Uchaguzi 2020 TRIANGLE ATTACK: Lazaro Nyalandu atikisa Singida Kaskazini, ni kama anasubiri kuapishwa tu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,572
217,937
Lazaro Nyalandu ni kama ameiua CCM Mkoa mzima wa Singida maana hata wakati Lissu akiwa nje ya nchi kwa matibabu, Mh Nyalandu aliendelea kuifyeka CCM bila huruma.

Mpinzani wake wa CCM anaitwa Ramadhan Ighondu, mtu anayetajwa bila kukanusha kuhusika na kumteka na kumtesa kinyama kiongozi wa chama cha Madaktari Tanzania, Dr. Ulimboka kwa lengo la kumuua.

Hata wana Singida wangekuwa wamelogwa na kufanywa misukule wasingeweza kuchagua mbunge wa aina ya Ighondu.

Pichani ni Mh Nyalandu akiwa kwenye kampeni jimboni kwake.

Mgombea Ubunge wa Chadema Jimbo la Singida Kaskazini, @lazaronyalandu akizungumz ( 479 X 640 ).jpg
 
CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya chakula, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom