Tribute to Silent Heroes!. Hongera “Idara” Kuhudumia Wastaafu Wake Till Death!”. Jee Huu Sio Ubaguzi?. Why Only Some are Cared to Death but not All?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,440
113,449
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili iliyopita.
Hongera Idara Kuhudumia Wastaafu wake..png

Naendelea na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", leo ikiwa ni makala ya Tribute to certain Silent Hero, na kuipongeza “Idara” kwa kuwahudumia wastaafu wake hadi mwisho!” kifoni, lakini nina swali, nikiamini watumishi wote wa serikali ni sawa, na wastaafu wote wa serikali wako sawa na wanastahili kuwa treated equal, sawa sawa, kwanini wengine walipwe mafao makubwa manene manono, na kuhudumiwa hadi kifoni, huku wengine wakilipwa mafao madogo, kiduchu membamba na siku wakifa, huachiwa familia zao tuu kupambana na hali zao?. Kama wastaafu wote wa serikali ni sawa, they are supposed kuwa treated equal, kwanini Serikali yetu sikivu, isiwahudumie Mashujaa wake wote kwa sawa sawa kwa haki sawa?.

Kwa vile tulirithi sheria zetu zote, taratibu na kanuni toka kwa wakoloni, na wakoloni walitumia mfumo wa indirect rule, kuwagawa ili uwatawale, vivyo hivyo kwenye utumishi wa umma, walipanga madaraja kwa ubaguzi kuwabagua wengine kwa kuwapa umuhimu, kuwajali hadi siku wanakufa serikali inagharimia, halafu kuna wengine, inawaacha wapambane na hali zao!, huu sio ubaguzi?. Kama ni ubaguzi ambao serikali yetu imeurithi toka kwa wakoloni wazungu, jee kuna haja ya kuuendeleza?, au ni ukweli kwa vile watu hawalingani, kuna wastaafu wengine ni muhimu kuliko wengine hivyo they deserves some preferential treatment hadi siku ya kifo, serikali inagharimia hadi mazishi halafu wale wasio muhimu, kuachwa kujifia na familia zao kuachiwa kupambana na hali zao?.

Ushujaa ni kitendo cha kufanya jambo kubwa kwa taifa lako. Mashujaa hawa wako mashujaa wa aina mbili, mashujaa wa wazi, Open Heroes, na Mashujaa wa Kimya, “Silent Heroes”. Mashujaa wa wazi ni wale wanaotambulika na kutambulishwa rasmi kuwa ni mashujaa, kama wale mashujaa wa majeshi yetu, ya JWTZ, Polisi, Uhamiaji, Magereza na Zimamoto, ambao huvishwa nishani za ushujaa, wazi wazi huku vyombo vya habari vikialikwa. Lakini mashujaa wa "Idara" wenyewe pia wanavishwa nishani, ila wanavishwa kimya kimya.

Jumamosi iliyopita, tarehe 05/02/2022, katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo Moshi, mmoja wa mashujaa hawa, “silent heroes” wa "Idara", kwa jina la Graciana Morris Kundi, amehifadhiwa katika nyumba yake ya milele, baada ya kufariki dunia, akiwa na umri wa miaka 86.

Kufuatia unyeti wa "Idara" japo sijui Graciana Morris Kundi, alifanya ushujaa gani, ila Mwaka 1985 alitunukiwa nishani na rais Nyerere, kisha mwaka 1991 akatuukiwa tena nishani nyingine na rais Mwinyi.

Graciana Morris Kundi, alizaliwa tarehe 30/09/1936 katika kijiji cha Iwa Kirua Vunjo, Mosh. Kati ya 1944-1949, alipata elimu ya Msingi, shule ya Iwa. Mwaka 1950-1954 - akaendelea na masomo ya sekondari Ndala, Kipalapala Tabora. 1955-1958 akajinga Tabora Girls. Mwaka 1960 akajiunga na Chuo cha KNCU kusomea kozi ya Stenograph. Mwaka 1961, aliajiriwa rasmi serikali, na kufanya kazi hadi kustaafu mwaka 1992, ikiwa ni amelitumikia taifa kwa miaka 41.

Baada ya kustaafu, alirudi kijijini, Kirua Vunjo Moshi, na kuishi maisha ya kawaida hadi mauti yalipomkuta, Jumatano ya tarehe 02/02/2022 kwa kufariki akiwa usingizini na kuzikwa Jumamosi ya tarehe 5/2/2022 kwenye shamba lake, kijijini kwake Uparo Kirua Vunjo Moshi.

Japo huko nyuma, nimewahi kuilaumu "Idara" kwa haya TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! lakini kwa hili la Idara kundelea kuwajali watumishi wake wastaafu miaka yao yote ya maisha yao, hadi kifoni, Idara inastahili pongezi, kwani baada ya Idara kupokea taarifa ya kifo hicho, maofisa wa Idara, walifika nyumbani na kutoa rambirambi kubwa nene ya kutosha kugharimia mazishi.

Kama nilivyosema, sikuujua ushujaa wa mama huyu zaidi ya kuvishwa Nishani na Rais Nyerere na rais Mwinyi. Kikawaida majeshini, wale wanaovishwa nishani ni maofisa wa ngazi za juu. Wale maofisa wa ngazi za chini, huvishwa nishani na wakuu wa vikosi vyao. Hivyo Graciana Morris Kundi, itakuwa ni alikuwa ofisa wa juu wa idara ila hadi kifoni, sikuwahi kumjua alikuwa nani.

Kwa vile nimetokea kufahamu kiwango cha pensheni aliokuwa akilipwa, na kwa vile nayafahamu mafao ya kisasa ya viongozi wakuu wanapostaafu, hulipwa asilimia 80% ya mshahara wa ofisa aliye madarakani, hivyo wastaafu hawa, waliolitumikia taifa miaka yao yote, nao wana haki ya pensheni zao zipangwe kwa asilimia, ili mishahara ya ofisa wa ngazi yake ikipanda, na pensheni za wastaafu hawa nazo zipande. Mwalimu Nyerere aliamini katika falsafa ya binadamu wote ni sawa, na baada ya kuwa rais wa Tanzania, akakuta jinsi mshahara wake ulivyokuwa juu kulinganisha na wengine, aliupunguza mshahara wake ili kujenga usawa.

Kama ni kweli binadamu wote ni sawa, hivyo maofisa wa ngazi zote za serikali ni sawa na wanastahili kutendewa sawa. Iwaje maofisa
wakuu tuu ndio wanajipangia mafao makubwa, manene, manono ya kustaafu kwa kiwango cha asilimia 80% ya ngazi husika, halafu kwanini wastaafu wengine, wa zamani, wanalipwa mafao madogo, kiduchu ajabu?. Kama ni kweli tunamuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwenye usawa wa binadamu, maofisa wote wa serikali, wanapaswa kutendewa haki sawa na wengine, na sio haki kwa maofisa wakuu tuu halafu wengine, kuachwa kupambana na hali zao, huu ni ubaguzi!.

Nimeipongeza Idara kwa kuwajali Wataafu wake sio tuu kwa kuendelea kuwalipa maisha yao yote, toka uhai, hadi kifoni, kwanini ni baadhi tuu ya wastaafu na sio wote?. Wastaafu wengine wanaojaliwa na serikali hadi kifoni, ni majaji wastaafu, na hili la majaji pia niliwahi kulizungumzia humu Hongera Jaji Mkuu kutumia uadilifu wa kaisari, kwanini Majaji wastaafu hawatibiwi?, wanasubiriwa wafe tuu? na sio mahakimu au watumishi wengine wa mahakama, swali ni kwanini, baadhi tuu ndio wajaliwe hadi kifoni, lakini wengine waachwe wajifie na hali zao?, Huu sio ubaguzi fulani hivi?.

Watu wanapojiunga na idara fulani ya serikali, na kuitumikia serikali maisha yao yote hadi kustaafu, kitendo tuu cha kufanya kazi serikalini maisha yao yote, na viwango duni vya mishahara ya serikali, hilo pekee tuu ni ushujaa. Hivyo watumishi wote wastaafu wa serikali, ni mashujaa kimya, “silent heroes”, kama walijitoa kuitumikia serikali maisha yao yote, japo wanalipwa pensheni kiduchu, lakini inapofika kifoni, serikali, inyooshe mkono wake kuwajali hadi kifoni katika safari yao ya mwisho.

Kuna msemo usemao, “mwana wa nyoka ni nyoka”, I has happened wazazi wangu wote wawili walikuwa wanafanya kazi ofisi moja, hivyo kwa watu wanao nifahamu mimi Pascal Mayalla, kama mwanahabari jasiri, asiyeogopa, kumuuliza kiongozi yoyote swali lolote, ujasiri huo nimeurithi kutoka kwa Silent Hero huyu, Graciana Morris Kundi, kwasababu huyu ni mama yangu mzazi!. Kwa Baba Mzee Andrew Mayalla (RIP), kwake nimerithi tabia zake nzuri fulani za Kisukuma ambazo naomba nisizitaje hapa maana....
Kwasababu enzi hizo recruitment ilikuwa inafanywa kwa walio in service kupeleka majina ya watoto wao kuwa recruited, sisi tumezaliwa 8, we can't all be recruited, mimi najizungumzia mimi kuwa I'm not, ila kitu nilichonacho ni intelligence mind ya kwenye damu, hivyo vitu ninavyoshaurigi humu, kama ushauri huu Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya? visipuuzwe!.

Kwa niaba ya Familia ya Shujaa huyu mwanamke,
SHUKRANI

Shukrani .jpeg

Wasalaam.

Paskali
 
Pole sana baba mkwe kwa kuondokea na mama yako mpendwa, kachelo mbobezi kundi.

Ni dhahiri sasa vyama vya wafanyakazi vipambanie 80% ya mtumishi baada ya kustaafu.
 
Pole kwa kufiwa na mama, hiyo pensheni ya viongozi wakuu wastaafu wanaolipwa 80% ya mishahara ya walioko ofisini ni uonevu na unyonyaji.

Haiwezekani hawa wafanyakazi wengine waliochangia kulitumikia taifa watengwe kwenye pensheni halafu pawepo na kikundi fulani cha wachache wanaofaidi nchi, hii keki ya taifa inayotengenezwa na wote lazima iliwe na wote pia.
 
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili iliyopita.
View attachment 2116923
Naendelea na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", leo ikiwa ni makala ya Tribute to certain Silent Hero, na kuipongeza “Idara” kwa kuwahudumia wastaafu wake hadi mwisho!” kifoni, lakini nina swali, nikiamini watumishi wote wa serikali ni sawa, na wastaafu wote wa serikali wanapaswa kuwa sawa, kwanini wengine walipwe mafao makubwa manene manono, na kuhudumiwa hadi kifoni, huku wengine wakilipwa mafao kiduchu membamba na siku wakifa, familia zao huachwa kupambana na hali zao?. Kawa wastaafu wote wa serikali ni sawa, kwanini Serikali yetu sikivu, isiwahudumie Mashujaa wake wote kwa haki sawa?.

Kwa vile tulirithi sheria zetu zote, taratibu na kanuni toka kwa wakoloni, na wakoloni walitumia mfumo wa indirect rule, kuwagawa ili uwatawale, vivyo hivyo walifanya kwenye utumishi wa umma, kuwabagua wengine kwa kuwapa umuhimu, kuwajali hadi siku wanakufa serikali inagharimia, halafu kuna wengine, inawaacha wapambane na hali zao!, huu sio ubaguzi?. Kama ni ubaguzi ambao serikali yetu imeurithi kwa wakoloni wazungu, jee kuna haja ya kuuendeleza?, au ni ukweli kuna wastaafu wengine ni muhimu kuliko wengine hivyo they deserves un equal treatment, wale muhimu kuhudumiwa hadi kifoni, wale wasio muhimu, kuachwa kujifia na kupambana na hali zao?.

Ushujaa ni kitendo cha kufanya jambo kubwa kwa taifa lako. Mashujaa hawa wako mashujaa wa aina mbili, mashujaa wa wazi, Open Heroes, na Mashujaa wa Kimya, “Silent Heroes”. Mashujaa wa wazi ni wale wanaotambulika na kutambulishwa rasmi kuwa ni mashujaa, kama wale mashujaa wa majeshi yetu, ya JWTZ, Polisi, Uhamiaji, Magereza na Zimamoto, ambao huvishwa nishani za ushujaa, wazi wazi huku vyombo vya habari vikialikwa. Lakini mashujaa wa "Idara" wenyewe pia wanavishwa nishani, ila wanavishwa kimya kimya.

Jumamosi iliyopita, tarehe 05/02/2022, katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo Moshi, mmoja wa mashujaa hawa, “silent heroes” wa "Idara", kwa jina la Graciana Morris Kundi, amehifadhiwa katika nyumba yake ya milele, baada ya kufariki dunia, akiwa na umri wa miaka 86.

Kufuatia unyeti wa "Idara" japo sijui Graciana Morris Kundi, alifanya ushujaa gani, ila Mwaka 1985 alitunukiwa nishani na rais Nyerere, kisha mwaka 1991 akatuukiwa tena nishani nyingine na rais Mwinyi.

Graciana Morris Kundi, alizaliwa tarehe 30/09/1936 katika kijiji cha Iwa Kirua Vunjo, Mosh. Kati ya 1944-1949, alipata elimu ya Msingi, shule ya Iwa. Mwaka 1950-1954 - akaendelea na masomo ya sekondari Ndala, Kipalapala Tabora. 1955-1958 akajinga Tabora Girls. Mwaka 1960 akajiunga na Chuo cha KNCU kusomea kozi ya Stenograph. Mwaka 1961, aliajiriwa rasmi serikali, na kufanya kazi hadi kustaafu mwaka 1992, ikiwa ni amelitumikia taifa kwa miaka 41.

Baada ya kustaafu, alirudi kijijini, Kirua Vunjo Moshi, na kuishi maisha ya kawaida hadi mauti yalipomkuta, Jumatano ya tarehe 02/02/2022 kwa kufariki akiwa usingizini na kuzikwa Jumamosi ya tarehe 5/2/2022 kwenye shamba lake, kijijini kwake Uparo Kirua Vunjo Moshi.

Japo huko nyuma, nimewahi kuilaumu "Idara" kwa haya TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! lakini kwa hili la Idara kundelea kuwajali watumishi wake wastaafu miaka yao yote ya maisha yao, hadi kifoni, Idara inastahili pongezi, kwani baada ya Idara kupokea taarifa ya kifo hicho, maofisa wa Idara, walifika nyumbani na kutoa rambirambi kubwa nene ya kutosha kugharimia mazishi.

Kama nilivyosema, sikuujua ushujaa wa mama huyu zaidi ya kuvishwa Nishani na Rais Nyerere na rais Mwinyi. Kikawaida majeshini, wale wanaovishwa nishani ni maofisa wa ngazi za juu. Wale maofisa wa ngazi za chini, huvishwa nishani na wakuu wa vikosi vyao. Hivyo Graciana Morris Kundi, itakuwa ni alikuwa ofisa wa juu wa idara ila hadi kifoni, sikuwahi kumjua alikuwa nani.

Kwa vile nimetokea kufahamu kiwango cha pensheni aliokuwa akilipwa, na kwa vile nayafahamu mafao ya kisasa ya viongozi wakuu wanapostaafu, hulipwa asilimia 80% ya mshahara wa ofisa aliye madarakani, hivyo wastaafu hawa, waliolitumikia taifa miaka yao yote, nao wana haki ya pensheni zao zipangwe kwa asilimia, ili mishahara ya ofisa wa ngazi yake ikipanda, na pensheni za wastaafu hawa nazo zipande. Mwalimu Nyerere aliamini katika falsafa ya binadamu wote ni sawa, na baada ya kuwa rais wa Tanzania, akakuta jinsi mshahara wake ulivyokuwa juu kulinganisha na wengine, aliupunguza mshahara wake ili kujenga usawa.

Kama ni kweli binadamu wote ni sawa, hivyo maofisa wa ngazi zote za serikali ni sawa na wanastahili kutendewa sawa. Iwaje maofisa
wakuu tuu ndio wanajipangia mafao makubwa, manene, manono ya kustaafu kwa kiwango cha asilimia 80% ya ngazi husika, halafu kwanini wastaafu wengine, wa zamani, wanalipwa mafao madogo, kiduchu ajabu?. Kama ni kweli tunamuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwenye usawa wa binadamu, maofisa wote wa serikali, wanapaswa kutendewa haki sawa na wengine, na sio haki kwa maofisa wakuu tuu halafu wengine, kuachwa kupambana na hali zao, huu ni ubaguzi!.

Nimeipongeza Idara kwa kuwajali Wataafu wake sio tuu kwa kuendelea kuwalipa maisha yao yote, toka uhai, hadi kifoni, kwanini ni baadhi tuu ya wastaafu na sio wote?. Wastaafu wengine wanaojaliwa na serikali hadi kifoni, ni majaji wastaafu, na hili la majaji pia niliwahi kulizungumzia humu Hongera Jaji Mkuu kutumia uadilifu wa kaisari, kwanini Majaji wastaafu hawatibiwi?, wanasubiriwa wafe tuu? na sio mahakimu au watumishi wengine wa mahakama, swali ni kwanini, baadhi tuu ndio wajaliwe hadi kifoni, lakini wengine waachwe wajifie na hali zao?, Huu sio ubaguzi fulani hivi?.

Watu wanapojiunga na idara fulani ya serikali, na kuitumikia serikali maisha yao yote hadi kustaafu, kitendo tuu cha kufanya kazi serikalini maisha yao yote, na viwango duni vya mishahara ya serikali, hilo pekee tuu ni ushujaa. Hivyo watumishi wote wastaafu wa serikali, ni mashujaa kimya, “silent heroes”, kama walijitoa kuitumikia serikali maisha yao yote, japo wanalipwa pensheni kiduchu, lakini inapofika kifoni, serikali, inyooshe mkono wake kuwajali hadi kifoni katika safari yao ya mwisho.

Kuna msemo usemao, “mwana wa nyoka ni nyoka”, hivyo kwa watu wanao nifahamu mimi Pascal Mayalla, kama mwanahabari jasiri, asiyeogopa, kumuuliza kiongozi yoyote swali lolote, ujasiri huo nimeurithi kutoka kwa Silent Hero huyu, Graciana Morris Kundi, kwasababu huyu ni mama yangu mzazi!.

Kwa niaba ya Familia ya Shujaa huyu mwanamke,
SHUKRANI

View attachment 2116932

Wasalaam.

Paskali
pole sana ,

Mama mkwe wangu apumzike kwa amani amina. (Nilihudhuria pia mazishi)
 
Bwana Paskali, pole sana kwa msiba wa mama yako. Back kwa hoja yako, ni kweli wastaafu wengi hawatendewi haki, Nina mfano huu kwenye familia yangu; mama yangu anatoka hapo hapo kirua vunjo na alisoma kisomachi then Mandaka, Asumpta girls (weruweru ya Leo) kisha Marangu TTC. Alifaulu vizuri sana mtihani wake wa Cambridge East Africa hapo Asumpta but kwa mapenz yake akachagua ualimu pasi kuangalia pass mark zake za juu! Aliajiriwa kwenye 1967 na amefanya kazi mpaka kustaafu akiwa serikalini . Lol kwenye mafao Mbona utacheka, Yaan ile pension ya mwezi anayopewa haiwezi Hata kidogo kumtosha kuendesha maisha yake kwa ndani ya mwezi husika na mind you alistaafu akiwa afisa elimu wa wilaya!
Hivo nashauri vyama vya wafanyakazi sehemu mbalimbali ni muda wao sasa kudai mafao mazuri kama wanayopewa viongozi and may be hao wa “idara”
 
Back
Top Bottom