Trump amtaka Biden ajiuzulu kwa kuruhusu Taliban kuteka Afghanistan

Che mittoga

JF-Expert Member
Mar 28, 2017
6,566
2,000
Wa Afghanistan wengi wanataka kuongozwa na Taliban.
Ndio maana wanachukua nchi bila upinzani wowote.
Waachieni Waafghanistan nchi yao chini ya Utawala wa Taliban.
 

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
May 26, 2009
8,584
2,000
Hakuna kitu kama hicho, tena wamarekani wengi wamefurahia uamuzi huu!!kwani hii vita ni miaka 20, sasa kama ni vifaa, mafunzo hadi mishahara USA, ndio alikuwa akiwalipa ili wajiandae kuna siku hatakuwepo, lakini wapi!ni zaidi ya $.bilioni mia moja, zimetumika, .Ni wazi kuwa USA, alijua kuwa akiondoka ndani ya miezi kama 3, watalibani watarudi, lakini sio kwa kisi hii ya kama siku 14 tu, wameshafika KABUL!!hata kama USA, asingeyatoa majeshi yake leo, akasubilia miaka 10, mbele kilichotokea leo ndicho kingekuja tokea tu!!!
Watu wanashindwa kuelewa. Hakuna muafghanistan anataka kuwa jeshini bila mmarekani.

Kilichofanyika mmarekani kaondoka wanajeshi wa afghanistan nao wamerudi makwao kwenda kunywa kahawa.

Taliban wamechukua nchi bila resistance yoyote. Hakuna jeshi Afghanistan, wenye jeshi lao wamemaumua kurudi Kwao.
 

binbaraghash

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
3,539
2,000
Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amemtaka mrithi wake, Joe Biden ajiuzulu baada ya wanamgambo wa Taliban kudhibiti Mji Mkuu wa Afghanistan, Kabul, pamoja na Ikulu ya Rais siku ya Jumapili.

Trump amemlaumu Biden kwa ‘kuruhusu’ Wataliban kutawala Afghanistan katika ushindi mwanana licha ya uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini humo kwa zaidi ya miaka 20.

Wanamgambo wa Taliban wamechukua udhibiti wa Mji Mkuu ikiwa ni wiki mbili kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa na Jeshi la Marekani kukamilisha kuwaondoa wanajeshi wake wote nchini humo - Agosti 31. Hata hivyo, mipango ya kuwaondoa wanajeshi wa Marekani ilianza wakati wa utawala wa Trump kwa makubaliano yaliyosainiwa Doha, nchini Qatar, mwezi Februari mwaka 2020, kwa makubaliano ya kuwaondoa wanajeshi wote wa Marekani ifikapo mwishoni mwa mwezi Mei, huku Wataliban wakitakiwa kukidhi vigezo kadhaa ikiwamo kuvunja uhusiano na Al Qaeda.

Baada ya Biden kuchukua madaraka, alisogeza mbele tarehe ya mwisho ya Marekani kuondoa uwepo wake nchini humo kufikia mwezi Agosti bila kuweka masharti yoyote. Trump anamlaumu Biden, akidai Marekani ingeweza kujiondoa kwa njia nzuri zaidi na yenye mafanikio.

“Alichokifanya Biden kitabaki kama moja ya maanguko mabaya zaidi katika historia ya Marekani,” Trump alisema siku ya Jumapili.

Kwa sasa, Marekani ipo katika hatua za dharura kuwaondoa wafanyakazi katika ubalozi wake mjini Kabul, ikiwa ni chini ya mwezi mmoja tu tangu Biden aliposema kuwa Wataliban hawataweza kuchukua utawala wa Afghanistan na kuwa serikali na jeshi la Afghanistan lipo imara dhidi ya Taliban.


Chanzo: AFP

Wanamgambo wa Taliban wameitangaza Afghanistan rasmi kuwa "Ufalme wa Kiislamu wa Afghanistan" (Islamic Emirate of Afghanistan) baada ya kuteka Ikulu ya Rais. [Picha na AP]
Well done Biden., Taliban wana haki zote kuishi katika nchi yao kwa uhuru Taliban ni Waislam kama waislamu wengine ulimwenguni na wao wameenda mbali zaidi kwa kutaka kusimamisha dola ya kiislamu kama ilivyo sharia kwa muibu wa dini yetu.

Na kule Marekani/Makafiri na wao wana uhuru wao na sheriza zao za kitwaghuuti wala hawakeri na mtu kwenye nchi zao na ukiristo wao ndani ya nchi yao.

Napongeza sana Biden ni kiongozi shujaa.

Trump zama zake zimeisha, bado ana mambo ya kishamba kupeleka majeshi na kuzikalia nchi za kiislamu kimabavu ilhali wao wanaishi kwa amani ndani ya nchi yao na ukafiri wao. pale taliban marekani waliua waislamu kibao akiwemo osama bin-landen unafkiri nani atalipa damu zao?

Kwenda zake huko trump, period.,
 

hukumundo

JF-Expert Member
Oct 8, 2011
849
500
Trump yupo sahihi, Biden ni kiongozi dhaifu sana na haelewi nini hasa Cha kufanya katika ofisi yake ya urais. Very incompetent!
What is your evidence? Makubaliano ya kuondoa majeshi Afghanistan yalifikiwa na Trump. Na ilitakiwa waondoke mapema zaidi kuliko alivyofanya Biden. Afghanistan was a double-edged sword. Damn if you withdrew and damn if you didn't.
 

let the caged bird sings

JF-Expert Member
Sep 19, 2020
780
1,000
Well done Biden., Taliban wana haki zote kuishi katika nchi yao kwa uhuru Taliban ni Waislam kama waislamu wengine ulimwenguni na wao wameenda mbali zaidi kwa kutaka kusimamisha dola ya kiislamu kama ilivyo sharia kwa muibu wa dini yetu.

Na kule Marekani/Makafiri na wao wana uhuru wao na sheriza zao za kitwaghuuti wala hawakeri na mtu kwenye nchi zao na ukiristo wao ndani ya nchi yao.

Napongeza sana Biden ni kiongozi shujaa.

Trump zama zake zimeisha, bado ana mambo ya kishamba kupeleka majeshi na kuzikalia nchi za kiislamu kimabavu ilhali wao wanaishi kwa amani ndani ya nchi yao na ukafiri wao. pale taliban marekani waliua waislamu kibao akiwemo osama bin-landen unafkiri nani atalipa damu zao?

Kwenda zake huko trump, period.,
nje na mada. . wewe ni KE au ME?
 

Citizen B

JF-Expert Member
May 13, 2019
6,106
2,000
Mimi ni kristo lakini kwa hili sifungamani na dini yoyote. Binafsi nimeufurahi sana ushindi wa Wataliban.

Ni fedheha kubwa sana nchi ya watu kushikiliwa na majeshi wa mababeru.
Kwani ukristo unaingiaje kwenye siasa za mbali?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom