Trump aiomba Mahakama kuzuia taarifa zake zisiingie mikononi mwa bunge

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,091
2,000
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, ameiomba Mahakama ya rufaa kuwazuwia wabunge wanaofanya uchunguzi wa ushiriki wake kwenye ghasia za Januari 6 dhidi ya jengo la bunge, Capitol, kupata taarifa kuhusu mazungumzo na matendo yake wakati huo.

Kupitia mawakili wake, Trump anaitaka Makumbusho ya Taifa pamoja na Kamati ya Kibunge inayochunguza tukio hilo kutokutowa hadharani taarifa hizo. Mahakama ya chini kwamba kumbukumbu za Ikulu ya White House zinapaswa kukabidhiwa kwa kamati hiyo ya kibunge.

Awali, kamati hiyo ilikuwa imeiomba Makumbusho ya Taifa, ambayo kawaida huhifadhi kumbukumbu zote za Ikulu, kuwapa daftari la wageni, mazungumzo ya simu na mawasiliano ya kimaandishi ya Trump na wasaidizi wake.

Wafuasi wa Trump walilivamia jengo la bunge wakitaka kulizuwia kupitisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2020 yaliyompa ushindi Joe Biden dhidi ya Trump.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom