Trump amtaka Biden ajiuzulu kwa kuruhusu Taliban kuteka Afghanistan

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
500
Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amemtaka mrithi wake, Joe Biden ajiuzulu baada ya wanamgambo wa Taliban kudhibiti Mji Mkuu wa Afghanistan, Kabul, pamoja na Ikulu ya Rais siku ya Jumapili.

Trump amemlaumu Biden kwa ‘kuruhusu’ Wataliban kutawala Afghanistan katika ushindi mwanana licha ya uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini humo kwa zaidi ya miaka 20.

Wanamgambo wa Taliban wamechukua udhibiti wa Mji Mkuu ikiwa ni wiki mbili kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa na Jeshi la Marekani kukamilisha kuwaondoa wanajeshi wake wote nchini humo - Agosti 31. Hata hivyo, mipango ya kuwaondoa wanajeshi wa Marekani ilianza wakati wa utawala wa Trump kwa makubaliano yaliyosainiwa Doha, nchini Qatar, mwezi Februari mwaka 2020, kwa makubaliano ya kuwaondoa wanajeshi wote wa Marekani ifikapo mwishoni mwa mwezi Mei, huku Wataliban wakitakiwa kukidhi vigezo kadhaa ikiwamo kuvunja uhusiano na Al Qaeda.

Baada ya Biden kuchukua madaraka, alisogeza mbele tarehe ya mwisho ya Marekani kuondoa uwepo wake nchini humo kufikia mwezi Agosti bila kuweka masharti yoyote. Trump anamlaumu Biden, akidai Marekani ingeweza kujiondoa kwa njia nzuri zaidi na yenye mafanikio.

“Alichokifanya Biden kitabaki kama moja ya maanguko mabaya zaidi katika historia ya Marekani,” Trump alisema siku ya Jumapili.

Kwa sasa, Marekani ipo katika hatua za dharura kuwaondoa wafanyakazi katika ubalozi wake mjini Kabul, ikiwa ni chini ya mwezi mmoja tu tangu Biden aliposema kuwa Wataliban hawataweza kuchukua utawala wa Afghanistan na kuwa serikali na jeshi la Afghanistan lipo imara dhidi ya Taliban.

Chanzo: AFP

1629096974533.png
Wanamgambo wa Taliban wameitangaza Afghanistan rasmi kuwa "Ufalme wa Kiislamu wa Afghanistan" (Islamic Emirate of Afghanistan) baada ya kuteka Ikulu ya Rais. [Picha na AP]
 
Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
22,391
2,000
Biden ameruhusu kamba ikatikie pabovu na hii itawacost Democrat uchaguzi unaokuja. Trump atapeta kiulaini sana. Wameshamsafishia njia.
 
Lekache

Member
Feb 15, 2021
39
125
Trump yupo sahihi, Biden ni kiongozi dhaifu sana na haelewi nini hasa Cha kufanya katika ofisi yake ya urais. Very incompetent!
 
TsafuRD

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
2,008
2,000
Mimi ni kristo lakini kwa hili sifungamani na dini yoyote. Binafsi nimeufurahi sana ushindi wa Wataliban.

Ni fedheha kubwa sana nchi ya watu kushikiliwa na majeshi wa mababeru.
 
kamdudu

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,126
2,000
kumbe nyuma ya vita kwenye Nchi za kiislam ni Marekani anapigana sisi tunadhani ni wenyewe kwa wenyewe ?
 
Pablo Blanco

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
7,342
2,000
Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amemtaka mrithi wake, Joe Biden ajiuzulu baada ya wanamgambo wa Taliban kudhibiti Mji Mkuu wa Afghanistan, Kabul, pamoja na Ikulu ya Rais siku ya Jumapili.

Trump amemlaumu Biden kwa ‘kuruhusu’ Wataliban kutawala Afghanistan katika ushindi mwanana licha ya uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini humo kwa zaidi ya miaka 20.

Wanamgambo wa Taliban wamechukua udhibiti wa Mji Mkuu ikiwa ni wiki mbili kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa na Jeshi la Marekani kukamilisha kuwaondoa wanajeshi wake wote nchini humo - Agosti 31. Hata hivyo, mipango ya kuwaondoa wanajeshi wa Marekani ilianza wakati wa utawala wa Trump kwa makubaliano yaliyosainiwa Doha, nchini Qatar, mwezi Februari mwaka 2020, kwa makubaliano ya kuwaondoa wanajeshi wote wa Marekani ifikapo mwishoni mwa mwezi Mei, huku Wataliban wakitakiwa kukidhi vigezo kadhaa ikiwamo kuvunja uhusiano na Al Qaeda.

Baada ya Biden kuchukua madaraka, alisogeza mbele tarehe ya mwisho ya Marekani kuondoa uwepo wake nchini humo kufikia mwezi Agosti bila kuweka masharti yoyote. Trump anamlaumu Biden, akidai Marekani ingeweza kujiondoa kwa njia nzuri zaidi na yenye mafanikio.

“Alichokifanya Biden kitabaki kama moja ya maanguko mabaya zaidi katika historia ya Marekani,” Trump alisema siku ya Jumapili.

Kwa sasa, Marekani ipo katika hatua za dharura kuwaondoa wafanyakazi katika ubalozi wake mjini Kabul, ikiwa ni chini ya mwezi mmoja tu tangu Biden aliposema kuwa Wataliban hawataweza kuchukua utawala wa Afghanistan na kuwa serikali na jeshi la Afghanistan lipo imara dhidi ya Taliban.

Chanzo: AFP

Wanamgambo wa Taliban wameitangaza Afghanistan rasmi kuwa "Ufalme wa Kiislamu wa Afghanistan" (Islamic Emirate of Afghanistan) baada ya kuteka Ikulu ya Rais. [Picha na AP]
huyo rais hawajamuua?
 
DAN LOKOMOTIVE

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,208

Ila binadamu huwa hatupendi ukweli kama sikosei hawa hawa watalibani , pamoja na wananchi wa afaghanisatni pamoja hata na wamerakani na jumiya za kimataifa walikuwa wanasihinikiza marekani itoe majeshi yake huko na kulikuwa na mkutano kama sikosei na iongozi wa trump pamoja na wataliban kwamba wataleta amani pindi haya majeshi yatakapoondoka sasa mbon wenyewe hawa watalibani ndio wamepingua serikali na kuua watu na kuteka miji kama wao talibai nia ilikua kumtoa marekani kwa nini wanaua watu wao wenyewe
Pili hivi hiyo nchi ingeendelea kukaliwa na wammarekai mpaka lini siku tuu ingefika wageondoka je ingekuwaje??
 
ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
2,544
2,000
Mimi ni kristo lakini kwa hili sifungamani na dini yoyote. Binafsi nimeufurahi sana ushindi wa Wataliban.

Ni fedheha kubwa sana nchi ya watu kushikiliwa na majeshi wa mababeru.
Watalibani huwajui watu wanajutia sasa kuondoka kwa majeshi ya mabeberu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom