G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,591
- 36,004
Ni aibu kwa serikali ya Tanzania kushikilia misimamo inayominya haki za waziwazi kwa manufaa ya Chama Cha Mapinduzi kwa vigogo wake huku Watanzania wa kawaida wakiendelea kuishi kwa ufukara.
Ni wazi kuwa watanzania wengi ni masikini sana na kwakweli fedha za ndani haziwezi kutekeleza hata nusu ya mahitaji muhimu ya nchi. Tunatakiwa kuheshimu haki za kila raia, kulinda uhuru wa kila mmoja na kutoa maisha bora kwa kila mmoja wetu.
Kushikilia misimamo hususani ya uchaguzi ambao uligubikwa na kuminywa kwa haki kusiko kawaida kule visiwani Zanzibar na kuwatia wale wanaokosoa mwenendo wa serikali pale inapokosea hatiani kwa kuitazama sheria mbovu ya makosa ya mitandao ambayo imegeuka na kuwa mtaji kwa CCM ni mambo ambayo tunatakiwa kuyarekebisha na kusimamia haki bila hata ya kushauriwa na mtu wa nje! Hayo ni mambo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na taifa lolote lile lililojitangaza kuwa ni taifa huru!
Leo bodi ya MCC inatushauri kufanya mambo ya muhimu kama hayo ili tupate fedha! Hii ni dalili kuwa bado hatujaweza kuwa taifa kamili! Kweli tulihitaji kushauriwa tena kwa kupewa zaidi ya trilioni moja Tshs kwa mambo yenye faida kwetu kwa mustakabali wa haki ya kila raia wa Tanzania?
Pengine Donald Trump aliposema kuwa "Nadhani kuwa Afrika bado haijaweza kujitawala" aliona mbali! Vyama vinavyotawala Afrika vinajigeuza kuwa vyama dola na ndivyo vinavyotakiwa kutunga sheria zote kwa maslai yao bila kuulizwa.
Pale tunapoambiwa kuwa tumekosea tujirekebishe tena kwa kuahidiwa misaada ya kijamii tunajibu kwa kujiamini kuwa tunaweza kujitegemea! Ukitoka mita chache tu kutoka miji mikuu ya nchi unajiuliza huwa tunajiamini nini hasa?
Hatimaye MCC imeendelea kuikazia Tanzania na sasa imeiomba Marekani kutoa mbinyo zaidi kwa Tanzania kufuata haki na misingi ya utawala bora!