True story: Nimeamua kumkataa mtoto rasmi

Hivi wanawake wa Jamiiforums mliobahatika kujiunga humu jf,kutokana na hizi mada mbalimbali zinazoletwa na wanaume kuhusu ushetani wenu,hivi bado mpo mnaofanya ujinga huu?
kwa sababu nyinyi ni malaika eti 😏😏
Hapa huwa tunasikia story za upande mmoja na bila ya kuwa na uhakika Kama ni true story ama laa.
 
Watu wa Jamii Forum Salaam, Naitwa Mfukuza Ndoto, Nina umri wa katikati ya ujana naishi mkoa fulani kanda ya kati. Basi bwana mnamo mwaka fulani nikiwa na 20+yrs nilitokea kumpenda binti fulani toka nyanda za juu kusini, binti huyo alikuwa mwanafunzi wakati huo katika chuo fulani hapa mjini. Namaanisha alikuja tu kwa ajili ya masomo.
Tukapendana, kwa kawaida huwa nikishaingia kwenye mahusiano huwa nadumu na kutulia ndio maana mpak sasa sina rekodi ya mtoto wa mtu niliyempotezea muda halafu nikamuacha, sina machozi ya mwanamke yeyote yanayoniandama zaidi wote hujutia na hicho ndio nilichokipanga kwenye maisha yangu mwanamke akitaka kupendwa atapendwa ashindwe yeye tu sipendi lawama.
Kabla yake nikiwa mwanafunzi miaka ya 2000's nilipoingia tu kidato cha kwanza nikapendwa na kabinti fulani(Na desturi yangu huheshimu sana hisia za mwanamke, yaani siingii kwenye mahusiano bila mwanamke mwenyewe kuonyesha interest na mimi nami nikiridhika nae anapitishwa. Hapa nazungumzia mapenzi sio ngono kwa maana ya tamaa za mwili, nikitamani kuna sehemu zinajulikana na mabaharia hujipoza maisha yanaendelea
Kwahiyo kwenye maisha yangu nimepitia mahusiano yasiyozidi matatu, acha wale wa kushare nao tu shuka, tukiwataja tutajaza kurasa za Jf.
Kwahiyo baada ya kabinti kunipenda hiyo ni pre-form one mpaka tunaanza form one mpaka kidato cha nne tulikuwa wapenzi na shule nzima ilijua hilo lakini cha ajabu hatukuwahi kufanya mapenzi kabisa,
Ilitokea hivyo kwa sababu kuu mbili, kwanza tulikuwa wadogo sana nadhani nilikuwa na miaka 14(kwa mwanaume wakati huo nilikuwa mdogo sana) na yeye alikuwa mdogo zaidi, pili kwa wakati huo mpaka umvue nguo mwanamke ilikuwa shughuli, sio kama sasa katika umri huo kijana anazijua tayari na kama binti tayari anazijua P2.
Kuna wakati nilikuwa naazima mageto ya washkaji tunakutana huko na kabinti basi washkaji wanajua nimemaliza kazi kumbe nimegomewa na mimi ujanja sina sana sababu ya tatu sitaitaja lakini ndio kubwa zaidi
Mimi na yule mwanadada tumekuja kuvunjana 'Upya' tukiwa tumeshamaliza form four tumefeli tuko mtaani, kwa kweli yeye na mimi wote tulikuwa wageni wa mambo kwahiyo tulifunguliana

Nayasema haya ionekane namna gani huwa siachi mwanamke nikishaingia nae kwenye mahusiano mpaka yeye aje kuharibu na ajilaumu mwenyewe na akishaharibu hata aje na Fiat (gari za zamani) huwa sibadili msimamo hata aroge vipi, kwa kuwa naamini ukishafanywa mpumbavu mara moja ukasamehe uwezekano wa kuonekana boya ni mkubwa na atakuumiza mara ya pili na zaidi
Kingine naamini wanawake ni wengi, shida ya nini kurudiana na mmoja aliyekuumiza? Sio kweli ile dhana ya kwamba umeandikiwa utaishi nae kumbuka binadamu wawili wawili kama uliandikiwa kuishi na huyo akizingua kuna aliyefanana tena na huyo huyo utampata, na ili tupeane masomo asijeenda kusumbua wengine unamgomea msamaha akienda kwa mwingine hatasumbua labda awe amepinda tu.

Kilichoniachanisha na huyu bikra mwenzangu nikiwa mtaani nimechoka sasa napigwa na maisha kotekote akanifuata jamaa mmoja, ni wale unakuta pale mjini ana sifa ya ukicheche(umalaya)
Zamani ilikuwa kama sifa, kila mji palikuwa na watu sifa yao ni hakuna demu anapindua kwao, na mara nyingi unakuta ni sababu ya maisha mazuri yake au ya familia yake, akishamudu kuwa na kageto na uwezo wa kubadili mavazi kidogo basi mademu wanapishana. Huyu jamaa akaniuliza kama huyo demu ni demu wangu(nafikiri aliambiwa kwa busara akaona asije kuingia anga zangu) basi mimi ile kujivunga eti nampima imani demu nikakataa ili kama atatongozwa akatae mwenyewe

Bwana wee sijakaa sawa demu ananipigia simu ananitukana kwa namba mpya sielewi sababu nini, huku akiwa na wifi zake(dada wa yule jamaa) kuja kufuatilia jamaa keshamtindua dah nikadata maana home kwetu walimjua mpaka dada zangu walimjua alikuwa anafika mpaka home, miaka zaidi ya minne ilikuwa lazima ajulikane. Na pia alipoanza kutoka na huyo jamaa dada zangu walijua ikawa fedheha sana, nikawaza, nikachanganyikiwa kwa aibu sio kwa sababu siwezi kupata mwingine.
Nikapiga moyo konde nikamove on, Mungu si athumani nikaotea kibarua kidogo, aliposikia akaanza kujirudisha.
Sikumtukana, sikumjibu vibaya nikamwangalia tu nikaachana nae mpaka leo ananiona tu mitandaoni.
Huyo ni mmoja kati ya hao watatu

Sasa tuendelee na huyu binti mwanafunzi wa chuo ngazi ya chini ya shahada...huyu nilikutana naye katika ofisi moja ya serikali ambapo alimsindikiza mwenzake na mimi ambaye mimi nilifahamiana nae, baada ya kusalimiana na kukaa wote kwenye benchi kwa muda mrefu tukisubiri huduma tukazoeana(na huyu binti mlengwa) tukabadilishana namba.
Nilipoondoka yule rafiki yake akanitanabaisha kwamba rafiki yake (Binti Mlengwa tumwite BM) anaonyesha namna fulani ya kunikubali/kunipenda/kunizimikiasasa kama ilivyo desturi yangu huwa sidharau hisia za mwanamke awe amenipenda au ametamani kushare shuka tu na mimi lazima nimtimizie adhma yake.
Note: Haya hayatokei ikiwa nina mwanamke tayari ninayedumu nae, ni pale napokuwa 'Loose ball' na pia isitafsirike kwamba labda nina mvuto saana hapana hii hutokea kwa yeyote maana wanawake wana sababu nyingi za kupenda mwanaume kama ambavyo wanaume tuna sababu nyingi tu za kuvutiwa na mwanamke.

Tuendelee, nilipopata ujumbe ule nikajua cha kufanya hapa ni kuanza ukaribu tu mwanamke akishakupenda hawezi kukuanza lakini ukimsalimi siku ya kwanza, ukamchatisha bize siku mbili weekend inayofuata ukimtaka appointment atakuja tu hata kama atazuga kidogo, Basi, nikaweka mazingira na uhusiano ukaanza kwa namna hiyo

Mwanzo sikukapenda baadae nikakazoea basi nikakapenda, sijui kalinifanya nini nakiri ndio mwanamke nimewahi kumpenda haijatokea tenaaaaa

Visa vichache vilitokea wakati ule vilifaa kabisa kumuacha sikuviona leo hii ndio nayaona na kujiuliza hivi nilikuwa mimi kweli yule? Mfano kuna wakati nilifuma meseji kwenye simu yake ni dhahiri ilikuwa ya mwanaume na ana mahusiano naye nikafunika kombe mwanaharamu apite
Kuna wakati msanii mmoja alikuja kupiga show kwenye ukumbi fulani sikwenda lakini kuna jamaa akaropoka kwamba alimuona usiku huo huyo binti na kutoka chuoni mpaka mjini ni umbali ambao sio wa kurudi usiku, sasa alilala wapi hicho kiulizo kingine, lakini wakati naoambiwa huyo binti alikuwa club mimi nimeonge nae sana usiku mpaka kwenye saa tano au sita kwa akili yangu ndogo wakati ule sikumuamini jamaa nikafikiri nimemfananisha....maisha yakaendelea

Nilikapenda sana kale kabinti, kuna wakati nilitishia kukaacha kakalia usiku kucha, nikajisemea mwanamke si ndo huyu bwanaaa...nikadumu nae kwa miaka mitatu mpaka anamaliza, kilichonipa imani kwamba mke nimepata ni wakati alipomaliza shule, wanavyuo wengi wakimaliza na mapenzi wanaondoka nayo makwao lakini huyu BM aliendelea "ku-keep in touch" mpaka nikaanza kunenepa, huko huko aliko bado mawasiliano yalikuwa mazuri huku akija kunipikia kila alipopata nafasi
Hata wenzangu waliokuwa na wanawake pale chuoni ambao walishaachana na wapenzi wao waliamini nimependwa haswaaa na mimi ukinipenda nakupenda nataka nini kingine.

Ndio ikawa hivyo, akamaliza akaondoka, akaanza kudai ndoa, basi mi ndo kabisaa naona nimepata mke mwema, nikachukua likizo nikampeleka nyumbani kumtambulisha, kwanza nikaanza kwao kisha kwetu.
Nyumbani kwetu walimpenda sana, she was hard working na mrembo kiasi, tukiwa hapo nyumbani nafasi za ajira zikatoka akaajiriwa mkoa fulani kanda ya magharibi
Wakati nampeleka nyumbani ilikuwa mnamo August ya mwaka huo, kufika December ndio picha picha zilipoanza...


.....Wacha nichukue mapumziko....leo ndio nimeona ugumu wa kuandika...wale wazee wa itaendelea hawafanyi kwa makusudi inawalazimu kupumzika

Will Be Back!!!
Nasubiri
 
Ushauri wangu ni bora upime DNA ili kuondoa huo walakini wa anaweza kuwa wangu au asiwe wangu,mda wote ulopoteza na gharama zote ungeshapima DNA kitambo naona wakati mwingine unakosa maamuzi ya kiume kwa sababu ya ule walakini sasa kwa nini usifanye jambo moja kumaliza utata huo
Kama ukifata ushauri wangu
★Ukishapima DNA★
Majibu negative:sasa unaweza kukata mawasiliano rasmi na hyo maza msijuane kwa lolote
Majibu positive: Anza kuplay part yako kama unavoweza na sio kuendeshwa endeshwa,malezi ya mtoto yawe kama unavoona inafaa ikiwa mama yake anachofanya siyo sahihi

Kuhusu cheti
Haina haja ya kuendelea kutumia cheti cha ndoa ikiwa ndoa hyo haipo,chukua hatua,japo unadai limbwata limeisha lakini inaonekana bado huyo bibie kakukalia kichwani(anakudrive mno)
 
Angeendelea kunidrive nisingefikia maamuzi haya, tunza huu uzi halafu uje kuniuliza miaka ijayo kama nitajihusisha nae tena

Unasema nipime DNA, inamaana unataa nimpigie simu mwanamke yule tena? Nimeshajirudi rudi kumpigia sana yeye hanaga shida na mimi
Haiwezekani mwanamke akaushe tu kirahisi kama mtoto ni wako na wazazi hamjawahi kukorofishana na zaidi yeye ndio alikorofisha

Kama masuala ya DNA ilikuwa wakati uliopita kwa sasa haijalishi ni wangu au sio wangu sitamuanza tena, sitajishughulisha tena labda aanze kunitafuta

Nimekaa nikafikiria sana kabla ya maamuzi haya, sioni ni kipi nitakosa kama nitaachana na hili suala
Mtoto sio wako .. mind your own business my nigga .. Huyo mwanamke amekuchoresha Sana .amekuvunjia heshima yako pakubwa Sana haupaswi kumpa nafasi hata yakuipata salamu yako ..mfungie vioo mazima jifinze kulinda brand name yako mkuu ' kina watu wengine au vitu vingine haupaswi kabisa kuvikaribisha maishani kwako
 
Ushauri wangu ni bora upime DNA ili kuondoa huo walakini wa anaweza kuwa wangu au asiwe wangu,mda wote ulopoteza na gharama zote ungeshapima DNA kitambo naona wakati mwingine unakosa maamuzi ya kiume kwa sababu ya ule walakini sasa kwa nini usifanye jambo moja kumaliza utata huo
Kama ukifata ushauri wangu
★Ukishapima DNA★
Majibu negative:sasa unaweza kukata mawasiliano rasmi na hyo maza msijuane kwa lolote
Majibu positive: Anza kuplay part yako kama unavoweza na sio kuendeshwa endeshwa,malezi ya mtoto yawe kama unavoona inafaa ikiwa mama yake anachofanya siyo sahihi

Kuhusu cheti
Haina haja ya kuendelea kutumia cheti cha ndoa ikiwa ndoa hyo haipo,chukua hatua,japo unadai limbwata limeisha lakini inaonekana bado huyo bibie kakukalia kichwani(anakudrive mno)
Naunga mkono hoja, mara nyingi sisi wanaume huwa tunakosa maamuzi halafu tunasingizia limbwata. Mtoa mada tangu aliposhtukia kuhusu mimba ya kwanza ilipotolewa angechukua hatua ngumu haya yote yasingetokea
 
hata nikikuta msg ya mapenzi nalia Mimi badala yake' ...Daahh dunia hii !!!!
Mpaka sasa sielewi nilikua katika hali gani, wadau watakuwa sahihi kama wataniita majina yoyote tu

Maana yale sio mapenzi ni kitu kingine tu
 
Mtoto sio wako .. mind your own business my nigga .. Huyo mwanamke amekuchoresha Sana .amekuvunjia heshima yako pakubwa Sana haupaswi kumpa nafasi hata yakuipata salamu yako ..mfungie vioo mazima jifinze kulinda brand name yako mkuu ' kina watu wengine au vitu vingine haupaswi kabisa kuvikaribisha maishani kwako
Nakubali
 
Naunga mkono hoja, mara nyingi sisi wanaume huwa tunakosa maamuzi halafu tunasingizia limbwata. Mtoa mada tangu aliposhtukia kuhusu mimba ya kwanza ilipotolewa angechukua hatua ngumu haya yote yasingetokea
Hili la limbwata sikutaka kulizungumzia tangu mwanzo kwa kuhofia kuambiwa kama ulivyosema ndio maana hata nilipojaribu kulielezea nimetaka wafuatiliaji wasilitilie maanani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom