Trump aamrisha kutolewa siri za kifo cha JF Kennedy

Iyegu

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
6,276
12,397
Rais Donald Trump wa Marekani, ameamrisha idara
ya kitaifa ya kuhifadhi kumbukumbu, kutoa zaidi ya
stakabadhi elfu tatu, yanayohusishwa na mauaji ya
aliyekuwa Rais wa Marekani John F. Kennedy
aliyeuwawa, zaidi ya nusu karne iliyopita.
Rais Kennedy aliuwawa mwaka 1963.
Ikulu ya White imesema kuwa mamia ya faili zilizo
na taarifa nyeti, hazitawekwa hadharani mwezi
Aprili mwakani, baada ya mashirika ya ujasusi, CIA
na FBI kukataa zitolewe.
Rekodi hizo, kwa sasa zimechapishwa kwenye
tovuti ya mtandao wa idara ya kitaifa ya Marekani
inayohifadhi kumbukumbu.
Swali kuwa, muuwaji wa rais Kennedy, Lee Harvey
Oswald, alitenda mauaji hayo kivyake ama alitumwa
na watu au kundi fulani, bado ni fumbo ambalo
halijafumbuliwa hadi sasa, huku vitabu, majarida na
hata filamu zikitolewa kuhusiana na mauaji yake.
chanzo:BBC
 
Back
Top Bottom