True Memories Of My Life [Kumbukumbu za Kweli za Maisha Ya Shigongo]

Nyamuleha jr

Senior Member
Feb 20, 2013
185
65
Bonge la story bonge la motivation and insiparation, walio isoma hii hadithi watakubaliana na mimi. Ni mtu aliyetoka maisha ya chini sana familia masikini sana, mambo ya vibarua vya kulima, kuuza sigara mtaani, hadi sasa kufikia level ya kuheshimika katika jamii na kuwa millionaire.

Kama bado hujaisoma itafute. Lazima itakufanya usongeee mbele zaidi.
 
bonge la story bonge la motivation and insiparation, walio isoma hii hadithi watakubaliana na mimi. Ni mtu aliyetoka maisha ya chini sana familia masikini sana, mambo ya vibarua vya kulima, kuuza sigara mtaani, hadi sasa kufikia level ya kuheshimika katika jamii na kuwa millionaire. Kama bado hujaisoma itafute. Lazima itakufanya usongeee mbele zaidi.

Eti nini?..Una akili kweli wewe?
 
Heheeee.. Inamaana zile tuhuma zilizo vuma Jf haziko kwenye memory yake?? Maana haziongelei kabisaaaa....
Cc warumi
 
Last edited by a moderator:
Nimekuja mbio mbio kumbe memories zenyewe zimeishia kwenye heading tu. Mxuuu!
 
Heheeee.. Inamaana zile tuhuma zilizo vuma Jf haziko kwenye memory yake?? Maana haziongelei kabisaaaa....
Cc warumi

Mtumishi wa mungu shigongo aka Mume wa MOO msagagaji, eeh shigongo mtumish uliyetukuka
 
Last edited by a moderator:
Duh Shigongo ushaharibu sana akili za ma-house girl wetu kwa hadithi na habari zako imetosha hukohuko kwenye tabloids zako,huku JF tuache basi naona unajipenyeza kwa kasi.
 
bonge la story bonge la motivation and insiparation, walio isoma hii hadithi watakubaliana na mimi. Ni mtu aliyetoka maisha ya chini sana familia masikini sana, mambo ya vibarua vya kulima, kuuza sigara mtaani, hadi sasa kufikia level ya kuheshimika katika jamii na kuwa millionaire. Kama bado hujaisoma itafute. Lazima itakufanya usongeee mbele zaidi.

Memories of my life
[Kumbukumbu za maisha
yangu]
by GLOBAL
Oct 22, 2012
SITAKI kuyafanya maisha yangu siri,
nataka watu wote wanifahamu, ndiyo
maana nimeamua kuanzisha ukurasa
huu ili kuelezea yale ninayoyakumbuka
maishani mwangu, tangu nilipozaliwa
mpaka siku nitakapokoma kuandika.
Ninaamini yatakuwepo mengi ya
kujifunza, kutia moyo na pengine
kuonya mtu mwingine asiyafanye kwani
nimefanya makosa mengi sana maishani
mwangu, mengine ni ya aibu lakini
nitayasema hadharani na ninapotakiwa
kuomba msamaha nitafanya hivyo.
Nawakaribisheni kwenye kumbukumbu
zangu za maisha ambazo nimezitunza
kwa muda mrefu, kwa lengo la kuandika
kitabu. Najua yatakuwepo ya
kuchekesha, kutoa machozi na kuinua
mioyo ya waliokata tamaa. Hivyo usikose
kusoma kumbukumbu hizi kila siku ya
Jumatatu kwenye Ijumaa Wikienda.
“Nina miaka mitano, ni asubuhi ya siku
na mwezi nisioukumbuka, mwaka 1976.
Kuna ukungu kila mahali, umande
umetapakaa kwenye nyasi. Baba yangu
amenishika mkono, ananipeleka Kijiji cha
Ishigwandama kilichokuwa kama
kilometa mbili kutoka kijijini kwetu
Mwangika.
Ingawa natetemeka kwa baridi kali na
meno yakigongana, kwani sina sweta
mwilini mwangu na manyunyu ya mvua
yanadondoka, bado moyo wangu una
furaha kwa sababu ni siku ya kwanza
napelekwa shuleni kuanza darasa la
kwanza kwenye Shule ya TAPA, sielewi
maana ya neno hili, lakini ndivyo
ninavyosikia linatamkwa.
Tunatembea kidogo, nachoka, baba
anaamua kunibeba begani. Ni mzee
masikini ambaye hakusoma hata darasa
moja lakini anapenda elimu na anaamini
ndiyo itakayowasaidia watoto wake
maishani.
“Ng’wanone, yaya eligusha, ukasome
getegete! Uligwa?”
(Mwanangu, usiendekeze michezo
shuleni, usome kabisa, unasikia?)
anasema baba yangu kwa lugha ya
Kisukuma tukiwa tumekaribia kufika
shuleni.
“Nali…gwa!” (Nasi…kia) naitikia huku
meno yakigongana.
Shuleni ananishusha mabegani kwake
na kuanza kutembea, kinachoonekana
mbele yangu ni majengo
madogomadogo ya nyasi, ni kama
mabanda ya kuku, nje kuna watoto
wengi, wote wakiwa hawana viatu kama
nilivyo mimi baadhi hawana hata
mashati, pamoja na baridi hiyo wapo
vifua wazi. Wamepauka kama vile
hawakuoga jana yake huku wengine
wakiwa na vipande vya vyakula
mikononi, nilipoangalia vizuri
nikagundua ni viporo vya ugali.
Namwona mtoto mmoja jirani yetu,
ambaye huwa nacheza naye siku zote,
najichomoa kwenye mkono wa baba na
kumkimbilia. Tunasimama pamoja
tukiwa na furaha, ni siku ya kwanza
shuleni. Huyu anaitwa Joki (hivi sasa ni
marehemu, alifariki miaka michache
iliyopita), haukupita muda mrefu sana
akaja mtoto mwingine, pia namfahamu
anaitwa Malila (huyu yupo kijijini mpaka
leo, ni rafiki yangu mkubwa).
Muda mfupi baadaye mwalimu
anajitokeza, simkumbuki jina na
tunamsalimia kwa Kisukuma lakini
anakataa na kututaka tuseme:
“Shikamoo Mwalimu.” Ni neno geni
kwangu kwani sijazoea kulitumia
nyumbani. Kwangu ni kama neno la
Kichina, nalazimika kulizoea kwani ndilo
litakalokuwa likitumika shuleni kila siku.
Furaha niliyonayo moyoni haina kipimo
kwani nilitamani sana kusoma na siku
zote nilipowaona watoto wakipita
nyumbani kwetu wakielekea shuleni
moyo uliniuma, hakika siku hii ya leo
niliisubiri kwa muda mrefu.
“Sasa tutawapima, waliotimiza umri tu
ndiyo watakaoanza shule!” Ilikuwa ni
sauti ya mwalimu baada ya salamu,
moyo wangu ukashtuka kugundua
kuwa kumbe kuna watu wasingeanza
darasa la kwanza sababu ya umri wao.
Wote tukapangwa kwenye mstari mrefu
na mwalimu akawa anapita na
kumwambia mwanafunzi mmoja mmoja
anyanyue mkono wake wa kuume na
kuupitisha juu ya kichwa na kugusa
sikio la upande wa kushoto, waliogusa
waliwekwa upande mmoja na ambao
hawakugusa waliwekwa upande wa pili.
“Wewe mtoto wa James, acha ujanja
weka mkono wako vizuri, weka katikati
ya kichwa, usiweke kichogoni!”
mwalimu alisema kwani mkono wangu
ulikuwa haugusi sikio, ili kulifikia ilibidi
niusogeze kwa nyuma ndipo
nikafanikiwa kuligusa.
Nikajaribu weeee, lakini sikuweza, bila
huruma mwalimu akanisukumizia
upande wa watu ambao walishindwa
kugusa sikio.
“Hawa warudi nyumbani mpaka mwaka
kesho, wakue kidogo.”
Haikuwa shule tena, iligeuka kuwa
hospitali au kliniki kwani mimi ndiye
niliyeongoza vilio vya wanafunzi wote
waliokataliwa kuingia darasa la kwanza,
nikagalagala chini huku nikimwita baba
ambaye alifika na kuninyanyua. Akaanza
kunibembeleza ninyamaze huku
akiniambia nivumilie tu mwaka kesho si
mbali, sikukubali niliendelea kulia kwa
nguvu nikiamini mwalimu angebadilisha
mawazo lakini haikusaidia, wenzangu
wakaingia darasani nami nikabebwa na
baba begani na kuanza kurejea
nyumbani, njia nzima nililia mpaka
nilipofika nyumbani macho mekundu na
yakiwa yamevimba na sauti imepotea,
inawezekana kabisa nilikuwa na deko.
“Nyamaza mwanangu utasoma tu!”
ilikuwa ni sauti ya mama yangu.
“Labda jaribu wewe, mimi nimeshindwa,
mtoto hasikii!” baba aliitikia.
Kubembelezwa na mama
kulininyamazisha, nikaendelea na
mchezo, kumbukumbu ilinirejea
nilipowaona baadaye Joki na Malila
wakirejea kutoka shuleni, roho iliniuma
mno lakini nikajipa moyo na kuamini
mwaka kesho na mimi ningeanza shule
ingawa wao wangekuwa tayari darasa
la pili.
***
Mwaka huohuo 1976, nikawa
nimeshasahau habari za shule, mama
yangu alileta mtoto mwingine nyumbani,
mdogo, mzuri, anafanana na padri Paulo
(huyo alikuwa ni Padri Mzungu wa
Parokiani kwetu Mwangika)
“Mama mtoto umemtoa wapi?”
Itaendelea
 
Memories of my life
[Kumbukumbu za maisha
yangu] - 2
by GLOBAL
Oct 29, 2012
ILIPOISHIA:
Mwaka huohuo 1976, nikawa
nimeshasahau habari za shule, mama
yangu alileta mtoto mwingine nyumbani,
mdogo, mzuri, anafanana na Padri Paulo
(huyo alikuwa Padri Mzungu wa
Parokiani kwetu Mwangika).
“Mama mtoto umemtoa wapi?”
SASA ENDELEA…
“Nimemnunua dukani,” ndiyo jibu
nililopewa, nadhani hivi ndivyo watoto
wengi walivyojibiwa siku hizo na wote
tuliamini kwamba watoto walinunuliwa
dukani mpaka tulipogundua baadaye
kwamba jambo hilo halikuwepo.
Mtoto huyo alikuwa ni dada yangu Lydia
ambaye hivi sasa ni mfanyabishara,
ameolewa na anaishi kwa kufanya
shughuli zake jijini Dar es Salaam. Mtoto
akaendelea kukua, nami nikasahau
mambo ya shule. Baba yangu naye
aliendelea na biashara yake ya duka, kila
alipokwenda Mwanza kununua bidhaa
zake ilikuwa ni lazima atuletee mkate wa
boflo na jioni anipe soda ya Fanta
ninywe, hiyo ndiyo iliyoleta ugomvi kati
yangu mimi na mdogo wangu Masha.
“Mimi ya kwenye chupa!”
“Mimi ya kwenye chupa!”
Ulikuwa ugomvi mkubwa, mwisho baba
alitoa uamuzi wa kumpa mdogo ya
kwenye chupa nami nikanywa kwenye
kikombe. Hapakuwa na jinsi, mdogo
ilikuwa ni lazima apendelewe, huyu
Masha ninayemwongelea hapa ndiye
mdogo wangu, Mkurugenzi wa Kampuni
ya Kihelya Auto Tractors ya jijini Dar es
Salaam na pia mkurugenzi mwenzangu
wa Kampuni ya Global Publishers Ltd na
kampuni nyingine kadhaa tulizonazo.
Katika hali ambayo sikuitarajia, kabla ya
mwaka 1977 haujaingia, baba yangu
alifikia uamuzi mkubwa wa kuhama
kijijini kwetu kwenda Shinyanga Vijijini
kwenye kijiji kiitwacho Kakola, jirani
kabisa na alikoishi mjomba wetu. Kwa
umri wangu ulikuwa mdogo sikuwa na
uwezo wa kuhoji, zaidi ya kupewa
taarifa tu na kujiandaa kuondoka.
Moyo wangu ulikuwa hautaki kuwaacha
akina Joki na Malila lakini ilishaamriwa
na wazazi, hivyo sikuwa na jinsi sote
tukapakiwa kwenye trekta na mizigo
yote ikiwa ni pamoja na mali za dukani.
Ninachokumbuka kabla ya uamuzi huo,
baba yangu alikuwa amesafiri kwenda
Shinyanga, kumbe huko ndiko alikwenda
kutafuta makazi mapya na kuirudia
familia yake.
Niliondoka Mwangika nikilia, safari yetu
ilikuwa ni ya usiku, sikumbuki tulikopitia
lakini siku iliyofuata mchana niliamshwa
usingizini, tulikuwa tumefika Kakola,
kwenye jumba kubwa ambalo mbele
yake kulikuwa na miti mikubwa ya
michongoma! Palikuwa ni kwenye kimji
kidogo, chenye nyumba nyingi za bati,
baba alikuwa amepanga nyumba ya
mzee mmoja aliyeitwa Luhemeja.
Mizigo ikaanza kushushwa na kuingizwa
ndani, nilikuwa kwenye makao mapya,
watoto wengi walikuwa wakishangaa,
Kiswahili kiliongewa kuliko kule
nilikotokea, hii ilionesha hapo Kakola
kulikuwa na ustaarabu kidogo na
wajanja walikuwepo.
Mizigo ilipoishia ndani nasi tuliingia,
vitanda vya springi vikaanza kuingizwa
vyumbani, hapo ndipo pangekuwa
makao yetu mapya. Kumbukumbu zangu
bado zilikuwa kwa akina Joki na Malila.
Chakula cha mchana kikapikwa, Mungu
wangu, ulikuwa ni ugali na mlenda!
Mboga inayovutika kama gundi, ni lazima
ujue namna ya kuukata utepe wake
wakati wa kula. Sikuzoea mboga za
majani, nilikotokea Kahunda ni nchi ya
samaki kwani kuna ziwa, huku
Shinyanga hakuna ziwa, kitoweo chao
kikubwa ni mboga za majani.
Niliambiwa kule tutakuwa tukila mboga
zenye majina mengi kama, Bunami,
Moga, Nsasa, Lyashili na nyingine nyingi
ambazo ulimi wangu haukukubaliana
nazo kabisa baada ya kula.
Nikabandikwa jina jipya la Nzoka yagili
ikubi, yaani nikawa naitwa jina hilo
lililomaanisha nyoka hali majani. Mpaka
leo, mboga za majani na mimi ni usiku
na mchana, nadhani ndiyo sababu
kubwa sana ya macho yangu kutokuona
vizuri.
Maisha yalikuwa magumu Shinyanga
sijapata kuona. Biashara ilimwendea
baba vibaya mno, nilikonda kwa sababu
ya kushindwa kula chakula cha huko.
Hali ilikuwa mbaya, hata hivyo
niliandikishwa Shule ya Msingi Gembe
kuanza darasa la kwanza, mimi na dada
yangu Joyce tulisoma darasa moja.
Tulifundishwa na mwalimu aitwaye
Marwa, mzee wa Kikurya ambaye hivi
sasa sijui alipo na sina uhakika kama yu
hai au marehemu.
Katika nyumba tuliyoishi, nakumbuka
kulikuwa na mtoto wa kike wa mpangaji
mwenzetu aitwaye Rebeka, mimi na yeye
tulikuwa rika moja. Huyo ndiye
tuliyecheza naye mchezo wa
kujipikilisha, mimi baba yeye mama.
Ingawa nilikuwa mdogo, sijui uzuri wa
msichana kwa wakati huo, kwani
nilikuwa sijawahi kabisa kukutana na
msichana kimwili na nilikuwa sijui
maana yake ni nini, lazima nikiri kwamba
Rebeka alikuwa mzuri.
Pamoja na umri mdogo, Rebeka alikuwa
mjanja kuliko mimi, kwani mimi kama
baba nilipotoka shambani nilimwambia
anitengee chakula, baada ya kula
tuliingia chumbani kulala, mchezo wetu
wa baba na mama tuliufanyia jirani na
nyumba ya kuku, hivyo wakati wa kulala
tuliingia kwenye nyumba hiyo na
kutandika mkeka, bila kujali utitiri
mwingi uliokuwa ukitambaa kwenye
miili yetu.
Rebeka alianza kunipapasa na
kunifanyia vitu ambayo sijui aliviona
wapi kwa umri wake, huku akivuta
pumzi ndani ya mdomo wake kama vile
ambavyo mtu hufanya akila muwa. Sitaki
kusema uongo, katika umri wa miaka
kumi nilikuwa sijui chochote kuhusu
mapenzi.
Akaja juu yangu lakini kabla hajafanya
lolote nikasikia sauti ikisema
“Pumbavuuuu, yaone! Mnafanya nini?”
ilikuwa ni sauti ya mama yangu, huku
akipiga kelele kwa hasira, iliyomfanya
mama Rebeka naye asogee karibu
pamoja na majirani wengine.
Ilikuwa ni aibu, tukachomolewa kwenye
nyumba ya kuku, kuvuliwa nguo zote na
kuanza kutandikwa tena kwa katani
iliyochanwachanwa huku mwili wote
ukiwasha. Sikumbuki kama nimewahi
kuadhibiwa namna hiyo tena maishani
mwangu, tangu siku hiyo mimi na
Rebeka tukawa tunaonana kama paka
na panya. Hata mchezo wa kujipikilisha
na kuitana baba na mama ukapigwa
stop.
Itaendelea
 
Memories of my life
[Kumbukumbu za maisha
yangu] - 3
by GLOBAL
Nov 5, 2012
WIKI iliyopita nilieleza kwa kirefu maisha
tuliyoishi kijijini Kakola, Shinyanga baada
ya kuhama kutoka Mwanza. Nilieleza jinsi
nilivyobaini tofauti kubwa ya maisha kati
ya Mwanza tulipokuwa tukiishi awali na
Shinyanga, kuanzia vyakula, mtindo wa
maisha, biashara mpaka michezo ya
watoto.
Leo naendelea kueleza kilichofuatia
baada ya maisha ya familia yetu kuanza
kuyumba, biashara ya baba ikiwa
inalegalega.
SONGA NAYO...
SIWEZI kuikumbuka siku wala saa,
ninachoweza kukikumbuka ni kwamba.
ilikuwa ni mchana, tukirejea kutoka
shule, tena ilikuwa siku ya mawingu
sana, dalili za mvua zikionekana.
Walinishawishi niwasubiri, mpaka
tukawa watu wa mwisho kutoka shule,
tena tukitembea taratibu.
Kwenye bwawa kubwa lililokuwepo
kando ya barabara, walikatisha kuelekea
kwenye vichaka wakitaka niwafuate.
Kichwani nikiwa sina hili wala lile,
nilifanya hivyo mpaka nikajikuta katikati
ya vichaka, wakanikamata kwa nguvu na
kuniangusha chini sababu walikuwa
watatu na kuanza kufungua vifungo vya
kaptura yangu wakiwa na lengo la
kutaka nifanye nao mapenzi kwa nguvu.
Kwa maneno niliyokuwa nimeambiwa
na mama yangu, juu ya magonjwa ya
zinaa yaitwayo Kisonono, Kaswende na
Kabambalu (wakati huo hapakuwa na
Ukimwi) yaliyotisha sana, sikuwa tayari,
meno yakatumika, niliwang’ata mpaka
wakaniachia na nikakimbia huku
nikifunga kaptura yangu mpaka
nyumbani. Sikumsimulia mtu yeyote juu
ya kilichotokea, ilibaki siri yangu.
Huo ndiyo ukawa mwisho wa urafiki kati
yangu na wasichana hao na msimamo
wangu juu ya mabinti ulibaki huohuo
kwa muda mrefu, yote hiyo ikiwa ni kwa
sababu ya mafunzo ya dini niliyoyapata
kwenye madhehebu ya Sabato ambako
mimi na familia yangu tuliabudu.
Dada yangu Leah ambaye hivi sasa ni
mwalimu huko Bagamoyo, ndiye
aliyetuingiza kwenye madhehebu hayo
baada ya kuhubiriwa na Wainjilisti wake.
Ni madhehebu yaliyofundisha sana juu
ya Neno la Mungu, nakumbuka uwezo
wa kukariri mafungu ya Biblia niliokuwa
nao.
Ni uwezo huu ndiyo ulionifanya nikiwa
na umri mdogo kabisa nihamishwe
kwenye madarasa ya vijana na
kupelekwa kwenye makundi ya
kujifunza lesoni (hiki ni kitabu ambacho
hutumiwa na Wasabato kujifunza Neno
la Mungu kikiwa na kalenda ya mwaka
mzima).
Hali ya maisha iliendelea kuwa mbaya,
biashara ya baba iliendelea kuporomoka,
duka likaendelea kubaki ngazi tupu.
Nilimwona kabisa alivyokuwa
akichanganyikiwa, mwisho alisafiri
kwenda Mwanza na kubaki huko kwa
muda mrefu, taarifa za chinichini
ambazo nilianza kuzisikia kutoka kwa
ndugu zangu zikaeleza kuwa
tungehamia Mwanza ambako baba
alikuwa amekwenda kujenga nyumba.
Furaha ya kuhamia Mwanza ilinijaa,
mjini? Ambako siku zote niliwaza kufika
na kuona magari na maghorofa? Hakika
ilikuwa ni furaha ya ajabu. Kuna wakati
usiku nilikuwa silali nikifikiria siku baba
atakaporudi na mimi kupanda basi
pamoja na ndugu zangu kwenda
Mwanza ambako nilijua tabu zote
zingekwisha maana nilishasikia maisha
ya mjini yalikuwa safi, kazi kidogo tu mtu
anapata fedha, hivyo baba yangu
angekuwa na fedha nyingi mno tukiwa
mjini na tusingeteseka tena.
Baada ya kama mwezi mmoja, baba
alirejea, furaha ikaitawala nyumba yetu
hasa baada ya kutangaza kwamba
tungehamia Mwanza siku chache
zilizofuata. Kama kuna kipindi katika
maisha dakika moja huwa mwaka
mzima, basi kilikuwa ni hicho cha
kusubiri iwadie siku ya kuondoka kijijini
Kakola kwenda ‘dauni tauni’ Mwanza.
Huo ulikuwa ni mwaka 1979, Tanzania
ikiwa katikati ya vita na Nduli Iddi Amini,
maana shuleni tulifundishwa kuimba
nyimbo za Joka Iddi Amini Dadaa, kama
nyimbo zile zingekuwa zinaua, Iddi
Amini angekufa kipindi hicho, zilikuwa
mbaya! Mbaya! Zilizojaa maneno ya
dharau na kejeli na matusi dhidi ya Iddi
Amini na watoto wote waliziimba na
kumchukia mtu huyo kupita kiasi.
Hatimaye siku ilifika, tukapanda ndani ya
basi la Umoja, ulikuwa ni usiku wa
manane, magodoro, vitanda vya springi,
kabati za mninga, mitungi ya maji ya
kunywa na vyungu vya kupikia
vikapakiwa juu ya basi. Mzee huyu jasiri,
ambaye hivi sasa namwita marehemu,
alikuwa ameamua kupakia watoto wake
wote kumi, mmoja wao akiwa mchanga
(Violeth) ambaye hivi sasa ni mmiliki wa
meli ya MV Juliana iliyoko mjini Mwanza,
kwenda mjini kutafuta maisha.
Huu ni moyo mgumu wa ajabu ambao
wanadamu wachache sana wanao,
lazima nikiri wazi kwamba hii ndiyo
sababu kubwa namlilia sana mzee
wangu, bila uamuzi wake wa kuhamia
mjini, bila shaka hata mimi ningekuwa
mlevi wa gongo kama vijana wengine
wengi niliowaacha kijijini wakati ule na
hakuna Mtanzania hata mmoja angekuja
kusoma maandishi yangu. VIVA JAMES
BUKUMBI, Mungu ailaze roho yako mahali
pema peponi, kila kitu nilichonacho
maishani mwangu ni kwa sababu yako.
Safari ilikuwa ndefu, kwenye barabara
mbovu yenye mabonde mengi na
madaraja yaliyoharibika. Wasukuma
kama kawaida yao walikuwa
wakitaniana usiku mzima tena
wakitamka maneno mabaya ambayo
nyumbani kwetu nilikuwa sijawahi
kuyasikia na siwezi kuyaandika hapa.
Hakuna aliyekuwa na uwezo wa
kuwanyamazisha wala hawakujali
kwamba mimi nilikuwa na wazazi
wangu humo ndani.
Hatimaye baada ya saa nyingi tukaingia
mjini Mwanza, mizigo yetu ikashushwa
na baba akakodisha gari dogo
tukabebwa hadi sehemu iitwayo
Nyakato Mecco huko ndiko baba
alikokuwa amejenga. Tulipofika kwenye
nyumba aliyojenga nilifikiri labda
hatujafika tunakokwenda, kijumba
kilikuwa kidogo mno, tena cha tope,
ambacho kilijengwa katika eneo lenye
unyevunyevu na chemchem nyingi za
maji na vyura walilia kila mahali.
Itaendelea wiki ijayo
 
upuuzi mwingine kutoka kwa shigongo. hivi mbona vigazeti vyake uchwara huwa haviandiki baba yake afufuka ameonekana tabata?
 
Back
Top Bottom