True story: mkasa wa ukweli ulionitokea katika pilikapilika za kutafuta maisha

Pole sana...

Ulimpa adhabu kali na mbaya sana...

Hakuna adhabu mbaya kama mtu kutenda kosa ukamshika alafu ukaamua kukaa kimya kama hakuna kilichotokea, lazima aweweseke kwa kuhisi unamuandalia tukio, kumbe wewe wallah...
 
Duuh huo ujinga mimi ningekodi mwana ndie ambebe demu na maagizo ya kumdondosha na jidume nalibeba nalipitisha kwa vibaka nalitupa mtaroni pora simu hadi madole
 
"Baada ya kumaliza chuo nilianza kupambana na maisha mtaani, kiukweli nilipitia maisha na nyakati ngumu sanaa.

Kuna rafiki yangu mmoja yeye ni dereva boda boda akawa ananipa boda boda yake jioni kuanzia saa 10 mpaka saa 4 au 5 usiku kama daywaka maana yeye alikuwa anakesha.

Siku moja mida ya jioni nilikutana na abiria mmoja akaniomba nimpeleke sehemu ilikuwa ni nyumba ya wageni (guest house).

Basi bhana nikamfikisha eneo husika akaniomba pia baadae nimrudishe kwake, akachukua namba zangu na kweli baadae mida ya tano kasoro kani-call na mimi nikaenda mpaka pale guest lakini akanambia kwanza mpeleke mgeni wangu kabla kwao hawajaanza kuleta noma.

Cha kushangaza aliyekuwa katoka mle ndani alikuwa ni DEMU wangu (girlfriend wangu). Aiseee niliishiwa nguvu na kwakuwa ilikuwa usiku hakunijua na hakutegemea kama ningekuwa pale hivyo alivyosogea alipigwa na butwaa mpaka hata yule jamaa akastuka lakini nikapiga moyo konde nikamwambia panda boda tusepe.

Kweli nikampeleka mpaka kwao na sikumsemesha wala kumuuliza chochote, nikawasha chombo nikarudi nikambeba na jamaa vile vile nikamrudisha kwake. Nikachukua hela yangu fresh.

Siku zikapita na mimi nikauchuna hakuna kumuuliza kitu wala nini kuhusu tukio lile, hata kila alipojitahidi kunichokonoa angalau nimuulize lakini nilichagua kukaa kimya na simtafuti wala nini, lakini akinitafuta naongea naye fresh tu kama hakuna jambo moyoni mwangu ila akiniuliza nasingizia sina SMS au salio la kumpigia.

Kumbe tukio lile lilikuwa linautesa sana moyo wake hasa alikuwa na shauku ya kutaka kujua nawaza nini kichwani mwangu kuhusu yeye, alikuwa anawaza nina mipango gani yeye? mbona simuulizi kitu?.

Baadae walishauriana na rafiki yake wakaenda kutoa report police kuwa natishia kumfanya kitu kibaya, na huyo rafiki yake akawa ndio kama shahidi. Nilivyoitwa police nikawaeleza tu hali halisi, police walicheka sana ila tu wakamshauri kuwa akae mbali na mimi.

Kuanzia hapo mpaka leo hajanitafuta na mimi tangu siku ya tukio lile, nilifuta namba yake kabisa.

Kuanzia pale nikaanza kuona ile kazi imekuwa ni changamoto kwangu sikuendelea nayo tenaaa".
Ulifanya kama yule jamaa wa kimara aliyemfunia mkewe na rafiki yake kipenzi kitandani halafu wote hakuwauliza mpaka wakajistaki
 
Mkuu unajuaje kama yeye ndio aliipost Facebook?
Sio yeye nae kacopy tu ila kaamua kuhadaa wanaume hapa hii stori ni ya mda sana huko niliiona pia na Leo nimeiona kama alikuwa yy kwann hakuileta hapa jukwaani tangu zamani na kama mnavyojua JF ndio huibua stori kisha kwenda mitandaoni maana FB most of users are anonymous so there comfortable to express something than FB were most of people have real user name na post ilikuwa kwenye page flan ivi ambayo ni ya story kama hizi,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom