Trucks and truckers special thread. Uzi maalum kwa wadau wa magari ya mizigo na wasafirishaji

Je kwa sisi tunaotaka kuanza hii biashara aina ipi ya gari inayotufaa
Zipi trucks aina mbalimbali kama Volvo,scania,Mercedes-Benz,Dad c.f.,Dad Xf,Man diesel na mengine ila kwetu Tanzania Scania ndio truck inayoongoza hasa ukizingatia upatikanaji wa vipuri na matunda makenika wengi wanafikiria sana,ila kama unaanza usikimbilie trucks za G Au R series Euro 5,yavuta truck ya Euro 2-3 ndio utapasua kichwa sana
 
Nasikia Safari ya Lubumbashi via Kasumbalesa huchukua zaidi ya miezi miwili na malipo yake ni laki sita
Dar Lubumbashi ikizidi sana ni siku 10 iwapo hakuna Mambo yatakayo kukwamisha jinsi uwezo safarini,kinachofanya watu kukaa sana Congo ni matajiri kutokupenda kulirudishia gari bila mzigo,ndio unajikuta nimeshashusha mzigo,unasubiria wa kurudi nao Tanzania
 
N
Zipi trucks aina mbalimbali kama Volvo,scania,Mercedes-Benz,Dad c.f.,Dad Xf,Man diesel na mengine ila kwetu Tanzania Scania ndio truck inayoongoza hasa ukizingatia upatikanaji wa vipuri na matunda makenika wengi wanafikiria sana,ila kama unaanza usikimbilie trucks za G Au R series Euro 5,yavuta truck ya Euro 2-3 ndio utapasua kichwa sana
imekupata boss
 
"Kwa hiyo bado unajichanganya. Tandem na Kipisi ni gari mbili tofauti".

Mkuu Pellman , tandem ni jina lililotokana na mpangilio(idadi) ya ekseli za nyuma...
Tandem ni lorry lenye double diff na lazima iwe na leaf spring,zipo lorry zenye diff moja ila ina axle nyingine yenye kutumia airbags hiyo axle ya nyuma inaweza kunyanyuliwa ikawa inatumika moja yenye diff Hiyo inaitwa tag axle
 
Siyo lazima iwe na leaf spring boss! Mbona kuna vipisi vingi tu ambavyo ni double diff na vina airbags kwenye diff zote..
 
Sio lazima iwe leaf spring, Kuna tandem tele zipo kwenye airbags
 
Tandem na kipisi sio majina rasmi ya aina za truck bali ni "slang" zinazotumiwa kurahisisha maisha.

Tunazoita SINGLE ni 10tons truck iwe fuso isuzu man etc zinakuwa na exel mbili with 18000 gvm

Waafrika tuna akili za kurekebisha hivyo kwa upande wa 10tons truck huwa tunaongeza exel ili kubeba zaidi so unakuta fuso isuzu hino za tani 10 zimeongezwa exel zinabeba tan 16 na tunaziita TANDEM

Tunazoziita KIPISI kitaalam hujulikana kama 15tons truck iwe ni scania, volvo, man etc na ni kawaida kuwa na exeli tatu with 26000 gvm.

Tunazoziita MENDE huwa na exeli nne with 32000 gvm 20tons truck. Ukisikia mtu anataka MENDE it means ana mzigo unaozidi 16tons
 
Vyuma....
Pic_1609661192934.jpg
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom