Trump amsifia Sadam

Natalia

JF-Expert Member
Jul 3, 2011
4,324
1,892
Trump msifia Sadam Hussein ' alikuwa kiongozi HASWA Aliua terrorist .Hii SI Mara ya kwanza ya Trump kulaumu serikali ya marekani Kuwaua Sadam Hussein na ghadafi .Trump pia amlaumu Obama kwa fujo za Middle East .Trump haogopi mtu sasa hivi .Leo amesema kutwa Mnasema corruption Africa na wakati clintons ndio wenyewe.Establishment watakoma Trump akishinda
 
Wana jamii,
Nimesoma kwa masikitiko habari hii,
Japo walitolewa kwa ubabe na kwa maslahi ya Marekan wenyewe ila karma inatafuna dunia nzima.maana kwa sasa dunia imekuwa na hofu na IS Kuliko wakati wowote.
Na dunia nzima inalipa ghalama za Vita ile!.
Source:
Trump awakumbuka Saddam, Gaddaf
 
Ushabiki pembeni...kuzivamia Iraq na Libya yalikuwa ni makosa makubwa sana ya kimaamuzi kuwahi kufanyika in the recent global community. Bahati mbaya ni kwamba kila kosa lina gharama yake. Kibaya zaidi tu ni kwamba maamuzi haya ya kijnga ya nchi chache kwasababu tu ya kiburi, jeuri, ubabe na kuangalia shortsitedly kwenye maslahi yao tu ya kiuchumi na ya washirika wao, yanaigharimu dunia nzima...na tishio hili kwa dunia litaendelea kwa muda mrefu sana!!
 
Maisha ya Libya yamekuwa tofaut....maisha yakikuwa ya aman na furaha....maisha ya Uhuru na nafaka...maisha ya shule bure,maji bure,umeme bure,....baghazi kutoka jagwa mpka sehem ya uzalishaji ...na sasa umekuwa mji wa maghofu...itachachukua miaka mingi saana Libya kuja kusimama,na tena mpk kizazi hiki kupita.
 
Wamemaliza kuharibu nchi za Wenzao wakidhani ndio watawahakikishia Maisha bora watu wa Mataifa yao sasa hali ni tofauti. Mwingereza anamuona Mfaransa na Mjerumani ndio chanzo cha shida zake wamejitoa EU nako Ireland ya kaskazin na Scotland hawataki kusalia kwny UK, Sasa wakatafute nchi za kupiga Mabomu kuahirisha ajenda za kichumi za nchi zao maana Mataifa yote makubwa wameshayaharibu
 
Ushabiki pembeni...kuzivamia Iraq na Libya yalikuwa ni makosa makubwa sana ya kimaamuzi kuwahi kufanyika in the recent global community. Bahati mbaya ni kwamba kila kosa lina gharama yake. Kibaya zaidi tu ni kwamba maamuzi haya ya kijnga ya nchi chache kwasababu tu ya kiburi, jeuri, ubabe na kuangalia shortsitedly kwenye maslahi yao tu ya kiuchumi na ya washirika wao, yanaigharimu dunia nzima...na tishio hili kwa dunia litaendelea kwa muda mrefu sana!!

Mkuu hakuna kosa lolote mbele ya wakubwa. Na kila kitu kinaenda kwa ratiba kama ilivyopangwa.
Wewe unathani ni serikali ya ccm kwa matamko na mihemko?
Watu wanajenga master plan in details.
 
Mkuu hakuna kosa lolote mbele ya wakubwa. Na kila kitu kinaenda kwa ratiba kama ilivyopangwa.
Wewe unathani ni serikali ya ccm kwa matamko na mihemko?
Watu wanajenga master plan in details.

Umekariri au umekaririshwa mkuu. Hauko sahihi. Kama umeamua kutokujishughulisha kuutafuta ukweli wote kuhusu mambo mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na vamizi zilizokuwa spearheaded na Marekani with their allies, basi angalau tumia dakika chache tu kufuatilia recent kitimoto anachowekwa Tony Blair na Waingereza wenzake kuhusiana na uvamizi wa Iraq. Kwa taarifa yako amekiri yeye mwenyewe kuwa alipotoshwa na pia hawakuwa na mipango madhubuti ya wakati na baada ya vita ile. Nashangaa wewe unasema kitu ambacho wenyewe wamekiri waziwazi kuwa walikosea. Usikubali kukaririshwa mkuu. Au unaamini wazungu hawakosei na kwamba dunia hii wenye mihemko na kukurupuka ni hao watani zako tu??? Wrong perception! Tujihimize kuwa objective kidogo...unazi na ushabiki usitufanye tuwe vipofu au viziwi au wenye cerebral palsy
 
Trump msifia Sadam Hussein ' alikuwa kiongozi HASWA Aliua terrorist .Hii SI Mara ya kwanza ya Trump kulaumu serikali ya marekani Kuwaua Sadam Hussein na ghadafi .Trump pia amlaumu Obama kwa fujo za Middle East .Trump haogopi mtu sasa hivi .Leo amesema kutwa Mnasema corruption Africa na wakati clintons ndio wenyewe.Establishment watakoma Trump akishinda
Trump pamoja na ukichaa wake anachosema ni kweli, Alqaeda waliona cha moto Iraq hawajahi kulipua hata kibiriti na Libya kulikuwa hakuna hao watu lakini tumeona baada ni mamia ya Alqaida na ISIS huo ndio ukweli. Halafu yule Blair jana the word is better place today. Jamaa pumbavu utasema haoni kinachotokea juzi tu watu 250 killed mambo ya ushia sijui sunni yamekuja baada ya Saddam japo walikuwepo lakini kimyaa.
 
Back
Top Bottom