Trump aapa kulipiza mara '1,000' shambulio la Iran dhidi ya balozi wa Marekani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,865
2020-09-15 (11).png

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kujibu mara "1,000’," kwa shambulio lolote la Iran.

Hii ni baada ya taarifa kwamba Iran ilikuwa inapanga kumuua balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Lana Marks.

"Shambulio lolotela Iran, la muundo wowote, dhidi ya Marekani litakutana na shambulio dhidi ya Iran ambalo litakuwa ni kubwa mara 1,000 !" Bwana Trump alitweet Jumatatu.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Iran Saeed Khatibzadeh amepuuzilia mbali taarifa juu ya mpango wa mauaji ambao kwanza uliripotiwa na Politico.

Iliripoti kuwa Iran ilikuwa inapanga kumuua Balozi wa Marekani, ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa Rais Trump, katika hatua yake ya kujibu mauaji ya Jenerali Qasem Soleimani mwezi januari.

Gen Soleimani aliuawa katika shambulio za ndege za Marekani zisizokuwa na rubani Baghdad mwezi Januari.
 
Kama alishindwa kulipa kisasi baada ya Iran kuvishambulia vituo vyake vya kijeshi na kuharibu vibaya sana vifaa vya mabilion ya dora.
Ndio atakuja kulipiza kwa kuuawa kwa barozi.
Huyu mzee anapenda sana kubwabwaja.
. Huyu jamaa ana mbwembwe ..ni hataree
 
Bush alikuwa haongei ongei hovyo

Mara trump atashambulia north korea ila wapi kiduku anafanya dharau kila uchwao

Wanawake ndio hukimbilia mitandaoni

Putin & Xi ping hivi vidume havina mipasho vitendo tu
North Korea ndio alisema ataishambulia Marekani, Trump alimjibu tu, North Korea iki provoke USA directly Kama ilivyofanya Iran kushambulia ubalozi wa USA kule Iraq halafu USA asijibu hapo ndio tutasema ana mikwara empty
 
Kama alishindwa kulipa kisasi baada ya Iran kuvishambulia vituo vyake vya kijeshi na kuharibu vibaya sana vifaa vya mabilion ya dora.
Ndio atakuja kulipiza kwa kuuawa kwa barozi.
Huyu mzee anapenda sana kubwabwaja.
Kubomoa ule ukuta kwa bomu haikuwa inshu kubwa kwa Marekani, kwanza ilikuwa hasara kwa Iran make gharama ya hilo kombora lililolipua ni kubwa kuliko gharama ya matofali yaliyoangushwa pale. Na kile hakikuwa kisasi cha Soleimani ingawa waajami wa JF mlikuwa mnajitekenya kujifurahisha kwamba Iran amelipa kisasi, wairan wenyewe wanahaha hadi sasa kulipa kisasi lakin bado hawajafanikiwa, na huyo waliyekuwa wanampigia hesabu ndo hivyo tena wameambiwa wakijaribu watakutana kipimo mara 1000 zaidi ya kipimo chao.
 
Haaaaa ya kwamba waliangusha ukuta .
Daah basi umeshinda.
 
Hayo ni maneno tunacho hitaji ni matendo, maana hayo maneno tumeyasikia zaidi ya miaka 40 sasa.
Ila punguza mahaba aisee. Iran nyumbani kunalipuliwa na hajui anayelipua kwa public info zilizopo ndio huyu unayedai kwamba US ajaribu?

Najua huipendi US na unatamani ingekuwa dhaifu ipigwe, ila ndio hivyo kwa sasa ni wababe wa dunia na hakuna utakaloweza kufanya. Iran wanajitahidi kujitutumua ila US kiuhalisia sio ligi yao. Huo ndio uhalisia na ukweli ulivyo!
 
Bush atabaki kuwa Mtu sahihi nayemkubali
Bush walikuwa marais wanajua vita tu wala hawana muda na masuala ya uchumi, haijalishi ni Bush baba au Jr. Kwa rais wa US kuingia vitani si vigumu hata kidogo, silaha si zipo. Ndio maana mnamshangaa kwanini Trump haanzishi vita. Yani mnampima rais kwa kuanzisha vita.

Trump yuko busy na uchumi zaidi na misingi yake. Hayo mavita yalikuwa ya kina Harry S. Truman. Ukitazama ranking za marais wa US Bush hutowaona nafasi za juu ya Clinton wala Obama.
 
Ila punguza mahaba aisee. Iran nyumbani kunalipuliwa na hajui anayelipua kwa public info zilizopo ndio huyu unayedai kwamba US ajaribu?

Najua huipendi US na unatamani ingekuwa dhaifu ipigwe, ila ndio hivyo kwa sasa ni wababe wa dunia na hakuna utakaloweza kufanya. Iran wanajitahidi kujitutumua ila US kiuhalisia sio ligi yao. Huo ndio uhalisia na ukweli ulivyo!
Hata ww unatamani Iran apigwe lakini haitowezekana kwa sababu wanao takiwa kumpiga wanajua uwezo wake na ndio maana wanamgwaya
Mashambulizi ya kimtandao ni kawaida kabisa kwa nchi yeyote ile,na shambulizi la kimtandao halijibiwi kwa shambulio la kijeshi.

Juzi tu hapa marekani ilikuwa inaishutumu Iran ya kwamba imekuwa ikiingilia mifumo ya uchaguzi ya marekani ili kuisaidia Democrat kushinda.

Marekani imeweka vikwazo vya mafuta Iran lakini kila siku Iran inasafirisha mafuta na hakuna anaye thubutu kuya zuia.
Marekani imeweka vikwazo vya silaha dhidi ya Iran zaidi ya miaka 40 lakini bado ndio taifa linalo ogopeka mashariki ya kati.
 
Bush walikuwa marais wanajua vita tu wala hawana muda na masuala ya uchumi, haijalishi ni Bush baba au Jr. Kwa rais wa US kuingia vitani si vigumu hata kidogo, silaha si zipo. Ndio maana mnamshangaa kwanini Trump haanzishi vita. Yani mnampima rais kwa kuanzisha vita.

Trump yuko busy na uchumi zaidi na misingi yake. Hayo mavita yalikuwa ya kina Harry S. Truman. Ukitazama ranking za marais wa US Bush hutowaona nafasi za juu ya Clinton wala Obama.
Kwani mkuu kipindi cha bush Iran haikuwepo?
 
Back
Top Bottom