TRL ngoma nzito

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,783
JITIHADA za Serikali kutaka kuzima mgomo kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), unaweza kugonga ukuta endapo madai yao hayatashughulikiwa haraka.

Utata huo umejitokeza leo asubuhi baada ya wafanyakazi hao kuandamana hadi katika ukumbi wa Kapuya huku wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Kati ya mabango hayo moja lilisomeka kuwa 'JK nchi imekushinda achia ngazi wengine washike usukani maana unalea ufisadi TRL ni rushwa tupu'.

Wakizungumza na gazeti hili wafanyakazi hao wamedai kuwa wamechoshwa na kitendo cha kila mara kudai mishahara yao kwa nguvu.

Wamedai kuwa hivi sasa wamechoka kuendelea na kazi katika kampuni hiyo hivyo wanachoiomba Serikali ni kulipwa haki zao kutoka TRC na haki zao zote.

"Sasa tumechoka kuendelea na kazi tunaiomba Serikali itangaze ajira mpya kwa wafanyakazi zaidi ya 300 kutoka India na sisi tutarudi kijijini kulima nyanya, " amedai mfanyakazi mmoja ambaye hakupenda kuandikwa jina lake gazetini.

Wamedai kuwa hadi leo ni Februari 10, hawajalipwa mishahara na wafanyakzi wengi hutumia usafiri wa daladala jambo ambalo linawawia vigumu kuweza kumudu gharama za matumizi nyumbani na ofisini.

"Asubuhi nalazimika kula pamoja na mchana na nyumbani pia lazima niache pesa za matumizi achilia mbali nauli ya watoto shule kila siku kwa kweli hatuwezi kumudu gharama hizi ni kubwa tunaomba tulipwe mishahara yetu, " amedai mfanyakazi mwingine.

Pia wafanyakazi hao walikuwa na mabango mengine yaliyosomeka kuwa 'Rushwa inaiangamiza nchi yetu, tunataka pesa zetu'

Bango lingine lilisomeka 'Serikali kuvunja mkataba TRL ni kuvunja uhusiano na India? Na Mtanzania aliyechinjwa India ni kudumisha uhusiano ?

Jana Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi (TRAWU), Sylvester Rwegasira alida kuwa tayari hundi za mishahara ya wafanyakazi hao imesainiwa na Hazina hivyo kuna uwezekano wa mishara hiyo kuanza kulipwa jana.
 
Back
Top Bottom