Trump afungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Maafisa wa kampeni wa rais wa Marekani Donald Trump wamefungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais katika jimbo la Michigan.

Wakati huo huo, Jimbo la Georgia limetangaza kurudia kwa hesabu ya kura jinsi maafisa wa Trump walivyoomba huku rais mteule Joe Biden akiwa anaendelea na mipango ya kupanga utawala wake.

Timu ya kampeni ya rais Trump, imekwenda mahakamani kujaribu kuzuia maafisa wa uchaguzi katika jimbo la Michigan kuidhinisha ushindi wa Joe Biden.

Trump alishinda kura katika uchaguzi wa Michigan, mwaka 2016 lakini akapoteza kwa Biden kwa karibu kura 148,000 katika uchaguzi wa Nov 3.

Biden anaongoza katika jimbo la Georgia kwa kura 14,000 ambalo wademocrat hawajawahi kushinda tangu uchaguzi wa mwaka 1992.

Waziri wa mambo ya nje wa Georgia Brad Raffensperger ametangaza kwamba kura zote zilizopigwa zitahesabiwa upya kuanzia wiki hii na matokeo rasmi kuidhinishwa kabla ya Novemba 20, ambayo ni siku ya mwisho kwa shughuli zote za uchaguzi kukamilika katika jimbo hilo.

Kura zitarudiwa kuhesabiwa kwa njia ya mkono na wala sio mashine.

Trump amekataa kukubali kwamba ameshindwa na Biden katika uchaguzi wa urais uliofanyika Nov 3 na badala yake ametangaza kupinga mahakamani matokeo hayo katika kaunti zilizo katika majimbo aliyoshindwa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Michigan Jake Rollow, amesema kwamba kampeni ya Trump inaeneza madai ya uongo ili kufanya watu wakose Imani na uchaguzi mkuu, akisisitiza kwamba uchaguzi katika jimbo la Michigan ulifanyika kwa njia ya haki na matokeo yake yanaonyesha mapenzi ya wapiga kura.

Wanasiasa maarufu katika chama cha Republican wanamuunga mkono Trump wakisema kwamba ana haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.
 
Ongeza nyama kwa kueleza hilo Jimbo la Michigan lina "ELECTORATE VOTES" ngapi ambazi TRUMP akishinda atakuwa amempiku Biden.
 
Yaani huyu babu inabidi ajitafakari sana. Yaani hata afanye vipi hawezi kumshinda Biden maana alimuacha mbali sana kwa kura na Electoral Votes. Halafu ukiona unapoteza mpaka strong hold yako ujue kuwa hatakiwi kabisa. Trump alianza kukataliwa na Wamarekani mapema sana sema kichwa maji halikujitambua au hakishauriki kama lile lingine lijitapalo kuwa eti ni final say. Hivyo niseme tu kama wakirudia uchaguzi Republican itapoteza saana maana kuna watu waliwapigia kura ila baadaye wakaregret. Na jinsi ilivyo behave anaharibia Republican kabisa. Ngoja tuone mwisho wa sakata.
 
Ikitokea akafanikiwa Flip Georgia na Michigan, Biden anapoteza 36
 
Ikitokea akafanikiwa Flip Georgia na Michigan, Biden anapoteza 36Bado atabaki na kura 270😀😀😀😀😀

Ikitokea akafanikiwa Flip Georgia na Michigan, Biden anapoteza 36
Georgia wakimaliza kuhesabu Tena Biden atakuwa na jumla ya kura 306. 306 ukitoa kura 36 zitabaki 270. Bado Biden atakuwa Ni mshindi. Trump anaweweseka tu 😀😀😀😀😀😀😀 angekuwa alishindwa kwenye Jimbo moja tungeweza kubeti lakini bahati mbaya jamaa kapigwa vibaya na Ni ngumu kufanikisha kubadilisha matokeo kwa majimbo yote. Marekani siyo Africa waboronge kusimamia Uchaguzi kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom