kigingi
 
Back
Top Bottom