Trump apigwa tena chini na Mahakama baada ya kukata rufaa!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,265
23,198
Breaking News!
A federal appeals court refused Thursday to reinstate President Donald Trump's ban on travelers from seven predominantly Muslim nations, dealing another legal setback to the new administration's immigration policy.

In a unanimous decision, the panel of three judges from the San Francisco-based 9th U.S. Circuit Court of Appeals declined to block a lower-court ruling that suspended the ban and allowed previously barred travelers to enter the U.S. An appeal to the U.S. Supreme Court is possible.

The court rejected the administration's claim that it did not have the authority to review the president's executive order.

Ruling: 3-0

Amri ya hovyo ya kukurupuka ya travel ban ya Rais wa Marekani Donald Trump imepigwa tena chini na jopo la majaji watatu kama unlawful and unconstitutional! Trump alikuwa amekata rufaa kupinga amri ya Jaji iliyopiga stop Executive order yake na kutaka hukumu hiyo itenguliwe.

Kwa kweli wenzetu wako mbali...kuwa Rais si warrant ya kutoa kauli za hovyo za kukurupuka halafu mihimili mingine ya dola ikakaa kimya kama kwetu. Rais ni mtumishi tu wa wananchi na si mungu-mtu kwamba akikohoa tu watu wanatetemeka! Katiba ya nchi haichezewi hovyo.
 
Amri ya hovyo ya travel ban kukurupuka ya Rais Donald Trump imepigwa tena chini na jopo la majaji watatu kama unlawful and unconstitutional! Trump alikuwa amekata rufaa kupinga amri ya Jaji iliyopiga stop Executive order yake na kutaka hukumu hiyo itenguliwe.

Kwa kweli wenzetu wako mbali...kuwa Rais si warrant ya kutoa kauli za hovyo za kukurupuka halafu mihimili mingine ya dola ikakaa kimya kama kwetu. Rais ni mtumishi tu wa wananchi na si mungu-mtu kwamba akikohoa tu watu wanatetemeka! Katiba ya nchi haichezewi hovyo.
Natamani sana hii kitu ije hata huku yaani hata tukipata uhuru wa kujieleza tuu itasaidia
 
Be the first 2reply!!!
Najaribu kufikiria hawa majaji wetu kwa issue kama hii wangefanya nini sipati picha. Sidhani kama tunaye Jaji hata moja mwenye ujasiri wa kumpiga stop Magufuli hata akiamua kuvunja kipengele baada ya kipengele cha Katiba kila asubuhi anapoamka. Kama alivyowahi kuonya Mwalimu Nyerere, ni hatari kuwa na Rais tusiyejua leo kaamka na mfadhaiko gani na hivyo kutoa kauli za ajabu ajabu!
 
Ndugu yngu wapinge???hawaogopi kutumbuliwa!!hii nchi niyajeshi la mtu mmoja wngne wasindikizaji tu,nimaagizo tu fanya hki fanya over!xo vtu vngne tusicompare na dunia ya kwanza sisi hku bdo tunacindikiza Upepo!!acha movie iendelee
 
Najaribu kufikiria hawa majaji wetu kwa issue kama hii wangefanya nini sipati picha. Sidhani kama tunaye Jaji hata moja mwenye ujasiri wa kumpiga stop Magufuli hata akiamua kuvunja kipengele baada ya kipengele cha Katiba kila asubuhi anapoamka. Kama alivyowahi kuonya Mwalimu Nyerere, ni hatari kuwa na Rais tusiyejua leo kaamka na mfadhaiko gani na hivyo kutoa kauli za ajabu ajabu!
Hii inapashwa kuingizwa kwenye syllabus mashuleni/vyuoni kwa wale wanaojifunza sheria maana ni mfano hai. Katiba ni msemaji na mwamuzi.
 
Najaribu kufikiria hawa majaji wetu kwa issue kama hii wangefanya nini sipati picha. Sidhani kama tunaye Jaji hata moja mwenye ujasiri wa kumpiga stop Magufuli hata akiamua kuvunja kipengele baada ya kipengele cha Katiba kila asubuhi anapoamka. Kama alivyowahi kuonya Mwalimu Nyerere, ni hatari kuwa na Rais tusiyejua leo kaamka na mfadhaiko gani na hivyo kutoa kauli za ajabu ajabu!
Tutafika tu usikate tamaa. ..nao pia walianza hivi even worse. ..
 
Katiba ya Tanzania imewekwa kwa jinsi ya kutengeneza miungu watu na sio kuisaidia. Ndio maana ukiwaambia tunataka katiba mpya wanairudisha ile ya zamani.
Katiba za nchi nyingi za ulaya na amerika zimeonesha a 'clear' separation of power na kila organ ina nguvu na hakuna organ yenye uwezo wa kuingilia maamuzi ya organ nyingine.
Hili la Trump na Mahakama ni mfano dhahiri kuwa wenzetu wameendelea kwenye kila nyanja. Kuheshimu katiba na utawala bora.
Safi sana mahakama. Hata kama watakuja marekani magaidi ila atleast haki imetendeka.
 
Hatimaye Ikulu ya Trump yakubali yaishe baada ya rufaa yake kutupwa na jopo la majaji watatu kwani kuendelea kulishupalia agizo hilo kunaweza kuzua utata zaidi. Sasa wanapanga kurudi mezani na kuanza kuandika Executive Order mpya na makini itakayozingatia sheria na isiyoenda kinyume na Katiba ya nchi.

Hii imekuja baada ya kuona uwezekano wa kupata ushindi kwenye Supreme Court ni mdogo kwa namna amri hiyo ilivyotolewa mwanzo na kusainiwa kwa mbwembwe na Trump. Hili ni pigo na linatoa funzo kwa uongozi huu mpya chini ya Trump kuwa makini zaidi katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za serikali.
 
Political diversion imefanya kazi sasa kutatulia ant trump rally hazitakuwepo tena.
 
Political diversion imefanya kazi sasa kutatulia ant trump rally hazitakuwepo tena.
Hapana, moto ndio kwanza ni kama umemwagiwa petroli, wawakilishi wanawekwa kiti moto katika majimbo yao kwa nini wananyamazia mambo ya kipuuzi yasiyozingatia Katiba wala sheria.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Trump's feeling the power of 'the so called Judge' and the Judicial system.
 
Back
Top Bottom