Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates

Kelvin X

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,939
2,396
Dana Boente amechaguliwa kuwa acting AG





Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu. Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti.

Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali. Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente.

Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni. Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Chanzo: BBC
 
A cracy man has been given a crub, then every one who passes in front of him has to be bitten
 
iyo barua aliyo andikiwa ina personal attacks nyingi, ila pia yule mama alikosea kupeleka maamuzi yake kwenye press

Nakubaliana nawe.

Pande zote zimekosea kwa kiasi chake.

Licha ya hivyo, alichokifanya huyo mama ni kuleta siasa kwenye kazi yake.

Fukuza tu maana hakuna namna.
 
I very much agree with Trump. He campaigned on all these issues. He is simply implementing what he said during the campaign trail. And that's why he was elected.

Sasa hizi kelele Watu wanaandamana siwaelewi aiseee. Wamuache Rais afanye kazi yake. Tatizo watu wamezoea blah blah za wanasiasa. All talk no action! Trump is different. Make America Great Again!
 
Back
Top Bottom