Trump again! Shambulio la anga laua alshabaab zaid ya 100

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,417
9,603
Zaid ya wapiganaji 100 wa Alshabab, ikiwemo makamanda 20 wa Alshabab wanaaminika kuuawa kwenye shambulizi la anga lililotekelezwa na Marekani mapema jana(Jumamosi) katika eneo la El-Adde kusini kwa Somalia.
Wenyeji na maafisa usalama katika eneo hilo ambapo wanajeshi wa Kenya walivamiwa na kuuawa na kundi hilo mwezi januari mwaka jana(2016) walisema kua walisikia ndege za kivita zikiangusha mabomu kwenye maficho ya kundi hilo.
Shambulizi hilo linajiri siku chache baada ya Marekani kusema kuwa itatuma jeshi lake nchini Somalia kutoa mafunzo na vifaa kwa jeshi la Somalia na AMISOM ili kuiwezesha kushinda vita dhidi ya Alshabaab.

Source: China Xinhua News
 
Weka picha ya waliokufa maana siku hizi mkiua mnawaficha tuna ndugu huko Somalia
0a66c858aa112a6641a00288b4513dea.jpg
 
Back
Top Bottom