Trump atishia kuzifungia NBC TV na nyingine zinazopotosha

Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
818
1,000
Rais Donald Trump wa Marekani ameviamuru vyombo husika vya nchi hiyo kukinyang'anya leseni kituo maarufu cha televisheni cha NBC, baada ya kutangaza habari za uongo"fake news" kwamba rais Donald Trump anataka Marekani iwe na nguvu za nyuklia mara 12 zaidi ya uwezo walionao sasa.(chanzo bbc world)

=====

Rais Donald Trump ameendeleza mgogoro wake na vituo vya runinga nchini humo akisema kuwa vimekuwa na upendeleo na kuonya kwamba atafutilia mbali leseni zao.

Alikasirishwa na ripoti ya kituo cha habari cha NBC iliodai kwamba kwamba aliwaagiza maafisa wake wa usalama na majenerali kwamba alitaka kuongezwa kwa kiwango kikubwa silaha za kinyuklia nchini humo.

Rais huyo alisema kuwa habari hiyo ilitungwa.

Waziri wake wa ulinzi Jim Mattis aliitaja taarifa hiyo kama isiokuwa ya ukweli.

Wiki iliopita NBC iliripoti kwamba waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alimuita bwana Trump 'mtu mjinga' matamshi ambayo Bwana Tillerson hajayapinga lakini ambayo rais Trump ameyataja kuwa habari bandia.

Wanahabari wanasema kuwa rais huyo atapata shida kufutilia mbali lesen za vyonbo vya habari.

Zinadhibitiwa na tume ya mawasiliano nchini humo.

Lakini baadhi ya makundi ya kupigania haki yanasema kuwa rais Trump anaweka mfano mbaya kwa viongozi wengine.

Chanzo: BBC Swahili
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,457
2,000
Rais Donald Trump wa Marekani ameviamuru vyombo husika vya nchi hiyo kukinyang'anya leseni kituo maarufu cha televisheni cha NBC,baada ya kutangaza habari za uongo"fake news" kwamba rais Donald Trump anataka Marekani iwe na nguvu za nyuklia mara 12 zaidi ya uwezo walionao sasa.(chanzo bbc world)

This is fake news too!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom