Tribute to Ruge Mutahaba: A smartest, strategist, silent Politician in Tanzania! Aliyebadili siasa za Tanzania

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi
Hili ni Jukwaa la Siasa na hili sio bandiko la Pole kwa kifo cha Ruge Mutahaba, bali hii ni Tribute ya mchango wa Ruge Mutahaba kwenye mapinduzi ya siasa za Tanzania, hivyo japo hakushiriki active politics alikuwa passive politician, mimi namuita Ruge Mutahaba as one of the smartest Strategists silent politician in Tanzania.

Kwenye uzi huu, tunaangazia na kuenzi mchango wa Ruge Mutahaba kwenye Siasa za Tanzania mimi nikimtambulisha kama "A Smartest , Strategists Silent Politician in Tanzania Aliyebadili Siasa za Tanzania", aliyefanya siasa za ukweli za mipango mkakati, Strategies, kwenye backstage na sio siasa open za majukwaani, ambazo sometimes sio siasa za kweli bali ni propaganda tuu zenye uongo mwingi. Ruge was always mkweli.

Ni Ruge ndie aliye introduce Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Bongo movies na kundi la the Comedy kwenye kampeni za kisiasa kwenye kampeni za Kikwete 2005.

This is a very big milestone kwenye Siasa za Tanzania, kwa sababu ndipo kampeni za kisiasa zikapata ladha mpya kuvutia vijana kushiriki Siasa.

Usikute hiki alichokifanya Ruge, ndicho kilichowafanya watu Kama Sugu, Prof.Jay na Wasanii kuingia kwenye active politics.

Hili sio bandiko la maombolezo but let's celebrate his life na mchango wake kwenye Siasa za Tanzania.

Hizi ni baadhi ya Tribute za Ruge Mutahaba kutoka kwa wanasiasa mbalimbali

Kwa maoni yangu, kama ile premises ya Clouds ilipo ni owned by Clouds na sio rented, then napendekeza azikwe pale pale nje ya Clouds pale mahali anapopark gari yake. This will be the best tribute ever Kama alivyofanyiwa Prof. Hubert Kairuki wa Mikocheni Hospital, amezikwa pale mbele ya Mikocheni Hospital.

Jee wewe unam tribute Ruge Mutahaba kwa lipi katika siasa za Tanzania?.

Ruge ni Wetu Sote
Ruge ni wa Taifa, hivyo huu ni msiba wa Taifa.
RIP, Rafiki, Mshirika, Mpambanaji na Mwana Habari Mwenzangu
Bosi Ruge Mutahaba
Paskali
 
True umeongea ukweli lakin lazima tuliobaki tujisahihishe kidogo.....

Watanzania tumekuwa tukichukiana sana tukifanyiana fitina na mengine mengi....

Wanasiasa wanatafutana kumalizana na kuwamaliza wakosoaji wake bila kujari wao watakufa na kusahau kwamba kuna Mungu....

Wafanya biashara wanafanyiana figisu figisu ili mwenzie aanguke yeye aendelee kuwa juu mfano kwenye insue ya kupotea kwa Mo kuna mfanyabiashara mkubwa alikuwa akiomba apotee jumla....

Wafanyabiashara na watu wenye makampun wanawafanyisha kazi ngumu wafanyakazi wao kwa malipo kidogo ili waendelee kuwa watumwa kwao bila kujali kwamba kuna Mungu na wote tutaenda na mali kuziacha duniani......

Angalia maisha ya wasanii walio imba zaidi ya miaka 20 maisha yao wengine wanatafuta kukodi vijigari vyetu mtaani ili wasipate aibu uko waendako halafu leo hii tunakuwa wanafiki kusema ukweli kwamba pamoja na ukweli kwamba jamaa alibuni watu waimbe ila plan yake ilikuwa jinsi gani atapiga pesa kupitia wasanii wasio na shule haya sasa kifo icho hakina saa wala dakika .....

Tuache unafiki hawa ni moja ya wanyonyaji wakubwa wa wasanii mimi uwa naumia sana kuona mtu anakufa tunajifanya kumuonea huruma wakati ukweli tunaujua

Uwa pia naumia kusikia msanii kafa halafu tunaomba michango ya hali na mali kama kwa Ngwea na Godzilla inaniuma sana....

Najua mimi pia kuna vingi nimeshafanya vibaya lakin kiukwel uwa napenda sana kuwa mkweli mimi nachukia mtu anayetumia mgongo wa mwingine hasa asiye na elimu kupiga pesa au kujipatia utajiri au kujipatia mtaji wa kisiasa uwa inaniuma sana napenda sana JUSTICE

ingawa inauma kusema ukweli lakin ndio ivyo watu hawa na wengine wanaendelea wamesababisha maisha ya wasanii kuwa hivi yalivyo kwa kutumia nguvu ya media....

Wasanii wengi wanajua lakini wanakuwa wanafiki hongera kwa Lady J Dee na Platinums kwa kukubali kujitoa kusimama wenyewe maendeleo yenu tunayaona......

Ruge Mungu amlaze panapositahili
Tujiandae muda wowote tunaenda tusifanyie watu vitu vibaya tu, tusiwe na viburi, tusitumie elimu zetu kuwazamisha wasio soma tupendane.

R.I.P Ruge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jakaya Kikwete kaandika message ambayo hajawahi kuandika Kwenye kuomboleza Msiba wa Mtu yoyote kabla

Jakaya anakiri hadharan Kwenye page yake rasmi ya Instagram Kuwa Ruge Mutahaba 'KAMSAIDIA SANA' wakati wa Utawala wake Na 'BAADA YA KUSTAAFU' kwake . Ukisoma between lines hii statement ya Jakaya utajua Ruge alikuwa zaid ya Ruge Mutahaba

Jakaya kashindwa kuzuia hisia zake kufunguka lakin Mwanae Rais Mstaafu Ridh one kashindwa kuandika chochote zaid ya kuweka Picha ya maombolezo

Najua namna familia hii ya Rais Mstaafu ilivyoguswa Sana Na Msiba huu kwa Kuwa Ruge alikuwa nguzo muhimu Sana ya Utawala ule

Itatuchukua Miaka mingi Sana kupata Mtu wa Aina Ya Ruge Kwenye Tasnia ya Sanaa lakin yenye Mchango Mkubwa Sana Kwenye Utawala Na Jamii kwa jumla
 
Wanabodi
Hili ni Jukwaa la Siasa na hili sio bandiko la Pole kwa kifo cha Ruge Mutahaba, bali hii ni Tribute ya mchango wa Ruge Mutahaba kwenye mapinduzi ya siasa za Tanzania, hivyo japo hakushiriki active politics alikuwa passive politician, mimi namuita Ruge Mutahaba as one of the smartest silent politician in Tanzania.

Kwenye uzi huu, tunaangazia na kuenzi mchango wa Ruge Mutahaba kwenye Siasa za Tanzania.

Ni Ruge ndie aliye introduce Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Bongo movies na kundi la the Comedy kwenye kampeni za kisiasa kwenye kampeni za Kikwete 2005.

This is a very big milestone kwenye Siasa za Tanzania, kwa sababu ndipo kampeni za kisiasa zikapata ladha mpya kuvutia vijana kushiriki Siasa.

Usikute hiki alichokifanya Ruge, ndicho kilichowafanya watu Kama Sugu, Prof.Jay na Wasanii kuingia kwenye active politics.

Ruge ni Wetu Sote
Ruge ni wa Taifa.
RIP Mpambanaji
Ruge Mtahaba
Paskali
yeah, siasa za kuibeba CCM of course... translating into kuwabebesha Watanzania zigo la misumari!
 
Ruge Mutahaba ndio Mhasisi wa Neno Hapa Ni Kazi Tu ambalo kwa sasa hivi ni " Hapa Kazi Tu"

" Ogopa vitu viwili Mungu na Teknolojia" Ruge Mutahaba

" Kama kuna jambo unalolifanya halina Changamoto yoyote jua kuna sehemu unakosea" - Ruge Mutahaba.
 
He built the entertainment empire and used it smartly to the extent that he calmly forced those in power to come and join him. Mzee wa Fursa. Mzee wa kutafuta solutions zetu bila kulalamika lalamika.

Simjui vizuri, ila I must say I admire the way he was able to propel forward through what he was doing
 
..leo hii hao wasanii wamekuwa madodoki..wakimaliza safisha njia muda wa campaign wanatupwa kureeeeee...choka mbaya.

kwenye tasnia ya muziki na habari --aliweza ratibisha vipindi na kufanya Clouds media kuwa na mvuto kwa rika zote.....kaacha pengoo

RIP Ruge
 
Chadema watapinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma barua ya Polepole
IMG_20190227_074408.jpg
huyu alikuwa Kada wa CCM ,Chadema watapinga nini?!
 
Wanabodi
Hili ni Jukwaa la Siasa na hili sio bandiko la Pole kwa kifo cha Ruge Mutahaba, bali hii ni Tribute ya mchango wa Ruge Mutahaba kwenye mapinduzi ya siasa za Tanzania, hivyo japo hakushiriki active politics alikuwa passive politician, mimi namuita Ruge Mutahaba as one of the smartest silent politician in Tanzania.

Kwenye uzi huu, tunaangazia na kuenzi mchango wa Ruge Mutahaba kwenye Siasa za Tanzania.

Ni Ruge ndie aliye introduce Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Bongo movies na kundi la the Comedy kwenye kampeni za kisiasa kwenye kampeni za Kikwete 2005.

This is a very big milestone kwenye Siasa za Tanzania, kwa sababu ndipo kampeni za kisiasa zikapata ladha mpya kuvutia vijana kushiriki Siasa.

Usikute hiki alichokifanya Ruge, ndicho kilichowafanya watu Kama Sugu, Prof.Jay na Wasanii kuingia kwenye active politics.

Hili sio bandiko la maombolezo but let's celebrate his life na mchango wake kwenye Siasa za Tanzania.

Hizi ni baadhi ya Tribute za Ruge Mutahaba kutoka kwa wanasiasa mbalimbali

Jee wewe unam tribute Ruge Mutahaba kwa lipi katika siasa za Tanzania?.

Ruge ni Wetu Sote
Ruge ni wa Taifa.
RIP Mpambanaji
Ruge Mtahaba
Paskali
Paskali, aha tu tuomboleze kifo cha kijana wetu, rafiki yetu, baba yetu, mzazi mwenzetu, mjasiliamali , Mtazania na mzalendo wa kweli kwa yale yanayofahamika, n.k. Tukiingiza siasa hapa utaharibu msiba. Acha kabisa
 
Back
Top Bottom